Nimeamini kwa sasa Watanzania hatuko huru, nimekamatwa kisa kunywa bia kabla ya saa 10

Mzee Chapuuka

Member
Apr 21, 2017
97
243
Wakuu salaam,

Naandika Uzi huu Kwa uchungu na hasira baada ya kuachiwa mida hii kutoka selo Central.

Ni hivi, mimi napiga mishe zangu tu sio muajiriwa wa serikali wala nini.. Sasa jana mida ya saa 9 kasoro nikaona niingie bar flani hapa Mjini Mwanza nipate moja moto moja baridi.

Ile naagiza chupa ya pili kabla sijaanza kuinywa ghafla naona jamaa wanakuja wananiamrisha nisimame na kutaka kunifunga pingu, nikawauliza kosa langu nini wananiambia wee huna kazi unakunywa pombe saa hivi nkawaambia kazi ninayo na hizi pombe nakunywa Kwa pesa yangu mida hii ndo natoka kazini.

Jamaa wakaning'ang'ania wakanifunga pingu wakawachukua wahudumu wa kaunta tukapelekwa central.

Wakati tunaelekea central nkawaambia nifungueni hizi pingu wakagoma eti nimwambie Magufuli ndo anifungue kisa yeye ndo kaweka Sheria watu kunywa ni kuanzia saa 10 jioni.

Nkajiuliza ni lini Bunge limepitisha hii Sheria au ni tamko la mtu mmoja mwenye madaraka ndo anataka kutunyima Uhuru Watanzania wenzake? Kama kunywa nimekunywa Kwa pesa yangu nliyoitafuta Kwa jasho langu na nna kazi yangu Kwa nini niingiliwe Uhuru wangu na kupangiwa matumizi?

Kiukweli nimeamini sasa hatuko huru. Kule selo nimekuta watu kibao wengine Kwa kesi za kukutwa guest mchana wakiwa na Malaya wanagegeda yani sasa hadi mambo ya unyumba tunapangiana muda wa kufanya? Hii sio haki.

Nimelala central wamenipiga fine ya 50 thousands, ila police nao waache unoko kufuatilia starehe za watu. Waende wakapambane na uhalifu mkubwa huko mtaani na sio kukamata watu wanaojiburudisha tena kwa kinywaji halali.

We Need a Freedom.
 
Mwaka 1968 Nyerere alisaini sheria namba 28 ijulikanayo kama "The Intoxicating Liquor Act No 28, 1968" ambayo inatoa mamlaka kwa Afisa wa Halmashauri kutoa leseni za kuuza pombe. Kutolewa kwa leseni hizo kunaambatana na masharti kadhaa kwa mwenye duka ikiwemo ratiba ya kuanza kuuza pombe.

Ratiba hiyo iko tofauti kati ya maeneo ya jiji, miji na vijijini, na huwa itabadilishwa mara nyingi tu. Nakumbuka mara ya mwisho ilibadilishwa 2014 japo sikumbuki muda hasa. Fatilia..... Unaweza kuigoogle... (ina amendments kibao)
 
Back
Top Bottom