Nimeamini kuwa mtoto huja na sahani(riziki) yake

Kawaida riziki ya mtu hua inapitia kwenye mikono ya mtu mwingine.
Binasfi nilikua na msela wangu shughuli yake ilikua umachinga(wale wa kutembeza bidhaa mitaani), alijichangachanga akaoa, muda mfupi baada ya kuoa milango ya rizki ikafunguka akamiliki duka, ndani ya miaka 4 alikua na maduka 3, akajenga na akanunua chombo ya usafiri, mambo yalikua si haba na akajaaliwa mtoto.
Pesa ilivyomkolea akaongeza mke wa pili, na mapenzi kwa mke wa kwanza yakapungua.
Kufupisha story mke wa kwanza pamoja na mwanae walipata ajali wakafariki, hapo sasa kimbembe ndio kilipoanza.
Mwaka mmoja baada ya mkewe na mtoto kufariki biashara zikayumba vibaya mno na migogoro kwa mke aliyebaki ikawa haiishi.
Jamaa alienda kukopa bank ili kufufua biashara zake na dhamana akaweka nyumba.
Biashara ziligoma matokeo yake baada ya kashindwa kulipa deni nyumba yake ikapigwa mnada na mke akadai talaka wakaachana.
Jamaa alikua kama anaanza kudata hivi ila sasa hivi tunamshuru Mungu ameanza kukaa sawa na amefungua kagenge.
Binasfi maisha ya jamaa yamenipa somo moja kubwa sana.
 
Nilikuwa na maisha magumu baada ya kuoa, ila nilipomzaa mtoto wangu wa kwanza P, maisha yakachange. Pesa haijakatika kwa miaka 3 mfululizo. Na ikikata pesa ndani ya masaa machache napata.

Sasa Jumatatu asubuhi nikampeleka P kwa maza wake mdogo aka shem. Duuuuhhh wiki hii pesa ilikata kabisa. Ndipo nikakumbuka maneno ya wife ambayo aliyasema muda kidogo kuwa kuzaliwa kwa P kumeleta neema.

Leo namfuata mtoto wangu.
Nimecheka sana Mkuu hiyo sentensi ya mwisho. Anyway mimi sio mfuasi sana wa hayo maneno ila ninaamini kuwa Mwenyezi Mungu hukupa kwa wakati autakao yeye. Wakati nimepata watoto mapacha kauli za "Ujipange mapacha sio mchezo" zilikuwa hazikauki masikioni mwangu ila Mungu ni mwema hakuna kilichonipungukia sana sana nazidi kuuona mkono wake.
 
Nimecheka sana Mkuu hiyo sentensi ya mwisho. Anyway mimi sio mfuasi sana wa hayo maneno ila ninaamini kuwa Mwenyezi Mungu hukupa kwa wakati autakao yeye. Wakati nimepata watoto mapacha kauli za "Ujipange mapacha sio mchezo" zilikuwa hazikauki masikioni mwangu ila Mungu ni mwema hakuna kilichonipungukia sana sana nazidi kuuona mkono wake.
Mungu mkubwa.
Nimejifunza kitu kwa ushuhuda wako huu
 
Back
Top Bottom