Nimeamini mapenzi ya dawa yana mwisho

kakamgeni

JF-Expert Member
Feb 1, 2018
241
201
Mambo Zenu Wadau Wa Jukwaa Pendwa La MMU, Bila Shaka Mtakuwa Mnaendelea Vizuri Na Wazima Wa Afya, Pili Ningependa Kutoa Pole Kwa Wakazi Wenzangu Wa DAR Kwa Jua Kali Linaloendelea Kuwaka.

Nikirudi Moja Kwa Moja Katika Kiini Cha Hii Thread, Ni Kwamba Wapo Baadhi Ya Watu Miongoni Mwetu, Wakike Kwa Waume Ambao Wamekuwa Na Desturi Za Kitumia Ndumba Ikiwa Kama Njia Mojawapo Ya Kuwanasa Wenzi Wao Wakiwa Na Malengo Mbalimbali.

Basi Ningependa Nieleze Japo Kwa Ufupi Mtihani Uliowahi Kunikuta Miaka Kama 2 Hivi Nyuma, Ambao Ulinipelekea Kuja Kuomba Ushauri Katika Jukwaa Hili Hadi Kufikia Hatua Ya Wadau Wengi Kushangaa Ni Kwa Jinsi Gani Nilivyokuwa Nashindwa Kufanya Maamuzi Magumu.

Wahenga Hawakukosea Pale Waliposema "USICHEKE MAMBA KABLA HUJAVUKA MTO" Wakiwa Na Maana Huenda Ukamuona Mtu Wako Wa Karibu Au Jirani Yako Anapitia Katika Mtihani Ambao Wewe Kiuhalisia Na Kwa Kutumia Macho Yako Ya Nyama Ukaona Ni Wa Kawaida, Kumbe Katika Ulimwengu Wa Roho Huyo Mtu Akawa Katika Kifungo Kizito Kisichoelezeka.

Niliwahi Kuwa Kwenye Mahusiano Yaliyodumu Kwa Takribani Mwaka Na Mwanadada Mmoja Mkoani Mwanza, Lakini Kwa Mazito Niliyopitia Hadi Kufikia Hapa Nilipo, Hakika Ni Jambo La Kumshukuru Mwenyezi Mungu.

Hayakuwa Mapenzi Ya Kawaida Bali Ni Shirki Ya Hali Ya Juu Kiasi Hata Cha Kupelekea Kusahau Na Kutokuwa Na Muda Na Wazazi Walionizaa. Nakiri Kwamba Nilikuwa Katika Kiza Kinene Kisichoweza Kuelezeka.

Baada Ya Kuachana IIlinigharimu Kwa Kuanza Kuporomoka Kiuchumi Kwa Kiwango Cha Lami, Hela Nilikuwa Natafuta Kwa Tochi, Ilibakia Asilimia Chache Za Kudata, Marafiki Walinikimbia Nikabaki Mkiwa.

Ila Baada Ya Kuhangaika Sana Hatimaye Ilinichukua Mwaka Mmoja Na Nusu Kuweza Kuondokana Na Mawazo Na Ndoto Za Usiku Alizokuwa Akinijia. Navyozungumza Sasa Hayupo Kabisa Katika Mawazo Wala Kihisia Hadi Inafikia Hatua Ya Kujishangaa Mwenyewe Binafsi Kama Vile Nimeshikwa Na Butwaa

Ni Hayo Machache Niliyosema Nishee Na Nyie Kwa Usiku Wa Leo, Pia Nitoe Rai Kwa Wale Wanaokesha Kwa Waganga Wakiamini Mapenzi Ya Ndumba Huenda Yakaja Yakadumu Daima, Waache Mara Moja

Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole kwa yaliyokukuta je ulijuaje km ulifanyiwa shirki? Na ulitumia njia gani kujinasua?
 
Back
Top Bottom