Nimeambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa tunatakiwa kuchangia kila mmoja Tsh. 30,000/-

Hilo tumeshindwa kuelewana!Tatizo hakuna anayeiingia kwenye chumba cha mwenzio sasa uhakika wa kufahamu kama hatumii jiko la umeme na hiyo friji ni ngumu!Kwangu nimemuingiza ndani na kumuonyesha jagi ninalotumia kuchemshia maji ajabu anadai TV yangu ndiyo inamaliza umeme!Kwangu ni kitu kipya!
Ni mpenzi wa mwenyenyumba? Ni me au ke?Hapa huyo mtu anataka slope kwa kukutoa damu.Unatakiwa utumie unit 28 tu sh.10,000 tu.Mkazie ikibidi mwambie msinunue umeme uone atakavyopagawa.Ukiwa mlaini utakuwa unanunua umeme peke yako.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa tunatakiwa kuchangia kila mmoja sh.30000/- kila mmoja yaani umeme wa sh.60,000/- ndiyo unatosha kumaliza mwezi eti kwa kuwa kila mmoja ana TV screen na kwamba kwa Siku TV moja inatumia units mbili,naomba anayeujua ukweli aijuze tafadhali!!!
60,000Tshs/10,000Tshs=6x28 units=168 units.Matumizi ya watu wawili haiwezekani ,watu wasingetumia umeme maana itakuwa anasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa tunatakiwa kuchangia kila mmoja sh.30000/- kwa Siku TV moja inatumia units mbili naomba anayeujua ukweli anijuze tafadhali!!!
Kwa mahesabu ya kiumeme: kwanza hiyo Tv ina watts ngapi? Pili unnaitumia kwa masaa mangapi kwa siku?
Kipindi naishi Temeke niliwahi kuambiwa na mama mwenye nyumba kuwa tv yangu flat inakula umeme, nilicheka sana kwa vile naelewa, lengo ilikuwa ni kutaka kunipandishia bei ya umeme kutoka 10,000 kwenda ishirini nashukuru mitego hiyo nilii epuka pale nilipohama.



ᵃʳᵉᵉᵐ
 
Nahisi kama unakaa chumba nilicho hama mimi, ni Ubungo??

Nimekaa na mpangaji mmoja hapo kibangu tunashare umeme wawili. Yeye ni shosti wa maza house. Day one wakaniambia kila mtu analipa 25. so kwa mwezi 50. Hafu mita ipo sebuleni kwake uyo mpangaji so siwezi confirm.

Kila tar 25 alikua anatuma mtoto kuchukua 25 kwa madai umeme umeisha.

Mimi nina TV, pasi, PS3, jagi, PC, chaja ya LG G6 na feni tu ndio vya umeme. Katika siku nzima ghetto nakuja kulala tu mara chache kushinda mchana.

Kuna kipindi nilisafiri nikaenda Mwanza wiki 4. Kabla sijasafiri ndio nilikua nimetoka kulipa 25. basi kurudi akanionea aibu akanipa kama siku 6 hivi kisha nikasikia hoodiii, mama kasema umeme umeisha, fala mimi nikatoa 25 uyooo.

Nilivohama nikagundua yule maza alikua hanunui wa 50 wala wa 25 ila alikua ananunua wa 10 au 15.

Maana sahivi luku yangu nina friji taa tv ving'amuzi machine ya kufulia oven etc etc etc lakini umeme wa 20 unakata miezi 2 na kidogo na home kuna madogo wamefunga chuo kwahiyo TV sidhani kama uwa inazimwa.

Cha kufanya mtafute fundi umeme. Kama umeamua kukaa iyo nyumba zaidi ya mwaka au miwili, akuwekee kadude flani kanaonesha units ulizotumia wewe. kwahiyo alietumia zaidi atalipa zaidi. kanauzwa 50 tu wanazitumia san akwenye fremu za biashara
Wazo zuri sana ,Nakusahihisha kile kisoma umeme kinauzwa 25 mpaka 30 labda hiyo 50 na gharama za fundi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maswala ya luku ndo yanifanya hadi nikaamua kupanga chumba cha giza, baadaye nikahamia kwangu kukiwa bado pagale .

Tulikuwa tunachanga 25000 kwa mwezi na bado umeme ulikuwa hautoboi, hapo mchana unazimwa , siku ukiisha na bahati mbaya ikawa una kazi inayohitaji umeme usilogwe kununua wa buku mbili , yan utashambuliwa nusus saaa nyingi umekata tena, ilikuwa ni mwendo wa kukomoana kwa kweli,kitu ninachoshangaa hadi leo ni vifaa gani vya umeme wapangaji wenzangu walikua wanatumia , manake ilikuwa ni zaidi ya mashine za kusaga kwa kula units

Sent
Ndg sometimes ni mfumo mbovu wa umeme kama wiring ni chafu lazima mlie....pia vifaa used hasa mafridge yanakula sana umeme ambayo huku kwetu uswazi ndiyo yanatamba;nawashauri ndg zangu upande wa vifaa tusipende kunumua used vinatughalimu sana hasa mafridge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini msinunue kwanza wa hela kidogo mkaangalia unakaa siku ngapi hata wa elf 10 kwa maana ya elf 5 kila mmoja kisha hapo ndo mtajua kwa mwezi mtatumia unit ngapi ambazo ni sawa na sh.ngapi.

Huyo aliekwambia kwamba elf 10 anapata unit 28 ni sawa hajakudanganya kwa sababu hiyo ni tarrif kubwa,ambapo tarrif ndogo unanunua umeme wa elf 9 na kupewa unit 73kwh but matumizi yakisha zidi unit 73kwh kwa mwezi lazima wakupeleke kwenye tarrif kubwa automatically.

Hivyo basi kwenye kuchangia kila mmoja elf 30 siungi mkono kabla ya kununua umeme mdogo kwanza ili mjue matumizi kwa mwezi na yeyote atakae nunua basi aoneshe message ya mchanganuo na kapokea unit ngapi ili kila mmoja alidhike
 
Jagi silitumii Mara kwa Mara huyo mpangaji mwenzangu ndiyo ana friji na jiko la umeme ajabu anadai kuwa havitumii!!
Logic no hii mkuu....Mkinunu umeme was 60000 ndo anaanza kutumia mitambo take kwa hiyo utatosha wala hautabaki....Fanya vyovyote usijaribu kuona kama utatosha au utabaki hauto baki.
 
Logic no hii mkuu....Mkinunu umeme was 60000 ndo anaanza kutumia mitambo take kwa hiyo utatosha wala hautabaki....Fanya vyovyote usijaribu kuona kama utatosha au utabaki hauto baki.
Hapo ni kweli!
 
Nashukuru kwa ushauri!Tatizo toka nifike niliambiwa maji tutachangia sh.5000/- na umeme sh.10000/- kila mmoja!Sasa mwezi huu ambao ni wa pili kwangu kanibadilikia na kudai Mimi kwa umeme tu nitoe sh.30000/-eti TV inakula umeme sana!
 
Kama bado unapapeda kuendelea kuishi hapo, ongea na mwenye nyumba ili muite fundi akufungie SUB METER [ni sh 25k-30k], iki kitakusaidia kusoma unit ulizotumia kwa mwezi, unanunua zako umeme wa elfu 10 unit 28 unajaza kwenye luku uku unakuwa unaangalia SUB METER mpk isome hizo unit 28 ulizoweka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchawi hapo ni sub meter hakuna kingine, mm nilikutana na shida km yako kwa mwezi tulikuwa tunanunua umeme wa elfu 50 mpk elf 60, na mm sio mtu wa kushinda home, nina jagi hilo km lako ,fridge, microwave, tv, na fan, kwa sasa baada ya kufunga sub meter ni lipa elfu10 kila mwezi. Mpangaji mwenzangu yy ananunua wa elfu 20 mpk 30 coz ana fridge yale makubwa ya mtumba.
20200131_124651.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hiyo meter separator inafanyaje kazi mkuu? Yani naiconnect wapi na vipi ili iweze kunisomea units ninazotumia kwa mwezi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu yangu Analyse, hiyo separator meter(SUB METER) km umepanga chumba kimoja unamuita fundi anangalia waya zinazoingiza umeme kwenye chumba chako ndizo hizo anaziconnet na hiyo sub meter, km umepanga upande fundu atafanya hivyo kwa waya zinazo ingiza umeme kwako, kazi kubwa ya sub meter ni kusoma matumizi yako tu kwa unit, unweza kujua kwa siku unatumia unit ngapi au kwa mwezi, unanua umeme labda wa elfu 10 unit 28 ww unaziweka km kawaida kwenye luku, kazi yako ni kuangalia hicho kisub meter chako mpk kisome hizo unit 28 hapo ndipo utajua umeme ulionunua umeisha, km kuna sehem haujaelewa nifamishe nikueleweshe
(sub meter)
20200412_160608.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom