Nimeamini masharti ya marehemu wakiyasema kabla ya kukata roho

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Asikudanganye Mtu popote pale ulipo kuwa kauli za Watu waliokufa namaanisha Marehemu wakizisema huwa hazitimii. Ni kwamba huwa hawatanii kabisa na wayasemayo hutokea na hutimia.

Mwaka jana nilihudhuria Msiba Mmoja ambapo kumbe Marehemu wakati anakata Roho alisema akifa azikwe Dar es Salaam na Ndugu wakampuuza wakamsafirisha wanafika tu Segera wakapata Ajali na wale wale waliolazimisha asafirishwe Wakafa na Msafara ukageuka na kuja Kuzikwa Dar kama ambavyo Marehemu aliagiza.

Mwaka huu Mwezi February kuna Marehemu alisema akifa tu asizikwe Dar es Salaam na akazikwe Kijiini Kwao na Ndugu walipolazimisha Kumzikia Dar es Salaam kwa Kigezo cha Kuokoa Gharama Jeneza lake liligoma Kubebeka ila baada ya muda tu Ndugu walipokubaliana asafirishwe kama alivyoagiza Jeneza lilikuwa jepesi mno Kubebeka na akasafirishwa Kijiini Kwake kwa Maziko.

Leo hii kwa wale Wakazi wa Chang'ombe Temeke nadhani Ajali mbaya iliyotokea Mataa na kusababisha Vifo na Majeruhi mmeisikia.

Ni kwamba Marehemu ambaye ndiyo alikuwa anasafirishwa kwenda Kuzikwa kabla ya kufa kwa Hasira alisema kuna Watu Wawili katika Familia yake akifa hataki waende Kumzika kwani wakati anaumwa na Kalazwa Hospitali walishindwa kwenda Kumuona huku uwezo huo wakiwa nao isipokuwa Dharau na Kupuuza kuliwatawala.

Na katika Ajali hi ya leo ambayo ilikuwa na Msafara wa Gari kadhaa Gari ambayo imegongwa na Kuharibika vibaya ni ya Watu wale wale Walengwa Wawili ambapo wote Wamefariki huku Mmoja Viganja vyake vikikatika.

Hivyo basi baada ya Msiba huu kutokea Msafara wa kumsafirisha Marehemu umeendelea na wale Watu aliowakataa wasimzike nao Wamefariki hivyo Maiti zao zipo Mochwari kwa sasa ukisubiri Msafara ulio Safarini ukirejea ndiyo waanze Kuhangaika nao na Wawazike.

Hata hivyo kuna Mbinu moja nilipewa na Wabobezi wa Kusafirisha Maiti / Marehemu wenye Masharti magumu hasa ya Kusafirishwa kuwa mkianza tu Safari tafuta Jiwe Kubwa / Jiwe Dogo liweke juu ya Jeneza na Marehemu / Mwili hautowasumbueni hadi mnafika. Bado sijaiamini ila kama hapa JamiiForums kuna wenye kuijua zaidi watufafanulie tafadhali.

Jamani tujitahidi mno na sana Kuziheshimu Kauli za mwisho mwisho za Marehemu kwani nimeamini kuwa kwa 85% huwa zinatimia japo kwa 15% zinaweza zisitimie vile vile kama ilivyo kwa Chanjo ya UVIKO-19 ambapo kwa 15% inaweza isikusaidie na ikakuathiri ila kwa 85% huwa inasaidia Kukukinga.
 
Ngoja niwasubiri wajuvyi wa mambo waje kushusha nondo ili nipate Elimu
Hata Mimi pia nawasubiria sana Ndugu na nataka hasa hasa kujua katika hiyo Mbinu ya kuweka Jiwe Kubwa au Dogo juu ya Jeneza la Marehemu mwenye Masharti mengi, Kisirani na Mbishi Mbishi ambaye anasafirishwa kwenda Kuzikwa Mkoani Kijijini ambako alikuwa hataki Kupelekwa / Kwenda.
 
Akikataa kuzikwa eneo A, akang'ang'ania kuzikwa eneo B. Na ninyi ndugu kwa sababu za msingi sana mkaona azikwe eneo A msipate shida sana. Kukwepa hayo mabalaa tumeni ndugu mmoja wa Kiume eneo B akachukue udongo kidogo katika kisado aulete eneo A.

Mkichimba kaburi miminieni udongo mloleta kutoka eneo B, bakisheni kidogo. Jeneza likishawekwa chini kaburini ule muda wa kuweka udongo malizieni na ule mlobakisha.

Muhimu kukumbuka udongo ulioletwa ufike siku moja au zaidi kabla ya maiti kutolewa mortuary. Kwenye udongo ule kuwe na mawe madogo madogo kadhaa. Chukueni jiwe moja miliweke kwenye gari itakayosafirisha maiti kutoka mortuary mpaka makaburini.

Baada ya shughuli yote kukamilika. Gari lililombeba marehemu lisiende nyumbani kabla halijaoshwa. Lioshwe na mtu/watu baki (wasio ndugu) prefferably kwenye Car Wash za mitaa jirani au mtoni. Yule ndugu aliefuata udongo eneo B asiende kwake moja kwa moja baada ya msiba, wengi hupitia Bar kuzuga zuga walau three hours hivi, ikiwezekana kulipia lodge akaoge huko kwanza itapendeza.
 
Akikataa kuzikwa eneo A, akang'ang'ania kuzikwa eneo B. Na ninyi ndugu kwa sababu za msingi sana mkaona azikwe eneo A msipate shida sana. Kukwepa hayo mabalaa tumeni ndugu mmoja wa Kiume eneo B akachukue udongo kidogo katika kisado aulete eneo A...
Lakini shida yote hii ya nini? Yaani ni ubahili tuu wa kumtoa Dar labda mpaka Morogoro, Dodoma au Arusha wakati mwenyewe kaacha maelekezo? Labda itokee hakuna mwenye uwezo kabisa wa kuchangishana na kukodi gari.
 
Uwekaji wa jiwe kubwa au dogo, hautengui maamuzi ya mwendazake. Ni vena kufuata maamuzi yake ili kuepusha maafa kwa wale wanaobatilisha maamuzi yake.
Hata Mimi pia nawasubiria sana Ndugu na nataka hasa hasa kujua katika hiyo Mbinu ya kuweka Jiwe Kubwa au Dogo juu ya Jeneza la Marehemu mwenye Masharti mengi, Kisirani na Mbishi Mbishi ambaye anasafirishwa kwenda Kuzikwa Mkoani Kijijini ambako alikuwa hataki Kupelekwa / Kwenda.
Jiwe huwekwa jirani na sanduku baada ya sanduku kupakiwa ndani ya gari, na huondolewa baada ya sanduku kushushwa toka garini. Kazi ya jiwe hili sio kuzuia ajali, bali ni kuiondoa nuksi au mkosi unaofuatana na mwili wa mfu.

Baada ya sanduku kushuswa ndipo jiwe huondolewa toka garini na kudondoshwa chini . Kwa kufanya hivyo, nuksi iliyofuatana na sanduku huondoka ndani gari pamoja na jiwe. Hivyo, gari litakuwa salama.

Hujawahi ona gari lililotoka kusafirisha maiti linapata ajali wakati linarudi toka safari?.
" Kalaga bahho."
 
Asikudanganye Mtu popote pale ulipo kuwa Kauli za Watu waliokufa namaanisha Marehemu wakizisema huwa hazitimii. Ni kwamba huwa hawatanii kabisa na wayasemayo hutokea na hutimia...
Kifupi kauli zao hutimia.

Nakumbuka nikiwa mdogo mama yangu mkubwa alikuwa na pesa na Mali zisizo hamishika lakini kwakuwa alikuwa na UGONJWA wa ajabu wa kujivua Gamba (Kama mdudu) baadhi ya ndugu walimnyanyapaa. Sasa hivyo hivyo alisema endapo at ONDOKA duniani wasimsafirishe na watu fulani wasipewe chochote kutoka ktk Mali yake.

Kilicho tokea Alipofariki walilazimisha kusafirisha walipo Anza safari TU sanduku likatoka kwenye gari, mwili ukatoka kwenye sanduku ukaangukia mbalii! Naam toka SAA 3 asubuhi Hadi saa11:30 jioni hawawezi unyanyua hata kuusogeza Hadi pale walipo badili uamuzi wasimsafirishe ndo ukabebeka.

2. Wale waliokuwa wakimnyanyapaa kila aliye pewa Mali toka katika Mali zake alisepa hakuitumia hiyo Mali aliyopewa!
 
Back
Top Bottom