Nimeambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa tunatakiwa kuchangia kila mmoja Tsh. 30,000/-

Pole Sana mkuu. Hapo utapigwa Hadi uchakae. Fanya namna utafte separate meter ufunge.
Mimi Nina jagi la umeme nalitumia kila siku asubuhi na sometimes jioni, Nina friji, flat screen (anayokutishia kuwa unakula umeme), rice cooker na pressure cooker za umeme Ila kwa mwezi haizidi 15,000. Alafu flat screens nyingi zimetengenezwa katika mfumo ambao inakuwa eco friendly na hivyo kuwa na very minimal Power consumption.

Jirani yako sio mtu mzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee kwa15k/month kwa hizo appliances ulizonazo unatudanganya Kiongozi. Angalia hapa.. 15k=14units. Ukichukua 14units/30days=0.46units/day. Matumizi ambayo hayawezekani hata ufanyaje.
 
Mkuu huyo mwenzio atakuwa anatumia friji full time, hapa kwangu natumia umeme wa elf 50 ila nilichogundua friji langu ndo linakula zaidi, kama unit 4 kwa siku, nimepanga nimtafute fundi aje acheki namna linavyofanya kazi, maana kwa mahesabu niliyofanya, nikiamua kulizima hilo friji mwezi mzima nitatumia umeme kama wa elfu 20 tu kwa mwezi....
 
Ndugu yangu Analyse, hiyo separator meter(SUB METER) km umepanga chumba kimoja unamuita fundi anangalia waya zinazoingiza umeme kwenye chumba chako ndizo hizo anaziconnet na hiyo sub meter, km umepanga upande fundu atafanya hivyo kwa waya zinazo ingiza umeme kwako, kazi kubwa ya sub meter ni kusoma matumizi yako tu kwa unit, unweza kujua kwa siku unatumia unit ngapi au kwa mwezi, unanua umeme labda wa elfu 10 unit 28 ww unaziweka km kawaida kwenye luku, kazi yako ni kuangalia hicho kisub meter chako mpk kisome hizo unit 28 hapo ndipo utajua umeme ulionunua umeisha, km kuna sehem haujaelewa nifamishe nikueleweshe
(sub meter)View attachment 1459573

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nashkuru sana kwa maelezo yako. Yapo very clear na nimeelewa kwa kadri nilivyohitaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee kwa15k/month kwa hizo appliances ulizonazo unatudanganya Kiongozi. Angalia hapa.. 15k=14units. Ukichukua 14units/30days=0.46units/day. Matumizi ambayo hayawezekani hata ufanyaje.
Mkuu 15k unapata 14units? Au ni typing error? Huo utakuwa mkoa gani wanatoa hizo 14units, kwa hapa Dar umeme wa 10k ni 28unit na umeme 5k ni 14unit, jumla umeme wa 15k unapata 42unit.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa tunatakiwa kuchangia kila mmoja sh.30000/- kila mmoja yaani umeme wa sh.60,000/- ndiyo unatosha kumaliza mwezi eti kwa kuwa kila mmoja ana TV screen na kwamba kwa Siku TV moja inatumia units mbili,naomba anayeujua ukweli aijuze tafadhali!
Kanunue separate mita itakusomea units unazotumia mwezi mzima zidisha na bei ya tanesco kazi iishie hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mwenzangu anayo friji ambayo huwa anahifadhia fresh food maana ni mpenzi wa chakula hicho!
 
Yaani watu 2 ndio mtumie umeme wa 60? Mna kiwanda au

Huyo atakuwa labda mchepuko wa mwenye nyumba anataka apate kitonga toka kwako
Nilishawahi kuishi na mpangaji wa namna hiyo, mie namtumia hela ya umeme yeye ya kwake hanunui, baada ya wiki mbili anamwagiza shem kuwa umeme umekata, niliporejea na kuchunguza kumbe hata ile niliyokuwa nikitoa alikuwa hanunui yote, baadaye mwenye nyumba alimchoka na kumtimua kwenye nyumba yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa tunatakiwa kuchangia kila mmoja sh.30000/- kila mmoja yaani umeme wa sh.60,000/- ndiyo unatosha kumaliza mwezi eti kwa kuwa kila mmoja ana TV screen na kwamba kwa Siku TV moja inatumia units mbili,naomba anayeujua ukweli aijuze tafadhali!
Sifa ya nyumba ya kupanga, kila mpangaji na mita yake. Labda zile za uswazi za kizamani sana.
Siku hizi kuweka mita nyingine sio issue kubwa. Service line TShs 321,000. Watapiga simu wenyewe kuja kuweka mita. Hakuna kufuatilia kwenda kutoa rushwa.
 
nyumba ya kuchangia umeme huwa ina matatizo sn. tafuta nyumba luku ya peke yako ili uishi kwa amani. hapo utaibiwa, fridge, jiko, birika vyote vinakula umeme.
 
Nimeambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa tunatakiwa kuchangia kila mmoja sh.30000/- kila mmoja yaani umeme wa sh.60,000/- ndiyo unatosha kumaliza mwezi eti kwa kuwa kila mmoja ana TV screen na kwamba kwa Siku TV moja inatumia units mbili,naomba anayeujua ukweli aijuze tafadhali!
Nitumieni namba zenu za simu niwawekee hela kwenye akaunti zenu. Elfu 60 hela kidogo sana hamhitaji kukaa mnalia lia hadi mnafikia kutoa matangazo kwenye mitandao ya jamii
 
Hilo jagi la umeme pia ni kwikwi mzee..japo umeme wa elfu 60 kwa watu wawili bado ni kisanga aisee
Jagi la umeme halili umeme,kwani interval ya kutumia Ni dakika tano nyingi,hata Kama Ni watt 500,bado sio tatizo,
Tv kula unit 2 labda I we inawaka masaa 24 bill kuzimwa
 
Nimeambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa tunatakiwa kuchangia kila mmoja sh.30000/- kila mmoja yaani umeme wa sh.60,000/- ndiyo unatosha kumaliza mwezi eti kwa kuwa kila mmoja ana TV screen na kwamba kwa Siku TV moja inatumia units mbili,naomba anayeujua ukweli aijuze tafadhali!
Mita yangu inameza sana umeme. Huwa natumia unit 120 kwa mwezi. Nina mpangaji mmoja lakini huwa anatoa sh 10000 na mi huwa natumia sh 30000. ila cha kushangaza, mpangaji hulalamika. Yeye ana tv na taa 2, mimi nina tv, friji na pasi, taa4 za ndani na taa4 za nje (hizi za nje naamini naamini zinatusaidia sote)

Anachonishangaza, akitoka kwenda sehem yoyote, hata kama ni siku nzima tv huiacha inafanya kazi. Nadhani humaanisha hela yake ya umeme itumike vizruri kitu ambacho mi sioni kama kina logic na nilishamwambia mrs asiwaulize chochote.

Kwa upande wako, sio sahihi, hiyo fedha ni kubwa mno aisee
 
Jagi la umeme halili umeme,kwani interval ya kutumia Ni dakika tano nyingi,hata Kama Ni watt 500,bado sio tatizo,
Tv kula unit 2 labda I we inawaka masaa 24 bill kuzimwa
Hata kama itakuwa inawaka saa 24 bila kuzimwa inategemea na power yake (W)

ᵃʳᵉᵉᵐ
 
Back
Top Bottom