Nimeamini jamani hakuna kitu kigumu kama wajasiriamali

sisi wauza hardware kidogo afadhari.
Kiboko yetu tukiambiwa tukae lock down.
Asikwambie mtu kukaa nyumbani baba,mama watoto kunachoshaaaa.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
Just wait, muda si mrefu hakutakuwa na mtu wa kujenga. Uchumi unaenda kuanguka vibaya sana endapo gonjwa hili litaendelea kwa miezi mitano ijayo duniani. Uchumi utaanguka vibaya, biashara karibu zote zitaanguka, tunaweza rudi kwenye kubadilishana kitu kwa kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Germany watu zaidi ya 2 million wamepoteza kazi.
Lakini uzuri wenzetu wanalipwa 60% ya mshahara wao wa kawaida na hii wanalipwa na wizara ya kazi(jobless money)
Hata hiyo nayo sio sustainable Endapo watu wengi zaidi watapoteza kazi. Huwezi kuwalipa kwa muda mrefu watu kama hamna uzalishaji, hiyo wizara nayo inaweza kufilisika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili balaa ni suala la how long will the crisis exist

BUT

Every body will experience the pain

Walianza mashirika ya ndege

Wakaja makampuni ya bahati nasibu

Wakaja sekta ya utalii na chain yote

Sasa ni ma hotel ya ndani na waendesha shughuli za masherehe

Wasanii, Wanasoka (hasa hasa Ulaya) wameanza kuumia (japo wao wana saving)

Wakati huo huo wajasiriamali wadogo wadogo kama wale wa minadani n.k.

Sekta binafsi kama shule binafsi na staffs wote, vyuo binafsi, daladala n.k.

Tutaenda na mwisho watumishi wa Serikali wanaweza kuambiwa wapunguziwe % flani ya mshahara

Wenye nyumba za kupanga nao wameanza kuambiwa wawe wavumilivu kwenye kukusanya kodi

Hata hao wa hardware na wengine ambao kwa sasa wapo stable wataumia maana uwezo wa watu kununua utapungua, na vipaumbele itakuwa mahitaji ya msingi kama msosi ambapo watu watakuwa hawana hela za kununua

Najaribu kuwaza, mwakani tunaweza tusiwe na wanafunzi wa kidato cha kwanza, cha tano na wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni




Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly! Kama covid19 itakuwepo kwa miezi mitano zaidi, hakuna mtu atakayeacha kuguswa na pigo kubwa la kiuchumi, hadi watumishi wa umma watapata pigo ambalo hawajali shuhudia miaka mingi iliyopita. Hakuna sekta itakayobaki salama, isipokuwa wazalishaji chakula pekee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kumbuka sasa hivi vilio vyote unavyoviona humu, corona haijamaliza hata mwezi hapa nchini na wala hatujaingia lockdown. Na ukweli ni kwamba, hata dawa ya corona ipatikane leo, itachukua si chini ya mwaka kwa hali kuanza kurudi kama ilivyokua mwanzo. Sasa niambie ni wafanyabiashara wangapi wanaweza kujiendesha kwa kipindi hicho bila income yoyote?
Mkuu athari za corona tunazopata sasa ni matokeo ya korona kuenea huko duniani, ikienea zaidi hapa TZ hali itakuwa mbaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: amu
Poleni sana..angalau Una bi mkubwa wa wa kurudisha mpira Kwa kipa..

Sasa Mr nae kashindwa kuokoa jahazi?
😂😂😂😂we jamaa, nimecheka kijinga sana, si wengine ukirudisha mpira nyuma unajifunga, kipa hayupo wa kumrudishia lazima uanze kati mpira usonge mbele. Kanuni moja tu.
 
Huku nilipokuja nilitaka niingiwie na tamaa nikicheki mkaa gunia buku 8k, limao mmoja shambani bei yake ni shilling 10 ya kitanzania. Kuku ni kama bei ya singida tu.

Nikawaza nikawazua nikajisemea nikomae ni kitu kimmoja tu kilichonitoa dar na si kingine bali 'mawe'

Maana nikitaka vyote nitarudi kulekule kwa mwanzo.


Kwaiyo kama usemavyo ni vizuri ku deal na kitu kimoja tu.
Wapo huko kwenye mkaa wa 8k ndugu? Nina kahifadhi hapa natafuta fursa
 
Kwanini unasema ni tapeli?
Nilienda pale na washkaji zangu wawili. Tumefika tunaoneshwa fomu, fomu inaonesha gharama ya kumkuza kukuchotara ni 7,000 kisha wao wanaenda kumuuza 14,000. Faida 7,000 ndio ya mwekezaji. Tukatoka nje wanauza kuku hapohapo. Nikamuuliza sista anaeuza kuku bei gani akaniambia kuku 6,500 chotara ameshakuwa packaged. Nikamuuliza hii ni bei ya mwanachama au? Akaniambia hapana ni bei ya wote. Tukawasha gari tukaamsha hapohapo.

Lingine ni kuwa hawa watu wamebadilisha jina. Kabla walikuwa wanaitwa TM Agribusiness na walikuwa wana 'mashamba' unawekeza kwa eka wanalima wakivuna unapata faida hivihivi 'mara mbili'. Bimkubwa aliinvest hapo wakazungushwa zaidi ya mwaka hamna returns zozote bahati nzuri kuna insurance hivyo waliweza kupata pesa zao. Kwa hii ya pili ipo pia hivyo natumai watawalipa mambo yatapoenda mrama baada ya kuwazungusha. Hii Mr. Kuku imesajiliwa Febuari mwaka huu ukitazama kwenye registration zao za Brela.

Lastly mkataba wao ni wa upande mmoja. Shahidi wako na mwanasheria wa mkataba ni wa kwao. Hivyo kiujumla kama hili jambo likienda kortini upande wao una nguvu kushinda wewe. Kamwe si mkataba wa kuingia iwapo uoande mmoja una nguvu kushinda wewe katika kuusimamia mkataba.
 
Hii nikwa kila mtu aisee mi nna broiler zimeshakua wateja hakuna na hela ya chakula karibu itaniishia yaan nawaza kwani nikiwatoa nje hawatasavaivu mana siwez endelea kulisha.
Hii ni awamu ya pili ya kwanza ela nliona tamu sasa karona hii kubabeki kama nilieeeee.
 
Ila we jamaa umejua kunichekesha Broiler uwatoe nje
Hii nikwa kila mtu aisee mi nna broiler zimeshakua wateja hakuna na hela ya chakula karibu itaniishia yaan nawaza kwani nikiwatoa nje hawatasavaivu mana siwez endelea kulisha.
Hii ni awamu ya pili ya kwanza ela nliona tamu sasa karona hii kubabeki kama nilieeeee.
 
Pole mkuu
Mwezi wa kwanza galfriend wangu alianguka akiwa anaenda dukani akavunja Mkono, ni wiki ya pili tu tangu nitoke kulipa kodi ya ofisini kwangu na ninapoishi. Nikahangaika kupata fedha ya kwenda kumtibia nikafanikiwa kiasi fulani akatiwa POP, nimemuuguza kwa miezi miwili mpaka alipotoa POP, nikamwambia aende kwake kwanza angalau nipate nafasi ya kukusanya kodi ya ofisini, mwezi ujao.

Biashara mwezi wa tatu ikawa ya kuvuta na kamba, inapatikana pesa ya kula tu inaisha. Hamna kusave wala nini, mara upande wa pili kidudu kikashika speed hapa kwetu. Sasa hivi nimeamua itakavyokuwa na iwe tu aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii yako ya kujaribu hiki na kile kwa wakati mmoja nimeshafanya sana uko nyuma na Mara zote nimedondokea pua mkuu.

Sababu ya kufanya kitu zaidi ya viwili nimejikuta gari iliyokuwa ikibeba abiria toka simu 2000 to gongolamboto ipo juu ya mawe kwa miezi kadhaa sasa na uwezo wa kuitoa sina, najikusanya kidogo kidogo irudi njiani.

Sasa hivi na komaa na kitu kimoja tu ambacho kinaonekana kwenye avater yangu.( biashara ya mawe ya dolomite)

hata wahenga walituasa
Mshika mawili mmoja humponyoka.
Hii daladala... macho akili mawazo vyote viko hapo, nazichanga...nikiwa tayari nitakuja kupata ushauru

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom