Nimeambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa tunatakiwa kuchangia kila mmoja Tsh. 30,000/-

Mita yangu inameza sana umeme. Huwa natumia unit 120 kwa mwezi. Nina mpangaji mmoja lakini huwa anatoa sh 10000 na mi huwa natumia sh 30000. ila cha kushangaza, mpangaji hulalamika. Yeye ana tv na taa 2, mimi nina tv, friji na pasi, taa4 za ndani na taa4 za nje (hizi za nje naamini naamini zinatusaidia sote)

Anachonishangaza, akitoka kwenda sehem yoyote, hata kama ni siku nzima tv huiacha inafanya kazi. Nadhani humaanisha hela yake ya umeme itumike vizruri kitu ambacho mi sioni kama kina logic na nilishamwambia mrs asiwaulize chochote.

Kwa upande wako, sio sahihi, hiyo fedha ni kubwa mno aisee
Ana haki ya kulalamika huyo. 10,000 kubwa sana kwa matumizi yake..
Yan tv na taa mbili zimalize umeme wa elf kumi kwa mwezi ni ukichaa.
Kwakuwa wewe ni mwenye nyumba mfungie kimita chake uone kama atalalamika..atalipia kutokana na matumizi yake..

Tena utajukuta wewe unalipa paka 35 kwa mwezi ye anajazia kaki.
 
Iko hivi tanesco wanapokuinganishia umeme huwa unakua katka category 2
1.Single phase ambapo utaiziwa unit 1 kwa sh 121.95 hapo ukiwa na matumizi ya kawaida au kwa lugha nyngne wanaita umeme wa nyumbani
2 three phase hapa utauziwa unit moja kwa sh 357.14 au kwa lugha nyngne wanaita umeme wa viwandani ( hapa kama unatumia vtu Kama mashine ya kusaga unga,kukoboa, etc na mitambo yote mikubwa inayotumia umeme mwingi

Inapotokea kwa nyumba yenye wapangaji wengi wenye apliances kama fridge, oven pasi, jagi etc vinavotumia umeme mwingi tanesco wanahamisha matumizi yenu kutoka matumizi Madogo hadi matumizi makubwa ndo matokeo yake ukinunua umeme wa elf 10 unapewa units 28
suluhisho; kama amekuambia kwa siku natumia units 2 inatakiwa ujue kwa siku unatumia shilingi 714.29 ukizidisha kwa siku 30 itakua imefka 21428.70 ko hiyo elf 30 bado haijafika
chamsingi nunua kisoma mita ( sub-meter) kinauzwa kama elf 25 hv ufunge itakusomea units unazotumia uzidishe kwa hiyo hela per unit uone inatakiwa kulipa kiasi gani mzuri wa sub- meter unaweza kuhama nayo so haina hasara
Mkuu unaweza kubadilisha vipi kutoka hiyo phase kubwa kuja single phase.?
 
Ni LUKU,mwenye nyumba kadai yeye sh.10000/-anapewa units 28,sasa huyu mpenzi wake ambaye ni mpangaji mwenzangu ndiyo anadai nitoe 30,000/- eti na yeye atoe kama hiyo ndiyo umeme utatosha mwezi,hapo ndiyo nimeshtuka!!
Changisha alafu ununue wewe na uweke wewe uone kama utaisha huo umeme wa elfu 60 mimi nina AC na taa tisa na simalizi umeme wa elfu 50 unit 140.4 na pasi napiga nnavyotaka na friji linaunguruma halijawai kuzimwa
 
Usikubali KUTAPELIWA.

Nimeambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa tunatakiwa kuchangia kila mmoja sh.30000/- kila mmoja yaani umeme wa sh.60,000/- ndiyo unatosha kumaliza mwezi eti kwa kuwa kila mmoja ana TV screen na kwamba kwa Siku TV moja inatumia units mbili,naomba anayeujua ukweli aijuze tafadhali!
 
Unaibiwa chief.. mimi nilikua nakaa chumba nachemsha maji kila siku kwa jagi , natumia desktop kila siku , napikia kwa rice cooker. Na kwa mwezi elfu 10 ilikia inatosha kabisa.
 
Elfu 30?

Kila kipima unit cha umeme ni elfu 24.

Nunua kile.

Funga.

Rekodi unit unazotumia kwa mwezi.

Angalia unit 1 shilingi ngapi.

Piga hesabu kwa unit ulizotumia mwezi mzima unatakiwa kutoa shilingi ngapi.

Kisha toa hiyo.
Best option! Kwann ataseke? Nunua huko na awe mkali akileta kujifanya ako na hela itakula kwake
 
Changisha alafu ununue wewe na uweke wewe uone kama utaisha huo umeme wa elfu 60 mimi nina AC na taa tisa na simalizi umeme wa elfu 50 unit 140.4 na pasi napiga nnavyotaka na friji linaunguruma halijawai kuzimwa
Asante kwa ushauri,nitaufanyia kazi!
 
Mkuu unaweza kubadilisha vipi kutoka hiyo phase kubwa kuja single phase.?
Kama ilifungwa single phase ila kutokana na matumizi yako ukajikuta umepanda tariff yaan ukaingizwa kwenye matumizi makubwa kuna option 2 yakwanza unatakiwa kutumia units isiyozidi 75 kwa mwez ndani ya miez mitatu yaan ujilimit kabisa hata kama utalala Giza lakn units zako kwa mwezi zisizidi 75 yaan kwa mwez ununue umeme wa sh 9700 tu baada ya miez mitatu system itadetect na utahamishwa tariff
Njia ya pili nenda tanesco ukawaeleze watakusaidia kukubadilishia
 
Friji sina nina jagi moja tu la kuchemshia maji!Nimemwambia tuchangie hata sh.20000/-kila mmoja lakini bado amekataa!!
Mkuu hyo mbona rahisi.....wewe kanunue separate meter yako ni 29000 tu ufungiwe, utakuwa umekata hayo mambo.................... mim naishi mwenyewe, sishndi nyumbani, nina tv, pasi, radio na PC yangu, ninapasi nguo kila siku kwenda kazini, nlikuwa nalipa 10K per month, ila bado nikaona matumizi yangu yapo chini mno, nikafunga meter yangu, nikaweka umeme wa 10k mwezi February mpaka leo nimetumia unit 20.1KW, miez minne so roughly umeme wa 10K natumia kwa 5 months sababu umeme wa 10K ni Unit 28.1KW.
 
Asante kwa ushauri!
 
Kama ilifungwa single phase ila kutokana na matumizi yako ukajikuta umepanda tariff yaan ukaingizwa kwenye matumizi makubwa kuna option 2 yakwanza unatakiwa kutumia units isiyozidi 75 kwa mwez ndani ya miez mitatu yaan ujilimit kabisa hata kama utalala Giza lakn units zako kwa mwezi zisizidi 75 yaan kwa mwez ununue umeme wa sh 9700 tu baada ya miez mitatu system itadetect na utahamishwa tariff
Njia ya pili nenda tanesco ukawaeleze watakusaidia kukubadilishia
Asante,ngoja nijaribu hiyo ya miezi mitatu.

Maana baada ya kuunganishwa umeme tu sikuanza kwenye hiyo single phase
 
Nimeambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa tunatakiwa kuchangia kila mmoja sh.30000/- kila mmoja yaani umeme wa sh.60,000/- ndiyo unatosha kumaliza mwezi eti kwa kuwa kila mmoja ana TV screen na kwamba kwa Siku TV moja inatumia units mbili,naomba anayeujua ukweli aijuze tafadhali!
Pambana uwe na kwako mkuu. Kupangisha ndio mwanzo wa kunyanyasika hivyo
 
Mita yangu inameza sana umeme. Huwa natumia unit 120 kwa mwezi. Nina mpangaji mmoja lakini huwa anatoa sh 10000 na mi huwa natumia sh 30000. ila cha kushangaza, mpangaji hulalamika. Yeye ana tv na taa 2, mimi nina tv, friji na pasi, taa4 za ndani na taa4 za nje (hizi za nje naamini naamini zinatusaidia sote)

Anachonishangaza, akitoka kwenda sehem yoyote, hata kama ni siku nzima tv huiacha inafanya kazi. Nadhani humaanisha hela yake ya umeme itumike vizruri kitu ambacho mi sioni kama kina logic na nilishamwambia mrs asiwaulize chochote.

Kwa upande wako, sio sahihi, hiyo fedha ni kubwa mno aisee
Huyo mpangaji wako mfungie SUB METER utamaliza tatizo, baada ya hapo ndio utajua tatizo lipo wapi? Inawezekana hiyo Tv kuiacha ON na deki kaicha ON labda na vyenyew vinachangia umeme,
Sijawai kukutana na scenario ya luku kula umeme, hiyo inaweza kuwa wiring umeme unapotea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Changisha alafu ununue wewe na uweke wewe uone kama utaisha huo umeme wa elfu 60 mimi nina AC na taa tisa na simalizi umeme wa elfu 50 unit 140.4 na pasi napiga nnavyotaka na friji linaunguruma halijawai kuzimwa
Aisee siamini.
 
Nimeambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa tunatakiwa kuchangia kila mmoja sh.30000/- kila mmoja yaani umeme wa sh.60,000/- ndiyo unatosha kumaliza mwezi eti kwa kuwa kila mmoja ana TV screen na kwamba kwa Siku TV moja inatumia units mbili,naomba anayeujua ukweli aijuze tafadhali!
Hama nyumba faster
 
Back
Top Bottom