Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,962
Nimeamini kwenye maslahi CCM ni kitu kimoja, sasa hii itakuwa kazi kubwa kwetu kuanzia sasa kupambana na kuiondoa CCM na wataondoka tu.
Miezi michache iliyopita kulikuwa na bifu kubwa sana Kati ya Mataga(CCM ya mwendazake) na CCM asilia(ile ccm ya mafisi) , naiita CCM ya mafisi maana hata mwenyekiti wao kipindi hicho Jk aliita hivyo.
Hilo bifu limezikwa baada tu ya wanamageuzi wote nchini kuanza kudai katiba mpya, hapo ndio mpate jibu kuwa CCM kwenye maslahi huwa ni kitu kimoja.
Ukitaka kuamini hili angalia pia wakati wa uchaguzi mkuu uliopita wa 2020 waliungana nchi nzima kupita bila kupingwa, uchaguzi ulivyoisha bifu likaendelea.
Nilitegemea CCM Mataga kipindi hiki wangeungana na wanamageuzi wote kudai katiba mpya, ila ndio kwanza wamekuwa wapingaji wakuu wa katiba mpya tena kwa nguvu kubwa sana.
Wewe ona hata leo hii wote wameungana kupinga kauli ya kamanda mdude, ila tujiulize ni lini CCM waliwahi kuwa na staha?
Mwenyekiti wao wa sasa si ndio yule aliyesema Askari wao hawezi kupoga risasi 16 akakukosa, akipiga risasi tatu akikukosa basi hana kazi. Watasema ilikuwa kauli ya kisiasa, basi hata ya mdude ni ya kisiasa.
Makamanda popote mlipo bado nawaomba msichoke kumbukeni tumetoka mbali sana na tunakaribia kufika. Tumepita kwenye tawala za kila namna tulikuwa ngangari na pamoja hivyo tusikubali kuingia mtego wowote wa CCM.
Na hii inaonyesha wazi kuwa madai ya katiba mpya yana mashiko ndio maana unaona sasa hivi kila nyoka anatoka pangoni.
Katiba mpya kwanza