VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Niko hapa Iringa. Nimetokea Ruvuma. Classmate wangu wa sekondari na chuo kikuu aliniomba nipitie kwake hapa Kihesa,Iringa kumsabahi baada ya kumwambia natokea Ruvuma kurejea Dar es Salaam. Nitakuwa hapa hadi Ijumaa.
Sote ni makada wa CCM,tena wakongwe. Sote tumewahi kushika,na kuendelea kushika nyadhifa mbalimbali chamani na hata Serikalini. Sote,kichama,tumeishia U-NEC. Tunapokutana,siasa huzungumzwa hasa. Pamoja na kukumbushana ya shule,chuo na maishani,siasa hutawala mazungumzo yetu.
Rafiki yangu amenikumbusha moto alioanza nao Ndugu Lowassa aliposhika nafasi ya Waziri Mkuu. Akanikumbusha jinsi Lowassa alivyofanya ziara za kushtukiza,mikutano ya hadhara ya maswali na majibu ya papo kwa papo na hata kuwatimua kazi watumishi.
Rafiki yangu huyu anasema kuwa ayafanyayo Rais Magufuli ni marudio yenye maboresho ya yale mambo ya Lowassa kabla ya kujiuzulu mwaka 2008. Anamuunga mkono Rais kama alivyomuunga mkono Lowassa katika kutikisa watumishi na kuwaamsha kiutendaji.
Nimeambiwa kuwa haya si mapya. Yalishatendwa na Lowassa. Lowassa aliagiza mvua kutoka nje,Rais ameagiza sukari toka hukohuko. Yaleyale lakini yenye maboresho!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Iringa)