Nimeamua kuanza kujifunza computer programming (back end development)

Mkuu, ili uweze kujifunza Programming vizuri inabidi ujue ni kitu gani unataka kukitengeza kwa muda huo maana mambo ni mengi sana na ni ngumu sana kujua kila kitu. Hizi languages ni kama tools za kutusaidia kutatua tatizo letu tulilonalo. Cha msingi jitahidi uweze kumaster japo lugha mbona. Wabongo wengi ni Jack of all trades, master of none. We piga code tu. Ukiweza nunua course za Udemy zipo vizuri mno
Ninaomba kuuliza kusoma udemy kozi kwa kulipia faida yake ukilinganisha na kusoma bure. Vipi vya ziada unapata ukilinganisha ukiangaika na tutorials?
 
Komaa na kitu kimoja, kielewe vizuri, ukirukaruka utaishia kua shallow pote.
Personally sipendi php na javascript, napenda static typed languages, javascript nafanya kwa kua tu web frontend hakuna choice nyingine zaidi ya hiyo, nadhani kila developer ni muhimu ajue javascript, php naichukia, language ya kijinga sana hata aliyeitengeneza anajua kua php is shit, ila kwa market ya bongo wengi wanatumia.
kwanini unaichukia sana php mkuu
 
Hapo ulipo kwenye PHP nenda nayo tu maana ulishaianza, PHP ya leo 7.3 ni nzuri sana, wameboresha mambo mengi sana, isome na ufanye lots of practice, japo pia pembeni unaweza ukawa unajifunza na Javascript pia, haikwepeki likija suala la web development, ila kwa zote hakikisha umeanza na core languages zenyewe kabla framework yoyote.
Cha msingi kwa chochote utakachokifanya, usiwe na pupa au haraka ya kutaka kumaliza, tumia muda wako na nguvu nyingi, kuwa mvumilivu hatimaye utashinda.
asante kwa ushauri mzuri nitaufanyia kazi kikamilifu kwa uwezo wa mungu, kama unafahamu resorce nzuri za kujifunza na kupractice php naomba unisaidie pia,
 
kwanini unaichukia sana php mkuu

Ina performance mbaya alafu ilitengenezwa ovyo ovyo.

Mfano methods za php naongelea core achana na libraries, unakuta method nyingine zinatumia camelCase, huku method nyingine zinatumia under_score, unakuta method nyingine zimeandikwa kijinga hadi unacheka camelCase_under_score. Ukiwa unatengeneza software unatakiwa kufuata style moja when it comes to naming things sio unachanganya changanya ovyo bila sababu yoyote, inaonyesha php imetengenezwa na watu kibao ambao walikua hawawasiliani au aliyekua anafanya code review alikua anapitisha ovyo tu bila kujua style wanayotumia ni ipi.

Ni 2019 multicore CPUs zimekuwepo for a whole decade now, kutumia cores zote za CPU kwa kutumia php unaweza lia, concurrency ni mbaya kupita kiasi, kama hutumii load balancer on top ispin up new threads kuserve requests umeumia, php yenyewe haikutengenezwa for concurrency, ni ya zamani enzi hizo kila kitu ni single core tu. Language nyingi sana zinaperform better than php, hata node ambayo pia siipendi inajitahidi kuhandle concurrent tasks kuliko php.

Sababu ya kutumia php mwaka huu imebaki tu kua php inatumika kwenye websites nyingi sana, ni moja ya languages ambazo zilipata adaptation kubwa mno wakati zinatoka, tofauti na hapo hakuna faida nyingine yoyote ile. Jaribu kusoma language kama Rust, Golang kwa backend uone kama utarudi kugusa php.
 
Mbona node ipo vizuri tu mkuu.
 
Mbona node ipo vizuri tu mkuu.

Node.js runtime environment ni nzuri sana, yaani tangu nianze kuitumia sijawaza kingine chochote, ilivyo fast haswa kwa kutumia uwezo wake wa non-blocking na pia uwezo wa kuengeneza web server yako mwenyewe, na zaidi uwezo wa kutumia technology moja ya Javascript both fronted and backend.
Halafu ilivyo na wingi wa packages, leo hii kuna zaidi ya 500,000 freely available packages.
 
Mbona node ipo vizuri tu mkuu.

Kwa kazi unazofanya, ila kuna kazi ambazo kufanya kwa node ni kulazimisha tu, software zinazodeal na calculations kibao au highly concurrent applications ni uvivu kutumia node coz itakua na performance mbaya.
 
Kwa hiyo mkuu Graph wewe kwenye kazi zako unapendelea sana kutumia programming language zipi???
 
Kwa hiyo mkuu Graph wewe kwenye kazi zako unapendelea sana kutumia programming language zipi???
Kwenye hesabu na ufanisi wa hali ya juu utahitaji lugha zinazo support angalau concurrency. Node ni single threaded. So hapo ni lugha kama C++, Erlang/Elixir, Golang et al
 
Daaaaah you have said the "HARD TRUTH"

Mimi nko na experince ya mda mref sana na php na niliipenda php coz nilianza kuisoma nikiwa form 2 kipindi ambacho bado nalazimishwa kusoma masomo mengine kama history na kiswahili, ila kwa wepesi wa php niliweza kuisoma na kuimaster huku nasoma masomo ya shule.

My point is, Php ni nzuri kusoma kama uko na vitu vinakubana sana lkn bado unapenda programming coz iko simple na straight forward na itakuingiza katika ulimwengu wa webservers na internet na kukufanya angalau uelewe concepts ndg ndg kama vle COOKIES, CACHES, REQUEST_METHODS, ENCODING, DECODING etc... Ambazo sasa ukishakua free kufanya programming tu ndipo utaanza kujifunza lugha nyngne na itakua rahisi ww kuzimaster coz tyr zle concepts ndogo ndogo unazielewa.

Mie ni shahidi wa hili coz baada ya kuelewa kiundani kabisa php na kucheza nayo kwa miaka kadhaa imenifanya niwe flexible kujifunza technology yyt ile coz rules nyingi za php zipo katika languages nying. Mfano kipind naanza kabisa kujifunza programming(as a kid) Kuna jamaa alikua anatoa tutorial ya Object Oriented Programming kwa Java, kiukweli jamaa sikumuelewa hadi nikaona OOP ni ngumu na nikaacha Kusoma java. But baada ya kufahamu kwamba kuna php, nilikaa mda mrefu natumia Proceudral php coz nlikua nmekariri OOP ni ngumu, but one day nikakutana na tutorial fln ya OOP kwa php, U cant Imagine I saw it very simple. Na hapo ndipo nkaanza kupiga Java, C++, Android dev na any technology inayokuja nakua niko flexible kujifunza

Learning Programming is just about getting a right base(foundation) suiting your Learning curve.
asante kwa inspiration, coz my point is to become software developer so nilikuwa nataka nianze na kitu ambacho hakitanikatisha tamaa then baada ya kuwa comfortable ndio nianze kupambana na lugha nyingine ambazo kwangu naziona ngumu kidgo like JAVA
 
Kwa hiyo mkuu Graph wewe kwenye kazi zako unapendelea sana kutumia programming language zipi???

Rust, C++, Golang. Kazi zangu nyingi zinahitaji very high performance, hizi ndo language tatu nazocheza nazo kila siku.
 
Kwa front end development tafuta kitabu kilichoandikwa na Jon Duckett HTML & CSS Kizuri mno haitaji sana kusaidiwa na mtu nilianza kujifunza mwenyewe kupitia kitabu chake kwakweli utakipenda
 
Wadau kama kichwa cha habari kinavyojieleza!! Nimeamua kwa moyo mmoja kuanza jifunza programming na sasa nimeanza na PHP katika back end!!

Naombeni ushauri wenu, je nisome vipi ili niweze kui master hii language? Je ili niwe developer mzuri nini nisome nini baada ya hii php??

Je soko la php kwa bongo likoje??

Je ni challenge zipi programmers mnzipata kwenye kazi zenu za kila siku?

NB: Napenda computer na Malengo yangu ni kuijua php na web development kwa ujumla!!

Na nna basics za css na html.

Karibuni kwa mawazo yenu katika hii safari kujifunza!
Jifunze php ufanye kazi. Mengine utajifunza when you need to. Nawajua watu wanajua ma c++, python, Golang.. Ila unakuta mtu akipata bug anachukua wiki kusolve kisa hakuna community nzuri, leo hii ukipata tatizo lolote la php unapata suluhisho la haraka na kazi zinaendelea.. I love php when you only need to get the job done na hauangalii sana mambo ya performance.. Ila kama unaandika software yenye processing nyingi its not advised.

Mara nyingi mature programmers tunasahau kwamba beginners jus want a place to start. Kwa ushauri wangu php ni kianzio kizuri sana kwa backend web development maana ata sehemu za kuhost zipo nyingi..tofauti na language zingine.. almost every server has a LAMP stack. Endelea na php mkuu.. Master it and then think about upgrading later.. For now don't stress about performance.

As Zuckerberg would say.. Code now, Fix later.
 
mimi pia natumia node.js mkuu hakika ipo vizuri mnooo
Node.js runtime environment ni nzuri sana, yaani tangu nianze kuitumia sijawaza kingine chochote, ilivyo fast haswa kwa kutumia uwezo wake wa non-blocking na pia uwezo wa kuengeneza web server yako mwenyewe, na zaidi uwezo wa kutumia technology moja ya Javascript both fronted and backend.
Halafu ilivyo na wingi wa packages, leo hii kuna zaidi ya 500,000 freely available packages.
 
Asante kwa kuniita huku, huwa nahisi fahari sana pale natoa mchango wangu kuwasaidia wanaoanza mambo haya.

Kwa sababu unasema tayari umejifunza CSS na HTML, nafikiri kwa wewe kuifuata PHP ni jambo nzuri. Lakini pamoja na kwamba PHP ni bora na ina mambo mengi muhimu, ila ina mapungufu fulani hususan kwa wanaonza programming. Ipo legevu sana kiasi cha kufanya uwe mzembe unapoandika codes zako. Huwa inaachia au kusamehe sana mapungufu mengi kwenye suala la umakini.

Ingekua bora ukaanza na lugha zinazohimiza umakini kama vile Java, C# au C++ halafu baada ya hapo ndio ufuate PHP. Naomba usinielewe vibaya, sipondi PHP, ni lugha ambayo naipenda sana na imenisaidia katika kutegeneza solutions nyingi na nimeitumia kwa miaka mingi sana. Kuna watu kwa unafiki wao hupenda kuiponda ilhali wanaitumia kupiga hela. Nina solutions nyingi ambazo nimetumia PHP na zinafaidi jamii.

Ni lugha yenye mambo mengi ya maana na inawezesha sana. Kwanza ukiielewa vizuri halafu ujifunze Javascript na framework yake kama JQuery, baadaye ufuate framework ya PHP kama Lavarel na pia usisahau DBMS kama MYSQL. Hapo utakua umeanza vizuri.

Zingatia nilivyo orodhesha, usianze kuingia kwenye frameworks kabla hujaelewa lugha husika. Yaani soma Javascript kabla ya kujaribu JQuery au Mootools n.k. Hakikisha umeelewa PHP vizuri kabla ya kufuata frameworks kama vile Yii, Codeignitor n.k.

Jifungie chumbani na vitendea kazi, laptop nzuri, download videos, vitabu vya PDF, IDE nzuri, ingia kwenye forums...pambana tu na kitaeleweka. Pia tafuta kitabu kinachofundisha concepts za software development cycles kwa undani. Jinsi unaweza kuangalia shida fulani kwa jamii, ukaiwazia suluhisho na kudadavua/analyse hadi upate mtiririko wake na kuitatua kwa software.

Nakutakia kazi njema....
Mkuu, nimependa vile umejibu swali.
Nadhani unaweza kunipa mwanga kidogo kwa hiki nnachotaka kujifunza.
Mie nataka kujifunza mobile app development from scrach, natakiwa nifahamu nini na nini ilhali sina ujuzi wowote wa programing zaidi ya kupenda kujifunza?!

Nimekuwa nikitengeneza native mobile apps kupitia 'appyet' na 'thunkable' lakini napenda kujua zaidi mkuu!

Msaada plz!
 
Back
Top Bottom