Nimeambiwa ninenepe kidogo ili anikubalie. Naombeni mbinu za kuongeza mwili

Msitari wa pambizo

JF-Expert Member
Sep 25, 2014
2,879
4,880
Kaaaaazi kwelikweli, sijui kama waowaji wote walipitia masaibu ninayoyapitia mimi.

Back to the topic. Huyu dada nampenda sana na amenisumbua sana maana mwanzoni hata kuongea na mimi alikuwa hataki. Lakini kidogo kidogo nikaanza kuruka kihunzi kimoja baada ya kingine. Vihunzi vilikuwa vingi sana lakini vyote nimevishinda na sasa kimebaki kimoja tu kwamba yeye hapendi wanaume wembamba so amenipa masharti kwamba niongezeke mwili kidogo ili anikubali niwe mume wake.

Nakuja hapa kwenu kuwaomba mbinu hasa za kiafya za namna ya kuongeza mwili kwa muda mfupi

Nawasilisha

UPDATES
Nahitaji ushauri wa namna ya kunenepa wala sio kumuacha. Maana naona kuna watu wanakuja mara ooh hakupendi, mara ooh hakuna ndoa hapo, mara hakuna mapenzi ya masharti.

Jamani kama ni mapenzi kuniendesha basi huyu binti ameshanimaliza imebaki kuniuwa tu. Nampenda na simuachi kama ni kuniua basi nifeeeee.

1619781851655.png

Kula mishkaki ya nundu kwa mwezi mmoja utaleta mrejesho! Hakikisha unaila na ugali wa nguvu mida ya usiku!

Asubuhi piga supu daily na vyapati vyapati!

Mchana kula chips mayai + Kuku wa kukaangwa!

Fanya hii Diet kwa mwezi tu kisha utaleta mrejesho
 
Mkuu, hata ahangaike nayo haya yote uliyo mshauri na akapata majibu chanya, ndoa haipo.
Na kama huyo jamaa ana mwili kama wa Polepole wa ccm hata alale na hivyo vyakula kitandani hanenepi ng'o.
Awaachie tu waoaji wamuoe huyo kisukunuku
 
Hahahahah sikutaka mkatisha tamaa bana ila mwanamke akianza kukuwekea masharti ya kijinga namna hio huyo ni wa kupiga chini tu! Haina namna
 
Back
Top Bottom