Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Hali ya hela haikua nzuri siku hiyo, niilpanga kwenda bank kuangalia malipo ya mshahara. Mimi na mwanangu wa miaka miwili tuliamka asubuhi nilimalizia maziwa kidogo yaliyobaki kwenye kopo kwa kuyapikia uji, nilimpa mtoto alipotosheka niliumalizia mimi uji ule.
Enzi hizo hakuna smapart phones na kama ingekuwepo nisingeimudu. Tulifika bank na kuambiwa mshahara haujatoka. Hapo nipo likizo. Plan B ilikuwa kumfahamisha mr huko alikokua hali halisi tuliyonayo.
Mtoto wakati huo alikua na njaa. Tuliingia kwenye mgahawa na kuagiza chai na maandazi mawili. Hapo ni baada ya kutoa pesa ya nauli ya kunifikisha nyumbani. Chai ilifika na kumkatia mtoto andazi. Tunaanza tu kula, kuna kijana aliagiza mtori, supu chapati na soda, wakati ule wenzake walifika kumchukua na gari. Aliagiza chakula chake apewe yule mtoto pale.
Kwakweli mwanangu alikula chai na andazi kwakua alikua na njaa lakini aliufurahia mtori mpaka mwisho.
Yule kijana alikua chuo kikuu na walikua wanakwenda field na wenzake.
Popote ulipo Mungu akubariki kijana. Mwanangu ni mhitimu wa chuo sasa hivi.