Nimeamua kufanya maendeleo ya kujengea nyumba 90% ya mshahara . Hakuna mjadala

Ne Mbwitu

JF-Expert Member
Aug 23, 2020
275
802
Nimeamua kujaribu kufanya maendeleo ya kujengea nyumba kwa miezi mitano kwa kutumia asilimia 90 ya mshahara wangu. Hoja hii ya maendeleo haina mjadala.

Watoto watapikiwa ugali na kachumbari mwanzo mwisho. Watoto wakifukuzwa shule kwa sababu ya ada warudi wakae nyumbani. Atakayenipinga huyo anatumiwa na majirani na maadui zangu. Mtoto atakayefungua mdomo ni kipigo kwenda mbele. Mimi ni jiweee!!!

Baada ya miezi mitano uchumi wa familia utakuwa umeongezeka, nikimaliza nyumba tunahamia kwenye gari....

Maendeleo ya vitu hoyeee
 
Kipindi hiki cha uchaguzi kampeni zimeruhusiwa rasmi, punguzeni kuandika kwa kukonekti dotsi jamani mweeeh....!!!

Mi sijaelewa hata kidogo zaidi ya kuishia kupasuka mbavu, ukiniuliza kinachonchekesha sina jibu. 🤣🤣🤣🤣🤣

K’ Matata.
 
Wanachama wenzio wanaweza wasikuelewe ila kwakuwa umeweka neno "kokoto", wataunganisha vinukta na pengine kuelewa kuwa kampeni zimeanza.
 
Kipindi hiki cha uchaguzi kampeni zimeruhusiwa rasmi, punguzeni kuandika kwa kukonekti dotsi jamani mweeeh....!!!

Mi sijaelewa hata kidogo zaidi ya kuishia kupasuka mbavu, ukiniuliza kinachonchekesha sina jibu. 🤣🤣🤣🤣🤣

K’ Matata.

Duh aisee, unajua wanaume tukisifia demu ana K Matata tunamaanisha nini..??
 
Nimeamua kujaribu kufanya maendeleo ya kujengea nyumba kwa miezi mitano kwa kutumia asilimia 90 ya mshahara wangu. Hoja hii ya maendeleo haina mjadala.

Watoto watapikiwa ugali na kachumbari mwanzo mwisho. Watoto wakifukuzwa shule kwa sababu ya ada warudi wakae nyumbani. Atakayenipinga huyo anatumiwa na majirani na maadui zangu. Mtoto atakayefungua mdomo ni kipigo kwenda mbele. Mimi ni jiweee!!!

Baada ya miezi mitano uchumi wa familia utakuwa umeongezeka, nikimaliza nyumba tunahamia kwenye gari....

Maendeleo ya vitu hoyeee
kupanga ni kuchagua
 
Yaani unaamini lissu akiingia madarakani ndio utapa mehela na maisha yako yatakuwa mazuri. Hivyo sana. Fanya kazi kijana.
 
Hawa wafuasi wa Lissu wanatoka mikoa gani? Kwa akili hizi za kufikiria atawaletea hela, wali, nyumba wao wakiwa hawafanyi kazi sababu Lissu rais pumbafff.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Maendeleo yalianza tangu enzi za mwl na yataendelea awamu hata awamu.. Acha watoto wale kuku kwa mrija eboh!
 
Back
Top Bottom