Nimeamini bongo kwenye muziki kuna uchawi; yaani 'ni wewe' haitambi?

Jomy

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
550
500
Nikiri kabisa nilikua siujui ila one nikasikia dogo mmoja anausikiliza alafu kaweka repeat 1 ikabidi niutafute mpaka leo most played song kwenye Playlist yangu
 
Eyce

JF-Expert Member
Mar 16, 2016
3,872
2,000
Killy sijui tatizo nini

Toka anaanza muziki huwa ana nyimbo nzuri na video kali lakini hatoki

At least alipokuwa kwa kiba ile kupewa nafasi kubwa akaanza kuonekana ila aliporudi kwa konde, karudi kule kule
 
Qwy

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
6,143
2,000
Nyimbo Kali sana! Imetulia Ila Wakianza kuimba mashairi Yao ya Kichoko eti "usizinyoe nikusuke mabutu" like wtf! mashairi ya namna hii nayachukia sana! Hapo Harmoize Bado hajaanza Kuchanganya R na L Yani ndo nachoka kbsa
Huwa hizo L na R anazichanganya zaidi akijilazimisha kile Kiingereza chake cha kuungaunga, lakini mdogomdogo labda mbele ya safari atajifunza jinsi ya kuzitumia kiusahihi.
 
Aug 23, 2021
24
45
Mapenzi asili yake upofu ukipenda huoni
Usishangae mtu kaacha minofu kafata ya vichochoroni.

So kila mtu anapenda cha kwake nyimbo ukiipenda wewe sio lazima na Msigwa, Mdee na Tulia waipende.
 
Tripple Jay

JF-Expert Member
Jul 9, 2017
215
500
nawasalimu kwa jina la JMT!
Nauzungumzia huu wimbo wa Killy aliyomshirikisha Harmonize uitwao 'ni wewe'. Jamani, huu wimbo unachosababisha usitambe ni nini haswaa kama sio uchawi tu?!!!

Melody nzuri,
Mashairi mazuri,
Beat poa kabisa ya kizamani na kisasa iliyotulia,
Shooting ni njema kabisa.

Vyote vinastahili kusikilizwa harusini, clubs na hata mitaani. Ajabu ni kuwa napita humo mwote na ni nadra kuusikia.

Nazisikia nyimbo zingine zinazopigwa mara kwa mara,.....nabaki nashangaa tu!

Mwishowe nimeona nihitimishe tu kuwa kumbe hapa Bongo kwenye muziki inabidi uroge pia, yaani ni WACHAWI KUMBE!
Ttzo wabongo hawajuagi wimbo mzuri hlf km wamekremisha wasanii. Kuna nyimbo nying nzuri tu lkn hazipewi airtime
 
Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,462
2,000
Kuna miziki mingi tu mitaani mizuri sana tu unasikia ghafla unauliza nani kaimba huu unaanza kutafuta kuna vipaji vinapotea sana na ngoma nyingi unaumia hazisikiki hawa wasanii wakubwa wanatumia nguvu sana kusukuma ngoma zao nguvu kubwa sana sio kitu kibaya lakini kuna vipaji vingi lakini hawana uwezo wa kutumia pesa kufanya promo na media zetu bila vipesa haziendi. Itokee Radio moja isukume kazi zinazopetea mitaani nzuri lakini hazina promo hii ndio shida kubwa kwa sanaa. Hawa wasanii wakubwa utasikia tunakuta kusaidiana kuinua sanaa yetu lakini wao hata siku moja huwezi kuona wamepost kazi nzuri ya msanii mwenzake hata siku moja lakini wakiwa kwenye media utasikia neno sisi tusaidiane ila hawajafanya kitu pamoja na ushawishi wao mkubwa na hili naongelea wasanii wakubwa mtakuwa mnawajuwa. Ni wote hawasaidii mtu ku push kazi za wasanii wadogo lakini kazi nzuri sio una push kila mtu ila kazi nzuri itambue mpost apate nguvu na yeye.
 
Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,462
2,000
Wasanii wengi wadogo wanakata tamaa njiani kwa sababu ya hawa wakubwa na kuna watu wanaimba sana tena sana kuliko hawa masimba sijui matembo lakini atatoka vipi? juzi nimeona clip tu insta nikapenda nyimbo ndio natafuta mbona ngoma nzuri kumbe ya Mrwanda sijui anaitwa Meddy inaitwa queen of sheba nilidhani ya bongo ngoma nzuri sana lakini sikuwahi kuisikia. Kwa industry hii hawa vijana wadogo nawaonea huruma sana watatokaje. Ngoma nzuri moja akipushiwa kwa kumpost inamsukuma msanii sana. Usimpe pesa sukuma kazi nzuri watu wamjuwe lakini ukweli sio Tembo, Simba wala Kiba wanataka mtu aje hawataki ni ile kujinadi tu tusaidiane ni unafiki tu sio nia yao.
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
4,335
2,000
nawasalimu kwa jina la JMT!
Nauzungumzia huu wimbo wa Killy aliyomshirikisha Harmonize uitwao 'ni wewe'. Jamani, huu wimbo unachosababisha usitambe ni nini haswaa kama sio uchawi tu?!!!

Melody nzuri,
Mashairi mazuri,
Beat poa kabisa ya kizamani na kisasa iliyotulia,
Shooting ni njema kabisa.

Vyote vinastahili kusikilizwa harusini, clubs na hata mitaani. Ajabu ni kuwa napita humo mwote na ni nadra kuusikia.

Nazisikia nyimbo zingine zinazopigwa mara kwa mara,.....nabaki nashangaa tu!

Mwishowe nimeona nihitimishe tu kuwa kumbe hapa Bongo kwenye muziki inabidi uroge pia, yaani ni WACHAWI KUMBE!
Mtu mweusi akiona mafanikio,yeye anaona uchawi na madawa ya kulevya ndio yametumika,aamini katika juhudi na kufanya kazi kwa bidii,
Wimbo hautambi na kuwa maarufu tu!!lazima ufanye promo!!sasa wewe unafanya corabo na Harmonize,anayeishi kwa kiki za kukamatwa na polisi Kenya,harafu unataka wimbo utambe!!piga corabo na Mond,mtu ananunua gari ya 800M!,hapo wimbo utavuma.
Lakini kumbuka,Mond hakufika hapo kirahisi,wimbo wake wa mbagala ndio uliomtambulisha,Alipo piga corabo ya kidogo dogo na Psquare na davido wa Naija,jina lake likawa kubwa.
Sasa huo wimbo unaousifia,jamaa angepiga corabo na wanaija au wasouth,ungefika mbali kama wimbo wa bia tamu.hakuna uchawi,hapo no juhudi binafsi tu
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
4,335
2,000
Wasanii wengi wadogo wanakata tamaa njiani kwa sababu ya hawa wakubwa na kuna watu wanaimba sana tena sana kuliko hawa masimba sijui matembo lakini atatoka vipi? juzi nimeona clip tu insta nikapenda nyimbo ndio natafuta mbona ngoma nzuri kumbe ya Mrwanda sijui anaitwa Meddy inaitwa queen of sheba nilidhani ya bongo ngoma nzuri sana lakini sikuwahi kuisikia. Kwa industry hii hawa vijana wadogo nawaonea huruma sana watatokaje. Ngoma nzuri moja akipushiwa kwa kumpost inamsukuma msanii sana. Usimpe pesa sukuma kazi nzuri watu wamjuwe lakini ukweli sio Tembo, Simba wala Kiba wanataka mtu aje hawataki ni ile kujinadi tu tusaidiane ni unafiki tu sio nia yao.
Kwani unafikiri nani alitaka Diamond,Kiba,harmonize atoke?
Hii Dunia hakuna anayejari kama itatoka au laa,lazima ujipange,mazee!!tafuta wimbo wa mbagala au nakshi nakshi wa Kiba,uone jinsi walivyokuwa choka mbaya,kipindi hicho waliokuwa wanatamba ni eastcost team watoto wa kidosi,mwanafa,ay,juma nature,Mond alikuwa hajulikani anaonekana kama chokoraa tu,jamaa wali hustle sana, hiyo ni 2008+
Sasa hv Hawa underground waliozaliwa juzi,wakimuona Mond,ananunua Gari ya 800M!wanataka awasaidie watoke hivi hivi bila kulipa gharama!!there is nothing like a free lunch jombaa,weka kitu mezani,watu waone,utapiga pesa,
Enzi za kina juma nature,gangwe mob,mabaga fresh,kulikuwa hakuna YouTube,Wala Instagram Wala smart phone,nyimbo zilikuwa zinauzwa kwenye Kanda,tape,au CDS,leo hii platform ni kubwa tu!!
Vijana pambaneni vipaji mnavyo!msitegemee mond,au kiba ataweka mgongo wake mpande Bure Bure kabisa!!! No way mazee
 
Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
9,161
2,000
Mtu mweusi akiona mafanikio,yeye anaona uchawi na madawa ya kulevya ndio yametumika,aamini katika juhudi na kufanya kazi kwa bidii,
Wimbo hautambi na kuwa maarufu tu!!lazima ufanye promo!!sasa wewe unafanya corabo na Harmonize,anayeishi kwa kiki za kukamatwa na polisi Kenya,harafu unataka wimbo utambe!!piga corabo na Mond,mtu ananunua gari ya 800M!,hapo wimbo utavuma.
Lakini kumbuka,Mond hakufika hapo kirahisi,wimbo wake wa mbagala ndio uliomtambulisha,Alipo piga corabo ya kidogo dogo na Psquare na davido wa Naija,jina lake likawa kubwa.
Sasa huo wimbo unaousifia,jamaa angepiga corabo na wanaija au wasouth,ungefika mbali kama wimbo wa bia tamu.hakuna uchawi,hapo no juhudi binafsi tu
Tuna tatizo lakumkutukuza shetani hatuamini kwenye ukuu wa Mungu na jitihada mtu anavyostruggle na kujituma na kukutana na changamoto nyingi usikii kuwa ni freemason au anauza madawa ya kulevya ila akishafanikiwa ndio yanakuja haya majina
 
Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
9,161
2,000
Kwani unafikiri nani alitaka Diamond,Kiba,harmonize atoke?
Hii Dunia hakuna anayejari kama itatoka au laa,lazima ujipange,mazee!!tafuta wimbo wa mbagala au nakshi nakshi wa Kiba,uone jinsi walivyokuwa choka mbaya,kipindi hicho waliokuwa wanatamba ni eastcost team watoto wa kidosi,mwanafa,ay,juma nature,Mond alikuwa hajulikani anaonekana kama chokoraa tu,jamaa wali hustle sana, hiyo ni 2008+
Sasa hv Hawa underground waliozaliwa juzi,wakimuona Mond,ananunua Gari ya 800M!wanataka awasaidie watoke hivi hivi bila kulipa gharama!!there is nothing like a free lunch jombaa,weka kitu mezani,watu waone,utapiga pesa,
Enzi za kina juma nature,gangwe mob,mabaga fresh,kulikuwa hakuna YouTube,Wala Instagram Wala smart phone,nyimbo zilikuwa zinauzwa kwenye Kanda,tape,au CDS,leo hii platform ni kubwa tu!!
Vijana pambaneni vipaji mnavyo!msitegemee mond,au kiba ataweka mgongo wake mpande Bure Bure kabisa!!! No way mazee
Umeongea jambo la msingi sana wafuate ushauri wako watafika mbali.
 
RobeCisco

Member
Apr 25, 2022
9
45
Tumia
Mchawi wake ni boss wake,kila siku anatoa nyimbo anataka kusikika yeye. Huyo dogo bora angebaki kwa Kiba au angeamua kuwa mwenyewe.

Harmonize hawapi nafasi wasanii wake na hana muda ya kuwapromoti na mwezi huu wa tano anatoa album nyingine ,huku akiacha kuipromoti EP ya Killy iliyotoka m
Mchawi wake ni boss wake,kila siku anatoa nyimbo anataka kusikika yeye. Huyo dogo bora angebaki kwa Kiba au angeamua kuwa mwenyewe.

Harmonize hawapi nafasi wasanii wake na hana muda ya kuwapromoti na mwezi huu wa tano anatoa album nyingine ,huku akiacha kuipromoti EP ya Killy iliyotoka mwezi wa pili.
Tumia akili Konde na Kiba nani ana fan base kubwa saivi BTW nyimbo imevuka over 2M views in YouTube kitu ambacho ni kikubwa huyo Kiba saivi anatoa nyimbo inachukua hata wiki kufika 1M je hao walioko chini yake itakuaje
 
Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,462
2,000
Kwani unafikiri nani alitaka Diamond,Kiba,harmonize atoke?
Hii Dunia hakuna anayejari kama itatoka au laa,lazima ujipange,mazee!!tafuta wimbo wa mbagala au nakshi nakshi wa Kiba,uone jinsi walivyokuwa choka mbaya,kipindi hicho waliokuwa wanatamba ni eastcost team watoto wa kidosi,mwanafa,ay,juma nature,Mond alikuwa hajulikani anaonekana kama chokoraa tu,jamaa wali hustle sana, hiyo ni 2008+
Sasa hv Hawa underground waliozaliwa juzi,wakimuona Mond,ananunua Gari ya 800M!wanataka awasaidie watoke hivi hivi bila kulipa gharama!!there is nothing like a free lunch jombaa,weka kitu mezani,watu waone,utapiga pesa,
Enzi za kina juma nature,gangwe mob,mabaga fresh,kulikuwa hakuna YouTube,Wala Instagram Wala smart phone,nyimbo zilikuwa zinauzwa kwenye Kanda,tape,au CDS,leo hii platform ni kubwa tu!!
Vijana pambaneni vipaji mnavyo!msitegemee mond,au kiba ataweka mgongo wake mpande Bure Bure kabisa!!! No way mazee
Ni kweli ila na wao waache wanapokuwa yamewafika shingoni huko serikalini kujinasibu mbele ya umma sisi tunapigana na kuwasaidia vijana wenzetu tuwe wengi tutoke tupigane na wa Nigeria tuwe wengi na bla bla nyingi haya ni maneno yao ila uhalisia hawana habari kuwasaidia wengine watoke. Nachopinga mimi kauli zao na mara nyingi tu utasikia tujitahidi kusaidiana tuwe wengi. Kurudi kwenye mada yako hakuna cha bure ni kweli basi wangekuwa wa kweli tu ukitaka boost gharama ni hii unajuwa biashara. Zamani hakukuwa na digital platform zamani watu ni umaarufu tu hakukuwa na pesa ni kama mpira zamani. Mbona Ronaldo kasema tu one post 1.5 Million$. Diomond anaongea sana hili jambo tuwasaidie wengi tutoke tukapigane nje tuwe wengi sasa swali yeye kamsaidia nani?
 
MoseKing

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
2,591
2,000
Muziki wa Tanzania una makundi ya kimaslahi.

Media zinamiliki Wasanii na Matamasha. Huku zikipewa nguvu na Mashabiki uchwara waliojaa Chuki.

Hakuna independent promoters.

Yaani, Clouds wana tamasha la la Fiesta, na hivyo wasanii wataokubali kutumbuiza kwenye Tamasha lao cheaply ndio watakaokuwa wanapata strong promotion kwenye Media yao.

Hivyo hivyo kwa Wasafi ( Wasafi TV ), E! TV ( Muziki Mnene) na EATV.

Kwahiyo Kama wewe haupo kwenye MTANDAO huo maana yake, hutapata SHOWS Wala ngoma zako hazitapata rotation kubwa kwenye main stream media.

Na hii ndio sababu sasa hivi Msanii 'kutoka" na kuvuma nje ya mfumo huu ni ngumu sana. Hali hi, imewapoyeza pia wasanii wa zamani.

Vile vile, Kama Msanii huna uwezo wa kuandaa shows zako mwenyewe na Matamasha ndio basi tena.

Na kibaya akili za wabongo zilivyo na Ushabiki uchwara, mpaka playlist anatengenezewa, maana mpaka aambiwe na media fulani kiwa hiyo ngoma ni Kali.
 
joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
9,865
2,000
Sasa wasanii wake wamefika wapi? Huyo kili mwaka sijui wa sita bado underground,Ibrah mwenyewe unaelekea mwaka wa tatu badohajasimama. Brother Diamond alishakaa zaidi ya miezi sita ili kumpromoti Harmonize, badala kuambiwa dogo hajui kuimba na sauti ya Harmonize imefanana na yake, Diamond na WCB resources zote walielekezaza kwa Harmonize (humu JF kuna thread kibao zilikuwa zinaponda sauti ya harmo inafanana na Diamond),Mondi aliipa muda sauti ya Harmo waizoee na kutofautisha na yake.

Ibra na Killy si wabaya tatizo boss wao, Angella katoa Kioo jana, nyimbo nzuri yy wiki ijayo tarehe 20 anaachia album hiyo nyimbo itapromotiwa vipi, wakati resource zote za Konde zitakuwa zina ipromoti hiyo album.

Ila sijui may be kwake label ni show off au kwa ajili ya kuwatumia watoto kujijenga yy na si kibiashara, anawapotezea mda madogo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom