Nimeamini Laana zipo, heshimuni wazazi na wanaukoo mlikotoka

Wewe huna tofauti Na mtu asieamini kuwa kuna COVID-19 sema hayajakukuta
COVID-19 ni suala la kisayansi, laana ni mambo ya kufikirika tu kama hekaya za Abunuwasi. Wengi wanaoamini hayo mambo ya laana ndio utawakuta pia hawaamini COVID ipo au wanasema chanjo zinabadilisha DNA kama wakina gwajiboi na wafuasi wake.
 
Kutoviamini ndiyo upuuzi wa upuuzi. Jaribu kuwafanyia wazazi wako hiyo kitu uone utakavyokong'otwa. Kusema ni rahisi kwa vile hulipii kodi. Kwa wajinga sana, hii kitu haipo. Kwa wenye akili hii kitu ni realistic.
Anacho kiamini MTU ndipo kinacho mtokea,kama umelelewa akiamini laana ni kweli basi itakuwa hivyo kama unavyo amino na vice versa.
 
Kuna familia ya mjomba wangu imeishia pabaya sana. Najitahidi kuamini vinginevyo lakini akili yangu inaniambia ni laana.

Mjomba wangu alikuwa ni msomi wa Ph.D na alikuwa na pesa kama uchafu. Majumba, magari na miradi mingine kibao. Alikuwa na mke na watoto watano wa kike wawili na wa kiume watatu. Watoto wote walikuwa wamesoma shule za maana, namaanisha za maana sio english medium ila shule za maana za kimataifa ambazo hata mtoto wa obama angesoma bila shida. Vyuo baadhi yao wamesoma nchi za wenzetu.

Mjomba alikuwa ni mtu mwenye upendo na alisaidia sana ndugu zake. Kiukweli alikuwa ni mtu ambaye ametoboa sana kimaisha ukilinganisha na ndugu zake wengine wa ukoo mzima. Baadae aliugua afya yake ikazorota sana na akili zikawa kama zimeruka kidogo (sio sana). Mkewe na watoto wake hawakumjali. Kila alilowaambia hawakumsikiliza akawa hana thamani tena. Huwezi amini houseboy alimtunza na kumjali kuliko mkewe na kizazi chake. Kuna siku watoto wake waliuza mashine fulani kwa mhindi ambayo aliipenda sana. Siku mhindi amekuja kuinunua alikuwa juu ghorofani nyumbani kwake akiangalia, aliwakataza wasiiuze mpaka machozi yakamtoka, lakini hakuna hata aliyehangaika kujishughulisha kumsikiliza, huku mkewe akiwa ndio mhamasishaji mkuu.

Baada ya miaka kama mitatu alifariki dunia, inasemekana alifariki na kinyongo sana. Lakini kabla ya kifo aliacha wosia akazikwe kijijini kwao, lakini familia yake haikutekeleza hilo takwa lake. Kipindi cha msiba ulitokea mgogoro mkubwa Kati ya familia yake na ndugu washamba wa kijijini. Ndugu walitaka akazikwe kijijini na walikuwa tayari kuchangia gharama, lakini familia iligoma katakata. Wakatokea wanasheria marafiki wa enzi za uhai wake huko mjini daslamu, wakatetea wakisema kisheria mke ana haki ya kuamua wapi mmewe akazikwe. Ndugu ikabidi wawe wapole na walivyo waporipori kusikia mambo ya sheria wakanywea.

Lakini walikuwa na kinyongo sana, maana walikusanyika kwa ajili ya kuzika na mwili haukuletwa. Hivyo wakaamua kwenda kutembelea sehemu ambayo kama angeletwa kijijini basi marehemu angezikwa. Sehemu hiyo kulikuwa na makaburi ya ukoo, unaambiwa wanandugu wakasafisha makaburi na kuomba dua ya kuwaombea laana wale watoto na familia ile.

Mpaka ninapoandika huu uzi, nipo bado safarini tunaenda kumalizia kumzika mtoto wa huyo mjomba aliyekuwa amebakia. Mjomba alifariki 2010 yaani ndani ya miaka takribani kumi tu familia nzima imepukutika, amebaki mama naye afya yake inasikitisha.

Kinachosikitisha watoto watatu walibahatika kufunga ndoa, lakini wote hawakuwahi kupata watoto hata wa kusingiziwa. Familia yote wameingia kaburini bila watoto, mama yao kabaki peke yake bila hata mjukuu. Mimi si Mungu ila naomba Mungu anisamehe kama nitatumia lugha isiyo na hekima wala nidhamu. Ila ukweli huyu mama ni wa leo wa kesho. Inasikitisha sana laana zipo jamani. NB familia bado haijafirisika, pesa bado ipo kama yote, ila waliopaswa kuifaidi wametangulia wote wakiwa bado vijana wadogo.

Hitimisho, tujitahidi kuishi vyema maisha yetu hapa duniani, maana tunaweza kukutana na kifo siku yoyote na siku hiyo inaweza kuwa leo.
Duuhhh ...Mama bado ameshupaza shingo?.

Pengine ni ndugu wa mwanaume. Wameamua kuwapukutisha ili wabaki na Mali??

Laana huwa inaleta majuto, ili ujutieee. Uone wapi umekosea. uombe radhi.

Hapo naona, ndugu wa mwanaume. Kuna maagano ya kimizimu waliyafanya juu ya familia hiiyo ya mjomba wako.

NA NDIO MAANA UZAO WAO ( WATOTO,) NDIO WAMEKUFA WOTE KABLA YA MAMA YAO..( MAMA SIO UZAO WAO).

Kwamba ilikua laana kwaajili ya kumtesa Mke ??? Huyo mke hana akili wala kujiuliza, kwann kafa wakwanza, wapili. Kwann hawapati mtoto??

NITAKUA WA MWISHO KUAMINI KUNA LAANA YA AINA HIYO. NYUMA YA MATAMBIKO WALOYAFANYA HUKO. KUNA MAAGANO MLIYAFANYA KUITESA FAMILIA HIYO.
 
Kuna familia ya mjomba wangu imeishia pabaya sana. Najitahidi kuamini vinginevyo lakini akili yangu inaniambia ni laana.

Mjomba wangu alikuwa ni msomi wa Ph.D na alikuwa na pesa kama uchafu. Majumba, magari na miradi mingine kibao. Alikuwa na mke na watoto watano wa kike wawili na wa kiume watatu. Watoto wote walikuwa wamesoma shule za maana, namaanisha za maana sio english medium ila shule za maana za kimataifa ambazo hata mtoto wa obama angesoma bila shida. Vyuo baadhi yao wamesoma nchi za wenzetu.

Mjomba alikuwa ni mtu mwenye upendo na alisaidia sana ndugu zake. Kiukweli alikuwa ni mtu ambaye ametoboa sana kimaisha ukilinganisha na ndugu zake wengine wa ukoo mzima. Baadae aliugua afya yake ikazorota sana na akili zikawa kama zimeruka kidogo (sio sana). Mkewe na watoto wake hawakumjali. Kila alilowaambia hawakumsikiliza akawa hana thamani tena. Huwezi amini houseboy alimtunza na kumjali kuliko mkewe na kizazi chake. Kuna siku watoto wake waliuza mashine fulani kwa mhindi ambayo aliipenda sana. Siku mhindi amekuja kuinunua alikuwa juu ghorofani nyumbani kwake akiangalia, aliwakataza wasiiuze mpaka machozi yakamtoka, lakini hakuna hata aliyehangaika kujishughulisha kumsikiliza, huku mkewe akiwa ndio mhamasishaji mkuu.

Baada ya miaka kama mitatu alifariki dunia, inasemekana alifariki na kinyongo sana. Lakini kabla ya kifo aliacha wosia akazikwe kijijini kwao, lakini familia yake haikutekeleza hilo takwa lake. Kipindi cha msiba ulitokea mgogoro mkubwa Kati ya familia yake na ndugu washamba wa kijijini. Ndugu walitaka akazikwe kijijini na walikuwa tayari kuchangia gharama, lakini familia iligoma katakata. Wakatokea wanasheria marafiki wa enzi za uhai wake huko mjini daslamu, wakatetea wakisema kisheria mke ana haki ya kuamua wapi mmewe akazikwe. Ndugu ikabidi wawe wapole na walivyo waporipori kusikia mambo ya sheria wakanywea.

Lakini walikuwa na kinyongo sana, maana walikusanyika kwa ajili ya kuzika na mwili haukuletwa. Hivyo wakaamua kwenda kutembelea sehemu ambayo kama angeletwa kijijini basi marehemu angezikwa. Sehemu hiyo kulikuwa na makaburi ya ukoo, unaambiwa wanandugu wakasafisha makaburi na kuomba dua ya kuwaombea laana wale watoto na familia ile.

Mpaka ninapoandika huu uzi, nipo bado safarini tunaenda kumalizia kumzika mtoto wa huyo mjomba aliyekuwa amebakia. Mjomba alifariki 2010 yaani ndani ya miaka takribani kumi tu familia nzima imepukutika, amebaki mama naye afya yake inasikitisha.

Kinachosikitisha watoto watatu walibahatika kufunga ndoa, lakini wote hawakuwahi kupata watoto hata wa kusingiziwa. Familia yote wameingia kaburini bila watoto, mama yao kabaki peke yake bila hata mjukuu. Mimi si Mungu ila naomba Mungu anisamehe kama nitatumia lugha isiyo na hekima wala nidhamu. Ila ukweli huyu mama ni wa leo wa kesho. Inasikitisha sana laana zipo jamani. NB familia bado haijafirisika, pesa bado ipo kama yote, ila waliopaswa kuifaidi wametangulia wote wakiwa bado vijana wadogo.

Hitimisho, tujitahidi kuishi vyema maisha yetu hapa duniani, maana tunaweza kukutana na kifo siku yoyote na siku hiyo inaweza kuwa leo.
Mungu akubariki sana mpendwa kwa ushuhuda mzuri, na itoshe kusema kuwa umetuokoa wengi sana kujua hii inshu.
 
Hao wamerogwa tu!!! hakuna laana Duniani Idiot!! ...Mungu pekee ndo alitoa laana zamani kabla ya Yesu kufa msalabani!...hizo laana ni wewe mwenyewe au watu wanawaroga ajilinya ustawi wenu!! kwa kusingizia eti laana!!

mwanao ulo mkojoa kumlaani ni ngumu sana!! ili iweje kwanza!!....saana utaona km amerogwa na wasio kutakia mema ...ukiona unakuwa na guts za kumlaani mwanao basi wewe ndo ulilaaniwa kwanza!!.... mtoto anauma sana!!

km unamlaani kwa nini ulimzaa?...wewe mwenyewe ni kituko! yeye ntoto hakuomba kuja Duniani! nyegenyege zako ndo zilimsababbishia kwa hiyo umlinde asikutukane watu nyie wabaya sana hasa ndugu!! ni mashetani!
 
Anacho kiamini MTU ndipo kinacho mtokea,kama umelelewa akiamini laana ni kweli basi itakuwa hivyo kama unavyo amino na vice versa.
wewe umenielewa ni km wanavyo amini Yesu mzungu anasamehe dhambi na kweli wanasamehewa!! eti yesu mzungu anaponya, anarudisha misukule mweee gwaji boy hapo kateleza mbaya!!...huwaga nacheeeka kuwa inaezekana gwajima anapiga ndefu maksudi..

halafu ameweka kibendera cha israel mbele ya mimbari......sijui alisomea wapi huyu jamaa...
 
Back
Top Bottom