Gily Gru
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 7,802
- 20,761
Kwa kweli Mungu ni mwema sana na Namshukuru kwa siku hii ya leo. Imekuwa na changamoto nyingi sana hii siku ya leo ila najua nimezishinda na usiku umeingia hapa ni kwenda kulala tu hakuna purukushani za ziada.
Kwanza kabisa wife kasafiri kaenda kwa wazazi wake, leo nimejikuta niko kwenye mitihani kidogo. Mke wangu amejaliwa kweli kwenye mapishi, huwa akiwepo nyumbani amepika; lazima niwahi nyumani nikapate maakuli. Napenda sana kula mimi na nafurahi sana kumpata mtu mwenye kujua kupika mapishi mengi sana.
Asubuhi imeanza nimeamka na njaa kali sana, imenibidi nikatafute sehemu nipate kifungua kinywa. Kwa kweli kila napoenda ukiangalia mazingira ya upishi na hata sehemu zenyewe kuna mainzi nimeshindwa kula ikabidi ninunue mkate nipike chai ninywe
Ile nimebandika chai nimeweka majani na sukari nikasubri ikachemka ili ninywe. Nilivyokunywa tu chai ilikuwa chungu sana kama mwarobaini. Ikanibidi nipige simu nimulize wife vipi mbona chai chungu majani leo mbona yamekuwa machungu. Akanijibu nitakuwa nimezidisha majani na yeye huwa anaweka vitu vingi zikiwemo mdalasini, iriki na vingine kanitajia sivijui. Kwa njaa ile nilimeza na ile mikate kama nyoka anavyomeza kuku.
Nilipomaliza nikaenda washa moto jiko la mkaa (Jiko Koa). Ule mkaa ulikuwa umelowa na maji. Niliuwasha sana kama saa nzima hivi ndo mkaa ukawaka. Niliwasha na karatasi wapi nikajikuta nimechana daftari la mtoto la shule lote kesho nina kazi ya kwenda kununua jingine. Nikaenda store kwenye makorokoro nitafute tu hata kimfuko cha plastiki, nilipokipata ndio kikawashia moto
Kazi ikaja bhana kuzisukuma, nilisukuma sukuma sukuma kila nikisukuma duara haliji naona linakuja ovyo ovyo. Huwezi amini nilisukuma ile chapati moja nusu saa. Nikasukuma sana mwisho nikaona nipike hivyo hivyo. Ile kuiweka jikoni tu na mafuta wacha niungue lile frampeni lilikuwa la moto sana. Mkono wangu nimeungua karibia vidole vyote, cha kusikitisha ile chapati ya kwanza ikatoka kama ina macho vile inanishangaa. Nimeshindwa kuila hii chapati hebu angalieni inavyonitizama kwa dharau kama hivi:
Nikapika chapati ya pili nayo imeungua imekuwa kaukau. Kwa kweli nimemkumbuka sana mke wangu na vyakula anavyonipikia. Nimejua hata kama mwanamke ni mama wa nyumbani hapaswi kudharauliwa kazi ya moto si kazi nyepesi ina shughuli pevu. Ukila chakula cha mkeo ujue ni damu yake, jasho lake, nguvu zake, upendo wake, maumivu yake ya kuungua nk. Kubeza chakula kilichopikwa na mwenzio ni dhambi kubwa Mungu atusamehe tu.
Ila nashukuru chapati moja tu kati ya kumi na tano ndio iliyotoka vizuri nyingine nimeunguza sana. Sijui kama kesho zitafaa kula kiporo, ila kwa kweli kuna haja ya kujua kupika hata kama una mke. Nimekulia katika familia za mfumo dume mwanaume hakai jikoni, siwezi kujilaumu mwenyewe kwa kutojua kupika. Kwa kweli leo nimejua umuhimu wa mke wangu katika maisha yangu, Nakupenda sana Mke wangu, Mungu akujalie maisha marefu, ukiniacha mwenyewe nitakonda. .
At least this one came out better compared to others: (Sadly, It is the only one)
Kwa jinsi nilivyoungua Yesu tu ndio anajua, Nawasisitizia tu tuwaheshimu sana wake zetu. Hata kutofanikiwa ni kwa sababu tu ya kutoheshimu nafasi za wenza wetu katika maisha yetu. .