Nimeamua kuachana na mtandao wa Tigo kutokana na huduma mbovu, nihamie mtandao gani?

BROKE BOYS

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
13,215
39,040
Habri za usiku wanajukwaa.

Wakubwa nimeamua kuachana na mtandao wa Tigo kutokana na huduma zao mbovu na hawataki kubadilika. Tatizo lao ni internet mbovu imagine unanunua GB30 lakini internet utajua pa kuipatia, nimevumilia sana lakini nimeshindwa.

Tigo kwaheri nimekua mteja wenu toka 2008 ila sasa hivi nawaachia mtandao wenu, mtu anakupigia upo hewani lakini hupatikani kweli haki hii?

Nisaidieni mtandao gani mzuri hasa kwenye internet kati ya Vodacom na halotel? Nataka internet yenye kasi gharama za vifurushi sio tatizo.
 
Huku hakuma nafuu mzee baba. Leo nimeweka pesa halopesa ili nijiunge, ufala niliokutana nao sijaamini. Wamebadilika, vifurushi vyote wamechange ikiwamo vya usiku. Dah nikapigwa na bumbuwazi hadi nimejuta yaani.

Mimi nataka internet yenye spidi nzuri gharama za bundles sio tatizo ntavumilia
 
Halotel nao internet n ya kubahatisha. Better ukomae nao hvohvo
 
Mtandao nchi hii ni Vodacom pekee.

Ukipenda vitu vya bure na dezo ila huduma mbovu basi nenda kwenye hiyo mitandao mingine.

Ila kama unataka huduma ya uhakika na ya kuaminika basi ni Vodacom pekee.
 
Kwa internet Tanzania Voda ndo baba lao hasa maeneo yote ya mjini yenye 4g
 
Nenda duka la tigo lililo karibu nawe waambie wakupatie laini ya 4G+ utapatiwa kwa namba yako iyoiyo muhimu fika na nakala zote muhimu
 
Back
Top Bottom