Nimeamini mapenzi yana nguvu sana

Mkuu huyo ni mwanafunzi kaa naye mbali, umri wako ni mdogo Sana kwahiyo hizo zote Ni tamaa tu, sababu umbo lake la balehe linaanza kujengeka, usisingizie mapenzi wala Nini, na ujinga,jinga mwingine,

pili ukianza hayo unayofikiria kuyaanza,(hata Kama hutompitia)itapelekea asifocus kwenye masomo sababu yako hivyo itapelekea yeye kufail masomoni,
Au utampa tumbo Kisha atimuliwe shule sababu yako pia, alafu lazima akubali sababu kwao hakuna kitu (pia usijidanganye hutompitia) baada ya hayo lazima arudi kwako,

Kati ya hayo likitokea Moja wapo, tayari
Utakua ushamuharibia maisha yake, na ndoto zake pia, ambapo angefanikiwa, labda angewasaidia wazazi wake (roho inaniuma)
Hivyo atakua tegemezi, na hutomtaka tena Kwani atakua Kama mzigo kwako, na kuanza kumnyanyasa sababu unajua kwao Hana kitu,

Tukirudi kwako, Kama ukijulikana una mahusiano na mwanafunzi, hapo lazima uingie jela, ukatumikie miaka 30 Kwani nyie ndio mna haribu watoto, Kama tungekua hatutumii fake I'd ungekua jela tayari(asikwambie mtu jela Ni mbaya Sana)

Alafu angekuwa mwanao wewe ambaye Ni mwanafunzi, alafu ana lidume pembeni, ungejisikiaje? Ungefanyaje?(Mimi ningekupiga Sana Kisha ukamalizie miaka yako jela) sitokubali huu ujinga wa kuniharibia mwanangu tena wa kike,
Kwanini usitafute wanawake wengine waliojaa,(wanawake wako wengi) ambao wanatafuta wanaume, hebu tutumie ubongo wetu vizuri jamani,


Tafadhali mwache, mwache mtoto wa watu usimwambie chochote, mwache amalize masomo yake, elimu ndiyo kila kitu kwa Sasa dunia ilipo, bahati nzuri sio mtu was matusi,
Nimeandika kwa uchungu mno sababu
Inasikitisha sana, tumepewa ubongo kufikiria Cha ajabu tunatumia kichwa(fuvu)

Kama Kuna watu mna tabia hii tafadhali acheni.
Ndungu unatumia hasira sana ,kwenye maelezo yangu hakuna sehemu niliyo sema asitishe masomo yake na ndio maana nikasema sijui ufauru wake kama ni mzuri au ni mbaya ikiwa ni mbaya basi nitamsubili, lakini kama ufahuru wake ni wa kiwango cha juu basi nitarazimika kumuacha asome kwa sababu sintaweza kumsubilia kwa muda mrefu sana, hicho ndicho nilicho maanisha ndugu usinielewe vibaya.
 
Nilikutana na binti street kisu hatari. Mwisho naambiwa yupo form two. Anyway, yashapita.

Kwako mleta uzi, nunua shamba la miti ya mbao lenye life span ya miaka 20 - 27. Ili ukifungwa siku unatoka hilo shamba la miti liwe mtaji wako.

Huyo binti humpendi na hata hujamtamani huyo binti ni unamuonea huruma kwa situation yake. So unatamani umsaidie na namna pekee kijana wa miaka 24 anaona anaweza msaidia mtu ni kupitia mapenzi.

Hiyo ishu ipo kisaikolojia zaidi. Wengi wetu hushindwa kutofautisha kati ya huruma na upendo. Wewe sasa ndiyo umenasa hapo.

Now kama unataka kujinasua nicheki PM na malipo yangu kwa session ya nusu saa ni mti mmoja wa mbao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom