Nimeamini kwamba gari ndio uchawi mkubwa unaowatesa wanawake.


WA KISHUA

WA KISHUA

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Messages
367
Likes
14
Points
35
WA KISHUA

WA KISHUA

JF-Expert Member
Joined Dec 11, 2012
367 14 35
Habari za majukumu ya kujenga Taifa letu la Tanzania wanajamvi, japo tumepita katika vuguvugu la masuala ya udini na ukabili lakini tunaamini kwa neema yake yeye aliye juu mbinguni hakika hakuna kinachoshindikana dhidi yake, bnafsi ni mzima wa afya na ninaendelea vyema na mambo yanaenda kama yalivyopangwa.

Leo nimekuja na kichwa cha habari hapo juu kinachosema ''NIMEAMINI KWAMBA GARI NDIO UCHAWI MKUBWA UNAOWATESA WANAWAKE''. , kwanza kabisa ningependa nieleweke na jamii nzima ya JamiiForums hasa katika hiki kipengele cha MMU kwamba siwaongelei na sipo hapa kuwalenga, kuwaponda wanawake au kuchambua makosa yao kama wengine walivyokuwa wakisema hapo nyuma kwani hata mimi nimetokea kwa watu kama hao, ila dhumuni langu kubwa nikutaka kuelimishana nikiwa kama mwanajamii na kuwapa tahadhari wale ambao wanataka kuingia kwenye mkenge kama huu ikiwa kama tahadhari kwao kwani walengwa wakubwa ni sisi vijana ambao ndio Taifa la leo ukizingatia kwamba magonjwa ni mengi na life is too short.

Nichukue fursa hii nianze kueleza kilichonipelekea mpaka nikaandika uzi huu hapa ili kuweza kushare mawili matatu na watu wazima wenzangu kwa maana naamini kwamba katika kila kinachonitokea huwa ni funzo na darasa tosha.


Weekend iliyoisha niliona sio mbaya niende kubadilisha mazingira nje kidogo ya mji wa Dar es salaam katika sehemu moja mpya imefunguliwa inayoitwa LEDGER PLAZA, kwa wale ambao ni watembezi kama mimi nadhani watakuwa wameshapafahamu ni wapi, sehemu hii ni nzuri sana ipo maeneo ya Kunduchi eneo la Bahari beach ambapo hii Plaza zamani ilikuwa inafahamika kwa jina la Bahahri Beach Hotel, kusema ukweli ni sehemu mpya imefunguliwa na watu wanotembelea pale ni wengi wenye hadhi zao tofauti tofauti, basi kama kawaida yangu mimi nikasogea maeneo yale kuweza kuangalia kipi kipya na wameongeza nini pale, kwa bahati mbaya au nzuri nilikutana na vijana au lugha nyepesi wadogo zangu ambao niliwaacha chuo nao walikuwa pale na wapendanao wao ikawa kama bahati ya kupata company, kama mnavyofahamu wa2 ambao hamjaonana kitambo tulikumbushana story za chuo na mambo mengine mengi pia nilipata kuwajua wake zao watarajiwa na kuweza kumake nao story mbili tatu huku bill za Dompo Wines na White Meet zikiwa zinakuja na kikao kikiwa kinaendelea vizuri, baada ya kupiga story sana bill ikaja nikaona sio mbaya kaka yao nisimamie show japo nilikuwa nimedandia Treni kwa mbele nikaona sio jambo baya kulipa baada ya hapo jamaa wakaniaga kwamba wanaondoka kwaiyo tutawasiliana because tulikuwa tumeshapeana contacts tayari, nikawambia hata mimi sina muda mrefu sana pale kwani giza lilikuwa tayari limeshaingia, jamaa wakaondoka lakini sikuweza kufahamu kama walikuja na usafiri au lah kwani parking ilikuwa imejaa magari mengi sana ivyo haikuwa rahisi kuweza kumgundua kila mmoja kama amekuja na private car au kwa Tz 11 kama wabongo wanavyosema namaanisha Miguu, baada ya dakika kama kumi na tano kupita mimi nikasogea nakuingia kwenye KaVerossa kangu huyo safari ya kuelekea nyumbani ikaanza, lakini cha kushangaza na kustaajabisha nikawakuta wale vijana wangu eneo la bus stand pale kunduchi wakisubiria daladala nikaona sio vyema kuwapita ikabidi nisimame na kuwaita, wakaja pamoja na kuingia kwenye gari yangu safari ikaendelea, kwa ufupi hawa vijana wangu mmoja wao anakaa Ubungo na mwingine Mbezi Beach sema hawa wake zao mmoja anaishi Mikocheni Regent Estate na mwingine naweza kusema ni jirani yangu kwani anakaa Msasani, Basi baada ya kuwaacha hawa jamaa mmoja pale Mbezi na Mwengine Mwenge safari ikaendelea na wale bi wadada, lakini nikagundua kuna aina Fulani ya kauli ambazo walikuwa wanatoa hawa mashemeji zangu watarajiwa kwa kuwaponda wadogo zangu, walikuwa wakilalamika usafiri shida isitoshe sehemu yenyewe mbali wamekuja bila kujua ila kama wangejua wasingekuja, mara mwingine akawa anasema pozi zote ziliisha wakati walipokuwa wanasubiria daladala pale stand, kutokana na busara zangu za kiutu uzima nikawa najaribu kubalance mzani kwa kuwatetea vijana wangu kwamba maisha bado ni taratibu na isitoshe wote wanatafuta kwaiyo uvumilivu ni jambo la msingi, wenyewe bado wakendelea kukazania bango kwamba hata kama ila hawajui kumtreat mwanamke, nilipoona hali imefika ivyo nikaone nitumie busara zangu tena kwa kukaa kimya, kila mmoja nikampeleka kwao lakini huyu wa msasani baada ya kumfikisha maeneo jirani na kwao akaomba namba yangu ya simu, nikaona kwa kuwa ni shemeji ngoja nimpatie kiroho safi, basi baada ya kumpatia nikanyoosha goti na kurudi nyumbani kwangu.


Siku ya jumapili nilipokea simu kwa wale vijana wangu kwa kunishukuru sana kwa aibu niliyowatoa kwani wanadai kwamba watoto walikuwa wanagoma kupanda daladala na walikuwa wanadai Taxi au Bajaj, mimi nikawambia hayo ni mambo madogo na kwenye maisha msingi mkuu ni kusaidiana, kukaa muda sio mrefu ikaingia text ya yule shemeji ambaye aliomba namba zangu za simu, kusema ukweli niliongea nae mazungumzo ya kawaida sana na yeye pia alinishukuru na kusema kwamba najua kucare, kitu kilichonishangaza yule shemeji mwingine wa Mikocheni akamwambia jamaa yangu kwamba anaomba namba yangu, jamaa ikabidi anitaarifu kwamba amempa mke wake mtarajiwa namba yangu ya simu, nikamwambia hapana shaka.


Nilichokisoma baina ya mawasiliano ya hawa mashemeji zangu wawili, kuanzia kwenye kuchart mpk ninapoongea nao ni dhahiri au kwa lugha nyepesi naweza kusema wamenizimia na wanahitaji huduma yangu ya kucare kama wanavyosema, japo nimefupisha hii story yangu lakini katika text ambazo nilikuwa nachart nao mpaka leo hii hawaishi kuniulizia mara upo kazini, au upo kwenye foleni na gari ndio nikaamini kwamba GARI NI UCHAWI MKUBWA SANA KWA HAWA VIUMBE WANAOITWA WANAWAKE na hiyo ni ndani ya Jumamosi mpk Jumanne tuu.

Ushauri wangu kwa Dada, Wamama na Wanawake wote kwa ujumla ni kwamba kuna msemo unaosema kwamba ROME WAS NOT BUILT IN ONE DAY, unapokuwa na m2 wako kwenye mahusiano na ukaona kwamba mambo yake hayajakaa vizuri sio uanze kumponda kwa w2 au m2 ambae umemjua kisa usafiri au v2 anavyomiliki wakati hamjui, Uvumilivu ni jambo bora kabisa katika Maisha ya kila Mwanadamu. Asanteni kwa Kunisikiliza.

 
Kaunga

Kaunga

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2010
Messages
12,580
Likes
868
Points
280
Kaunga

Kaunga

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2010
12,580 868 280
Acha fix wewe, umewalipia bill; inamaana pesa waliyosave (maana hawakuwa na miadi na wewe) walishindwa kulipia taxi?

In as much nakubaliana na umuhimu wa usafiri kwa wapendao lkn njia zako za kupresent mada (kujipa extra attention/importance) inaongea mengi zaidi.
 
B

ben van mike

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2010
Messages
468
Likes
32
Points
33
B

ben van mike

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2010
468 32 33
Sidhani ka ni fix dada Zetu hawataki shida Kabisa yaaani Kama sio ustaarab wako mkuu mtu mwingine angewahudumia fasta na hao sio mademu wa kuoa
 
IGWE

IGWE

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2011
Messages
8,827
Likes
3,157
Points
280
IGWE

IGWE

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2011
8,827 3,157 280
Naona unaendelea na story zako za kujifagilia kama kawaida yako_ndio kawaida ya washua lakini...lo!
 
S

sawabho

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Messages
5,232
Likes
1,857
Points
280
S

sawabho

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2011
5,232 1,857 280
Tenda wema nenda zako, usingoje shukrani.
 
Gamaha

Gamaha

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2008
Messages
2,863
Likes
1,069
Points
280
Gamaha

Gamaha

JF-Expert Member
Joined Jul 17, 2008
2,863 1,069 280
Jamani jumamosi kidogo nivunje ndoa na gari ya kuazima, nilikuwa ndio nimekalibia kufika nyumbani si nikakutana na mabinti wawili wazuri wakawa wananikodolea macho na kutabasamu, na mipombe yangu kichwani nikawapa busu la mbali basi walivyoona napaki gari wacha waje kunisalimia kumbe mimi ndio napaki gari kwangu. Ilibaki kidogo nikimbie bahati nzuri wife hakutoka nje.
 
M

Mokoyo

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2010
Messages
15,208
Likes
2,355
Points
280
M

Mokoyo

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2010
15,208 2,355 280
hahahahahah nicheke mie leo sina pesa ya lunch
Acha fix wewe, umewalipia bill; inamaana pesa waliyosave (maana hawakuwa na miadi na wewe) walishindwa kulipia taxi?

In as much nakubaliana na umuhimu wa usafiri kwa wapendao lkn njia zako za kupresent mada (kujipa extra attention/importance) inaongea mengi zaidi.
 
Kiwa

Kiwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Messages
2,112
Likes
207
Points
160
Kiwa

Kiwa

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2011
2,112 207 160
KiVEROSSA?!!!
Dah mkuu mbona umetaja as if sio kitu kabisa wakati wengine wanahustle usiku na mchana na bado hawaipati

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
43,162
Likes
40,565
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
43,162 40,565 280
Siku hizi hata watoto wa kiume wananaswa kiulaini na ulimbo wa magari
 
Passion Lady

Passion Lady

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2012
Messages
8,702
Likes
467
Points
180
Passion Lady

Passion Lady

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2012
8,702 467 180

mwanamke mpumbavu asiyejitambua
atashoboka na gari la mwanaume,ila mwanamke mwerevu
mwenye kujua thamani yake,anaejitambua gari c chochote, kalaghabaooo na kushoboka kwao!!
 
A

ayanda

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2013
Messages
1,342
Likes
218
Points
160
A

ayanda

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2013
1,342 218 160
Mkuu ni kweli kabisa! Gari ndio mtama wa watoto wa kike apa town. Utasikia baby come and pick me up apa Mlimani city...
ha ha ha ha kiukweli gari lina tia nyege, yaani asikwambie mtu wanawake wengine tunapenda magari. yaani sijui why?

yaani mtu hujatongozwa, chupi inaanza shuka yenyewe kwa kuona gari zuri tu ha ha ha ha

haya mambo ya mujini jamani yananiachaga hoi!

ila mimi si kivileeeeeeee kwa magari
 

Forum statistics

Threads 1,273,084
Members 490,268
Posts 30,470,767