Mzalendo39
JF-Expert Member
- Apr 17, 2015
- 881
- 1,033
Nina takribani mwezi hivi sasa toka nikutane kimwili na mpenzi wangu wa zamani na kwa bahati mbaya sikutumia kinga nilianza kuhisi kuugua ugonjwa huu kama wiki mbili zilizopita na kwa bahati mbaya mke wangu ananieleza anahisi kuwashwa, ingawa kwangu mimi nimeanza matibabu.
Sasa namna ya kumueleza mke wangu au kumshawishi akapime nashikwa na kigugumizi maana mwanaume nitaumbuka na nimekosa raha takribani siku ya nne hivi sasa toka mke wangu anieleze anawashwa na sina amani ndani ya nyumba yangu nimesingizia naumwa homa ili kuepuka usumbufu wa usiku.
Naombeni msaada nifanye nini ili mke wangu nae apate matibabu bila ya mimi kuumbuka maana najua mimi ndio chanzo kikuu.