King Innocent
JF-Expert Member
- Dec 13, 2011
- 1,001
- 623
Wakuu natumaini wote niwazima wa afya. Kweli nimeamini rangi nyeusi ikawa nyeupe. Ninampenzi wangu nimedumu nae zaidi ya mwaka mmoja, anajiheshimu na pia anatabia nzuri, tatizo la mpenzi wangu huwa na gubu na kununa bila sababu za msingi na zaidi ugomvi wetu uko ktk mawasiliano , anataka tuwasiliane hata mda wa kazi nikimwambia asubri mda wa lunch basi hununa hata wki moja na nikimpigia hapokei, nijana 2 nilikuwa bafuni akanipigia cm ikaita ikaata nilikamtafuta bdae hataki kupokea sim, nimemtext hataki kunielewa, mara nyingi nimejaribu kummweleza tabia hi siipendi na kuniahidi atabadilika lakini akikaamda hujisahau, nimekata shauri ya kumwacha najua kila binadamu anamapungufu yake lakini kwakweli siwezi kuvumilia, nahitaji ninapokosa niambiwe kosa langu nijirekebishe na si kununiwa bilasababu.