Nimeamini kweli tanzania ni kichwa cha mwendawazimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeamini kweli tanzania ni kichwa cha mwendawazimu

Discussion in 'International Forum' started by Mahatma Gandhi, Jan 17, 2012.

 1. Mahatma Gandhi

  Mahatma Gandhi Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mambo vipi Wanajamii Forum???Naomba musome hapa kwa makini kisha tujadili katika hili.Juzi nilikuwa nasoma ripoti ya UNDP ya mwaka 2011 kuhusu hali ya maendeleo katika nchi 187 wanachama wa UN.Ripoti hiyo imezigawa nchi hizo katika makundi makuu manne;yaani nchi zenye maendeleo ya juu sana,ya kati,chini na maskini sana.Nchi za Norway,Australia,Uholanzi,Marekani,New Zealand,Canada,Ireland,Liechtenstein,Ujeruman na Uswisi ziko katika kumi bora kimaendeleo.Barani Afrika nako Ushelisheli ni ya 52 na ni ya kwanza katika Afrika ikifuatiwa na Libya(ya 64 ingawa kulitokea mapinduzi mwaka jana) na ya tatu ni Mauritius(ya 77).Tanzania yenye madini kibao (hususani Tanzanite),mito,maziwa,bahari na misitu inashika nafasi ya 152 na ni kati ya nchi zilizo katika kundi maskini sana pamoja na DRC yenye Diamond,misitu(kwa ajili ya mbao),mto Congo,ziwa kivu n.k inashika nafasi ya mwisho (187).Ebu waungwana sisi kama wadau wakubwa wa maendeleo ya nchi yetu na bara la Afrika kwa ujumla tufanye tafakuri.Hivi hizi rasilimali (nilizotaja hapo juu) zipo kwa ajiri ya kutufanya tuwe maskini wa kutupwa kila kukicha?,au Mungu alitupa kama laana bila sisi kujua(lakini nisingependa kumkufuru Mungu wangu)?,na je hatuwezi kuzitumia kujiletea utajiri kama Norway na Australia?? Hivi katika hili,tatizo ni nini????
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  mmmh huwa tuajifariji kuwa bora tuna amani, sasa sijui kuwa na amani kama kunachukuliwa kama kigezo kimojawapo katika kuweka groups
   
 3. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tanzania haiwezi kuendelea. Kama wakiiweka kwenye kundi la nchi zinazoendelea watapanga vipi njama za kuinyonya? Amka Mahatma Ghandi. Hii ni ZYTGIEST. Unataja madini kama Tanzanite, mbona nchi inayo ongoza kwa export ya Tanzanite ni Kenya? Wizi wa aina hii utaendelea hapa Tanzania hadi tuamke kwenye usingizi wa ujinga. Kama unataka maendeleo yatakayo badilisha taswira ya Tanzania ngoja 2015 uchague viongozi kwa kupanga na sio kwa sura au chama. Kinyume na hapo badili uraia na uhame kwenye nchi yenye maendeleo
  KAPANGA NI KUCHAGUWA KWA MANUFAA YA TANZANIA:shock:
   
 4. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hakuna jipya, jambo hili limeshajadiliwa sana humu na sehemu nyingine...Tatizo letu waTanzania (sijui kama na wewe ni mTanzania) siku hizi tumekuwa na hulka ya kulalamika badala ya kutoa suluhisho. Pia tumebaki kusifia wenzetu wanapofanya vizuri bila ya kujisifia sisi pale tunapofanya vizuri.

  HDI yetu ingawaje bado ni mbaya lakini imekuwa ikikua kwa kasi miaka ya hivi karibuni ukilinganisha na nchi zingine. Kwa mfano hiyo ripoti yako inaonyesha tuko juu ya Nigeria pamoja na mafuta yao, pia nchi kama Pakistani ndio tuko nazo kwenye kundi hilohilo etc, etc, etc...Kama wewe ni mfuatiliaji miaka michache iliyopita tulikuwa tunashika nafasi ya tatu (3) toka chini na sasa tuko nafasi ya thelathini na saba (37) toka chini.

  Chamsingi ni kuendelea na mabadiliko na kurekebisha sehemu tulizokosea kama kwenye mikataba ya madini, mambo ya ufisadi etc, etc,. Hopefuly tukiwa na KATIBA nzuri na tukapata RAIS bora kipindi kijacho tutatoka kabisa kwenye kundi hilo....
   
 5. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  wewe! Suluhisho hata ukitoa linakuwa la mdomoni tu, nani atakusikiliza? Kila mtu anjaiangalia nafsini mwake. Kila mtu anajali maendeleo yake binafsi. Kamwe nchi hii haitaendelea kwa mawazo ya ubinafsi.
   
 6. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mkuu Mahatma Gandhi mambo yanayokwamisha maendeleo TZ ni mengi lakini kubwa zaidi ni utawala mbovu!!!!!!! Mikataba yoote iliyofanywa TZ ni ya kifisadi, kuanzia madini yetu, vtega uchumi kama umeme(IPTL,DOWANS,SYMBION POWER), reli, vivuko bandari!!!!! Njoo sasa kwenye fedha zetu watu wanaiba live toka BOT, EPA mfano wakikamatwa eti warudishe wasamehewe kama vile ni mchezo wa kuigiza!!!! Aridhi wanapewa mabwenyenye kwa majina ya wawekezaji wananchi wanafukuzwa na kuuwawa badala ya kusaidiwa wainuke kiuchumi!!!!!! Unategemea nguvu ya uchumi wa Mtanzania itatoka wapi, wakati mali za asili zoote wamepewa wageni na wanalindwa na serikali bila kujali umaskini wa Mtanzania wanachukua kila kitu hadi udongo, Mtanzania atainukia wapi?????????? Lazima ipatikane serikali inayochukia wizi rushwa ufisadi dhuruma kwa wananchi wake, ili Mtanzania aweze kufaidi hizo rasilimali zake!!!!!!!!!!

   
 7. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  KATIBA mpya, Rais na serikali bora....hakuna zaidi ya hapo, labda ubadili uraia....:A S-coffee:
   
Loading...