Nimeamua kuchukua fomu CCM kwa sababu zifuatazo

mendz

Senior Member
Dec 9, 2013
144
49
Nimeamua kuchukua fomu CCM kwa sababu kwa mtazamo wangu wagombea wote hawafai kwa sababu zifuatazo:

Mimi niko kwenye 50s kwa sasa. Wagombea wengi waliochukua fomu ni wale ambao walikuwepo tangu enzi ya Mwalimu hivyo wanastahili kupumzika kwa kazi kubwa walioifanya tangu tupate uhuru mpaka leo. Inabidi wajifunze umuhimu wa kung'atuka kwa maslahi ya taifa letu. Wengine ni wezi tu na waongo. Tunawavumilia kwa sababu sisi si watu wa visasi. Tuko tayari waliibie taifa hili lakini si katika ngazi ya Urais.

Kundi lingine ni kundi la vijana ambao wako kwenye 40s. Hawa wamekuja juzi tu kwenye chama tumewakaribisha sasa kuwakabidhi madaraka ndani ya chama na Serikali wasijione wana haki ya kuchukua nafasi kuu ndani ya chama na Serikali. Wasubiri mda wao utafika tu. Wawe na subira.

Kwa hiyo katika wagombea wote tumebaki wawili ambao umri wetu ndio pekee wenye haki ya kuwa marais ndani ya CCM. Mimi na Makongoro.

Namalizia hoja yangu kwa ujumbe huu ufuatao kwa mpinzani wangu:

https://www.youtube.com/watch?v=yaZ3RHCZauQ
 
Back
Top Bottom