Nimeamini viongozi wengi waliishi na Magufuli siyo kwa dhati ya mioyo yao bali kwa unafiki

JPM ameacha legacy kiasi kwamba hakauki midomoni na akilini mwa watu na wewe ukiwa mmoja wao.... Maana mwenyewe humalizi 1hr bila kumkumbuka, ila sijui kama ulishawahi kujiuliza kuwa wewe utaacha nini
Hakika legacy ya jpm zote ya mazuri na mabaya hayatafutika Tanzania na huwezi mkumbuka jpm kwa mazuri tu lazma ukumbuke mabaya maana yalitikisa yani ukimuona magu lazma umwone lissu na ukimuona lissu lazma umuone magu. Lissu is a living example
 
... Jiwe was very successful, for a spell of time, in using our fears to turn all of us into zombies! ... and it's not very wise to blame those waking up from that nightmare!
😅
1623360059450.png
 
Kwa mtu aliyekwisha kufa na kuzikwa, hakika bado amezitawala fikra zenu!

Manake mmeshindwa kabisa kumzika ndani ya hizo fikra zenu duni mlizonazo.

Kila kona Magufuli ndo gumzo!

Sucka bytches.
Huyu alikuwa Rais wa nchi sio kibaka wa Keko..utawala wake unaweza kuna na athari(-) vizazi na vizazi..mfano mmoja ni huu uamuzi wake wa kuruhusu watu kufanya biashara eneo lolote bila kusumbuliwa.

We can't stop talking about him,alikuwa Rais wa nchi hii kwa miaka mitano na miezi kadhaa.
 
JPM ameacha legacy kiasi kwamba hakauki midomoni na akilini mwa watu na wewe ukiwa mmoja wao.... Maana mwenyewe humalizi 1hr bila kumkumbuka, ila sijui kama ulishawahi kujiuliza kuwa wewe utaacha nini😂😂😂
Kutajwa tajwa siyo ishu. Hata mzee Adolf Hitler anatajwatajwa.
Binafsi simsahau Magu. Kuna marais wachache sana duniani wakatili kiwango cha Magu
 
Hawakumpenda vipi wakati walikuwa wanafanya kila alilowatuma, usiwaamini hao, kesho akitokea mwendazake mwingine wataanza kumshangilia kama kawaida yao mradi mikono yao iende kinywani, hata hayo mapambio anayopewa wa sasa ni kwa sababu hiyo hiyo mikono yao iende kinywani, hakuna mapenzi ya kweli hapo.
 
Kubadili gia angani na unafiki kwenye siasa ni jambo la kawaida. Na katika kiini chake, siasa ni mchezo wa kinafiki, mchezo wa kufuata mvumo na mwelekeo wa upepo - hasa katika siasa zetu hizi za kimasikini huku Afrika.

Mtazame, kwa mfano, Mwalimu Nyerere - kiongozi msomi mwanafalsafa na mwenye bashasha sana na aliyeamini kabisa na kutenda alichokiamini. Unaweza kunitajia hata mwanasiasa mmoja tu aliowaacha ambaye unaweza kusema kuwa alikuwa mfuasi wa kweli wa mawazo na fikra zake? Labda Sokoinne japo naye walimuwahi wakamuua mapema tu. Hata mwanafunzi wake aliyemwamini sana mpaka akaingia mtaani kumpigia kampeni nchi nzima (Ben Mkapa) aligeuka na kuwa wa hovyo tu utafikiri hakupita katika mikono ya Nyerere.

Hata mama naye akija kumaliza muda wake gia za angani zitapigwa tu. Ni kawaida!
 
56 Reactions
Reply
Back
Top Bottom