Nimeamua kuanza kujifunza computer programming (back end development)

Lodrick Thomas

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
1,339
2,430
Wadau kama kichwa cha habari kinavyojieleza!! Nimeamua kwa moyo mmoja kuanza jifunza programming na sasa nimeanza na PHP katika back end!!

Naombeni ushauri wenu, je nisome vipi ili niweze kui master hii language? Je ili niwe developer mzuri nini nisome nini baada ya hii php??

Je soko la php kwa bongo likoje??

Je ni challenge zipi programmers mnzipata kwenye kazi zenu za kila siku?

NB: Napenda computer na Malengo yangu ni kuijua php na web development kwa ujumla!!

Na nna basics za css na html.

Karibuni kwa mawazo yenu katika hii safari kujifunza!
 
wazo lako zuri, kuwa developer mzuri lazima ujitoe kwanza kwenye masuala ya muda, ufikiri vya kutosha,ku reason (logic) na ku attend meets up japo kuwa kwa bongo meets up sijawahi sikia kabisa au mtu anaweza jitolea ila watu wasi attend. Baada ya PHP unaweza soma tu lugha yeyote kulingana na mata
 
Nimejifunza thanks kwa mawazo yako mdau!
 
Wadau kama kichwa cha habari kinavyojieleza!! Nimeamua kwa moyo mmoja kuanza jifunza programming na sasa nimeanza na PHP katika back end!!

Naombeni ushauri wenu, je nisome vipi ili niweze kui master hii language? Je ili niwe developer mzuri nini nisome nini baada ya hii php??

Je soko la php kwa bongo likoje??

Je ni challenge zipi programmers mnzipata kwenye kazi zenu za kila siku?

NB: Napenda computer na Malengo yangu ni kuijua php na web development kwa ujumla!!

Na nna basics za css na html.

Karibuni kwa mawazo yenu katika hii safari kujifunza!
Pia katika mudaa wako wa Uhuru tafta kitabu cha hackers heroes of the computer revolution author Steve ni historia fupi kuhusu programmers wa MIT kitakupa hamasa ya kuendelea na kuelewa concept ya programming
 
Asante kwa kuniita huku, huwa nahisi fahari sana pale natoa mchango wangu kuwasaidia wanaoanza mambo haya.

Kwa sababu unasema tayari umejifunza CSS na HTML, nafikiri kwa wewe kuifuata PHP ni jambo nzuri. Lakini pamoja na kwamba PHP ni bora na ina mambo mengi muhimu, ila ina mapungufu fulani hususan kwa wanaonza programming. Ipo legevu sana kiasi cha kufanya uwe mzembe unapoandika codes zako. Huwa inaachia au kusamehe sana mapungufu mengi kwenye suala la umakini.

Ingekua bora ukaanza na lugha zinazohimiza umakini kama vile Java, C# au C++ halafu baada ya hapo ndio ufuate PHP. Naomba usinielewe vibaya, sipondi PHP, ni lugha ambayo naipenda sana na imenisaidia katika kutegeneza solutions nyingi na nimeitumia kwa miaka mingi sana. Kuna watu kwa unafiki wao hupenda kuiponda ilhali wanaitumia kupiga hela. Nina solutions nyingi ambazo nimetumia PHP na zinafaidi jamii.

Ni lugha yenye mambo mengi ya maana na inawezesha sana. Kwanza ukiielewa vizuri halafu ujifunze Javascript na framework yake kama JQuery, baadaye ufuate framework ya PHP kama Lavarel na pia usisahau DBMS kama MYSQL. Hapo utakua umeanza vizuri.

Zingatia nilivyo orodhesha, usianze kuingia kwenye frameworks kabla hujaelewa lugha husika. Yaani soma Javascript kabla ya kujaribu JQuery au Mootools n.k. Hakikisha umeelewa PHP vizuri kabla ya kufuata frameworks kama vile Yii, Codeignitor n.k.

Jifungie chumbani na vitendea kazi, laptop nzuri, download videos, vitabu vya PDF, IDE nzuri, ingia kwenye forums...pambana tu na kitaeleweka. Pia tafuta kitabu kinachofundisha concepts za software development cycles kwa undani. Jinsi unaweza kuangalia shida fulani kwa jamii, ukaiwazia suluhisho na kudadavua/analyse hadi upate mtiririko wake na kuitatua kwa software.

Nakutakia kazi njema....
 
Mimi naweza kuanza from zero kimtaamtaa nikaelewa nina knowledge kidogo sana ya programming.
 
Back end programming. Ni kitu kikubwa sanaaaa. kwa hiyo angalia unataka kufanya nini kwanza ndipo utafute language yako.

Ukisoma ohp kama php ukija kumaliza utashangaa huwezi fanya chochote. So anza na lengo. Je ninasoma php ili nifanye nini?

pia naomba tuwe connected instagram. nickyrabit ni akaunti yangu. mimi nafanya Android Applications ni vizuri nikiwafahamu na wenzangu pia. Karibu.
 
Nashukuru sana mkuu!! Ntakitafuta hicho kitabu
 
Wala nisikudanganye mkuu! Nilianza java nikaona si rafiki kwangu, ila dhumumi langu ni katika web dev...thats why i decided to take php!! Mpaka sasa naona maendeleo yangu si mabaya hasa ukizingatia ina connection na css na html ambazo tayari nna basics zake!!

Swali lingine, je kila website ni lazima utumie back end program kama php au django? Au ukitumia css na html na js unaweza kuiweka hewani??

Once again, thanks a bunch!
 
Mimi naweza kuanza from zero kimtaamtaa nikaelewa nina knowledge kidogo sana ya programming.
Mkuu unaweza unachohitaji ni passion na kujua what u want to achieve!! Unaeza enda kwenye web developent au software development we mwenyewe tu!!
 
Back end programming. Ni kitu kikubwa sanaaaa. kwa hiyo angalia unataka kufanya nini kwanza ndipo utafute language yako.

Ukisoma ohp kama php ukija kumaliza utashangaa huwezi fanya chochote. So anza na lengo. Je ninasoma php ili nifanye nini?

pia naomba tuwe connected instagram. nickyrabit ni akaunti yangu. mimi nafanya Android Applications ni vizuri nikiwafahamu na wenzangu pia. Karibu.
Mkuu nataka kusoma php ili niweze kutengeza websites na web applications! Najua ziko nyingine kama django na node js ila nimeichagua php maana kiasi flani naona naielewa kwa urahisi! Thanks mkuu
 
Bro PM namba zako kaka naona tuko sawa kiidea
 
Dah nimefurahi sana kukutana na watu wenye idea kama yangu mimi kwasasa najua juu ya HTML na CSS lakini nimekwama sijui niendelee na language gani naombeni msaada wenu
Mkuu kwa hapo ulipofikia angalia wapi unataka! Je front end au back end development!? Ukishapata jibu unaendelea!!

Ila jitahidi kufanyia mazoezi hizo languages mbili kwanza kabla huja move sehemu ingine!! Kila la kheri
 
Back
Top Bottom