Nimeamua kuachana rasmi na siasa, dini na mapenzi

love life live life

JF-Expert Member
Sep 12, 2021
2,529
2,896
Sometimes giving up is the sign of perseverance and not the sign of weakness aliandika mwandishi
wa habari mwanamama wa uingereza Reni Eddo-Lodge kwenye kitabu chake cha why i'm no longer talking to white people about race, akiwa anaelezea white supremacy and structual disadvantage of black people na nini kifanyike.

Watu wanasikia wanachokipenda na wanachotaka kukisikia iwe kwenye dini, siasa na mapenzi iko proved na wanasaikolojia to be honest sijazaliwa ku-mplease mtu yeyote hata baba yangu mzazi nilishindwa kwa mara zote nilizo jaribu, naye sitajaribu tena kum-please.

Kama alivyosema Newton "Socrate is my friend, Plato is my friend but my greatest friend is the truth", kusema ukweli katika jamii ambayo uongo na kujipendekeza ndio nguzo kuu ni kitu ambacho kimenishinda nimeamua
kukaa kimya nisiongee chochote kwani sitabadilisha chochote kwa aina ya watu kama hao sio tu wanao sujudu uongo
bali wamekuwa wakijidanganya hata wao wenyewe kwenye nafsi zao kwa mambo mengine mengi na pengine uongo mdogo umewakinai wanahitaji kudanganywa uongo mwingine mkubwa zaidi.

the first principle is that you must not fool yourself and you are the easiest person to fool, alituasa Feyman.

Sisemi nimeacha kujadili hayo mambo lakini nitajadili na open minded people ambao wamefungua mioyo yao
na akili zao na sio wale wanaojadili ili kushinda mijadala na sio kujifunza katika mijadala hiyo.

NB: unapoona jamii ina shule moja zahanati moja na makanisa 136 na hamna kiwanda chochote huhitaji kujua kuna matatizo
gani katika hiyo jamii mwenye hekima alisema.

Nimeamua kufanya hivyo sio kuwa nimekata tamaa na watu hao lakini kwa faida kubwa kwao na kwangu
kuokoa mda na nishati(to save time and energy).
 
Kimya kimya tuu hujaweza kufanya hivyo!

Na kwa nini unajihami sana, Mara ooh, sjakata tamaa n.k

Moja ya jambo naloamini, ukiwa kwenye jamii Fulani ambayo kwa mtizamo wako kuwa inaujinga Fulani unaouona wewe na wewe huna huo ujinga, maana yake wewe inakupasa uionyeshe namna inavyopaswa iwe, na usipofanya hivyo maana yake umeamua wote muwe wajinga,!!

Mungu akikupa kufahamu udhaifu wa mchungaji wako, maana yake umepewa kazi ya kumwombea na si kutoka kumsema kwa watu, haitakusaidia zaidi sana wewe utachuma dhambi na hutapata faida!!
 
Thread za namna hii zipo nyingi
Ila kubwa kabisa ni ya Bwana Mayalla
Yumo humu
Hizi ni thread naziita chai andazi
 
Pole Sana !
Hii ni baada ya kukatishwa tamaa na matarajio makubwa uliokuwa nayo!
Naamini uatapata mwelekeo mpya wa kuelekea nishati yako!!!
KILA la Heri!
 
Heart breaks zinafanya watu ku-philosophize maisha. You dont need justification, just live your life. Lay back and relax, don't take things so serious. Kunywa balimi akili ikae sawa
 
Siasa na dini sawa, ila unaachaje mapenzi mkuu? Yaani kwamba umeamua kabisa, mwenyewe bila kushurutishwa kuachana na mchakato wa kuchakata?
 
Ndugu yangu inaonekana kuna kitu unacho ambacho jamii ingenufaika kwayo lakini umeamua kukataa tamaa.
Nadhani Yesu ndio binadamu aliyepingana sana na desturi za jamii yake tafadhali kamsome na usome fumbuzi zake.
Kwangu Mimi nakupa changamoto "Je? Umeamua kuzima taa yako ili ufanane na giza?" Kama jibu ni ndio nakusihi usifanya hivyo,kama jibu ni hapana basi jifunze sana kwa Paul nabii wa mataifa alifanya kazi kubwa na ngumu sana.

Muhimu sana tambua duniani ulikuja kwa Kusudi na Kusudi lako limejificha kwenye yale yanayo kuudhi sana. Jipatie wasaa usome kwa makini nakutafakari vitabu vya maarifa na elimu ya ufahamu, Mithali, Muhubiri, Hekima ya Suleiman na Mausia ya Yoshua bin Sira. Maandishi yako yanaonesha unaweza kuwa msaada kwa jamii yako tafadhali angaza
 
Usikate tamaa mkuu ndio dunia tunayoishi..

Mpende mkeo au tafuta mmoja aliyeumbika umuoea muwe mnapapasana nakuangaliana mkiwa naked ( utafurahia maisha na utaishi maisha marefu sana)..... Wengine sisi tunao weeengi basi burudani ukiwa unaangalia maumbile yao wakiwa naked huku ukipapasa papasa...the life is good dont complicate it..

Hata mengine ya Siasa usiyachukulie serious saaana kivile, DINI ni imani hivyo ni jukumu lako kuamini au kutoamini..
 
Siasa na dini sawa, ila unaachaje mapenzi mkuu? Yaani kwamba umeamua kabisa, mwenyewe bila kushurutishwa kuachana na mchakato wa kuchakata?
Mkuu kuchakata siyo Mapenzi..kumbuka kuna Mapenzi na Ngono....Mapenzi na Ngono vinaweza kwenda pamoja na vile vile Ngono inaweza kwenda peke yake bila Mapenzi.
Hivyo anaweza kuacha Mapenzi akaendelea na Ngono.
 
Ukiwa unapenda ukweli kama ilivyosema basi huwezi ku hesitate kusema Mungu hayupo
 
Sometimes giving up is the sign of perseverance and not the sign of weakness aliandika mwandishi
wa habari mwanamama wa uingereza Reni Eddo-Lodge kwenye kitabu chake cha why i'm no longer talking to white people about race,
akiwa anaelezea white supremacy and structual disadvantage of black people na nini kifanyike.
Watu wanasikia wanachokipenda na wanachotaka kukisikia iwe kwenye dini, siasa na mapenzi iko proved
na wanasaikolojia to be honest sijazaliwa ku-mplease mtu yeyote hata baba yangu mzazi nilishindwa kwa mara zote nilizo jaribu, naye
sitajaribu tena kum-please.
kama alivyosema Newton "Socrate is my friend, Plato is my friend but my greatest friend is the truth", kusema
ukweli katika jamii ambayo uongo na kujipendekeza ndio nguzo kuu ni kitu ambacho kimenishinda nimeamua
kukaa kimya nisiongee chochote kwani sitabadilisha chochote kwa aina ya watu kama hao sio tu wanao sujudu uongo
bali wamekuwa wakijidanganya hata wao wenyewe kwenye nafsi zao kwa mambo mengine mengi na pengine uongo
mdogo umewakinai wanahitaji kudanganywa uongo mwingine mkubwa zaidi.
the first principle is that you must not fool yourself and you are the easiest person to fool, alituasa Feyman.
Sisemi nimeacha kujadili hayo mambo lakini nitajadili na open minded people ambao wamefungua mioyo yao
na akili zao na sio wale wanaojadili ili kushinda mijadala na sio kujifunza katika mijadala hiyo.
NB: unapoona jamii ina shule moja zahanati moja na makanisa 136 na hamna kiwanda chochote huhitaji kujua kuna matatizo
gani katika hiyo jamii mwenye hekima alisema.
Nimeamua kufanya hivyo sio kuwa nimekata tamaa na watu hao lakini kwa faida kubwa kwao na kwangu
kuokoa mda na nishati(to save time and energy).
Watu wanao acha huwa hawasemi. Utaona kwa vitendo
 
Maisha yamenifunza mengi;

Duniani kuna kila kitu lakini si kwa ajili ya kila mtu.

FURAHA ipo lakini si kwaajili ya kila mtu,
MAGARI mazuri yapo lakini si kwa kila mtu,

PESA zipo lakini si kwa kila mtu,

NYUMBA nzuri zipo lakini si kwa kila mtu,
VYEO vipo lakini si kwaajili ya kila kwa kila mtu,

MAISHA mazuri yapo lakini si kwaajili ya kila mtu.

Hii ina maana kwamba ni lazima mtu ujifunze kukubaliana na uahalisia wa maisha yako.
Ni lazima ujifunze kukosa,ni lazima ujifunze kupoteza.

Mimi binafsi kuna mambo nimepambana nayo sana ,imefika wakati siombi Mungu tena anisaidie nifanikishe bali namuomba Mungu anisaidie kuukubali ukweli kuwa hayo mambo sistahili.

Life is not fair kabisa, Mungu atusamehe kwa kweli..daah
 
Huu ndio ukweli ambao wengi wanapaswa waufahamu na waishi nao.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom