Nimeambiwa kuwa baba nilienae siyo my biological father nifanyaje?

saraka

Member
Jul 13, 2013
30
3
Ndugu wadau wenzangu wa jukwaa kwa takribani miaka 22 niliyo nayo nimekuwa najua kuwa ni baba yangu lakini hivi karibuni mama yangu alinitobolea kwamba huyo siyo my biological father ni kama mlezi wangu tu. kwa kweli sielewi hata nianzie wapi nahisi kuvurugwa. Naombeni ushauri wenu wana jamvi
 
Tuliza akili kwanza ndio utajua nini cha kufanya.Chochote ufanyacho uendelee kumpenda na kumueshimu baba mlezi kama baba yako.Pili ulizia kisa cha mama yako kutokukufahamisha juu ya baba mzazi hapo ndio utajua kama utataka kumfahamu au la
 
Pole.
Mama anasema your biological father yuko wapi?
Tia nyama kidogo story yako inenepe ili wadau waielewe vizuri bila kuwa na maswali mengi waweze kukushauri
 
Anzia kwa mama yako anayemjua baba yako mzazi. huyo mlezi endelea kumheshimu kama mwanzo. mbembeleze mama atoe maelezo ya kueleweka sababu za kuachana na your biological father, kukuficha ukweli huu, n.k tuliza akili kijana.
 
https://www.jamiiforums.com/mahusia...he-biological-fathers-nendaeni-mkapime-2.html

Inasikitisha sana lakini uzinzi Tanzania ndio sifa kuu.

Heshima, utu na adabu zinazidi kushuka kila kukicha, tutegemee nini ikiwa 60% ya mababa wanabambikiwa watoto.

Usimwambie huyo baba aliokulea kitu chochote endelea kumheshimu na kuwa nae kama hujasikia kitu. Baba ni yule akuleae na wala usimtafute huyo unaetakiwa awe ndio baba'ko. Kwanini kosa la mama'ko ulilipe wewe?
 
Ndugu wadau wenzangu wa
jukwaa kwa takribani miaka 22 niliyo nayo nimekuwa najua kuwa ni baba
yangu lakini hivi karibuni mama yangu alinitobolea kwamba huyo siyo my
biological father ni kama mlezi wangu tu. kwa kweli sielewi hata
nianzie wapi nahisi kuvurugwa. Naombeni ushauri wenu wana jamvi

Fanya DNA Test, then bring back here the results.
 
kama alishakulea na kukutunza kama mwanae una haji gani tena ya kummtafuta baba mwingine?
mthamini huyo ulie nae kama amaekupa mapenzi ya kibaba.
waza maisha yako kijana kama wasoma pigabuku kwenda mbele
huyo unaetaka kumtafuta hatakupa future kwa sasa.
 
https://www.jamiiforums.com/mahusia...he-biological-fathers-nendaeni-mkapime-2.htmlInasikitisha sana lakini uzinzi Tanzania ndio sifa kuu. Heshima, utu na adabu zinazidi kushuka kila kukicha, tutegemee nini ikiwa 60% ya mababa wanabambikiwa watoto.Usimwambie huyo baba aliokulea kitu chochote endelea kumheshimu na kuwa nae kama hujasikia kitu. Baba ni yule akuleae na wala usimtafute huyo unaetakiwa awe ndio baba'ko. Kwanini kosa la mama'ko ulilipe wewe?
Kwa kweli naanza kukubaliana na mila ya baadhi ya makabila ambayo yanachukua ukoo kutoka kwa mama.Makabila mengi ya Ghana yanatumia hiyo system kuwa mama anapokuwa mjamzito kila mtu anamuona na hakuna haya ya vipimo kwa sababu mtoto atakaye mzaa ni wa damu yake, hivyo mtoto anachukua ubini kutokea kwa mama na sio upande wa Baba kwani hakuna uhakika Baba halisi ni nani
 
pole kaka!! wanawake wana mengi sana mioyoni mwao!

yani kaficha siri kwa miaka 22 ? duh!

btw, mama yako sasa awe responsible kukuambia baba yako ni nani!

ila kama hakuwa mtulivu enzi hizo, sidhani kama atakuambia baba yako ni yupi hasa!
 
kama alishakulea na kukutunza kama mwanae una haji gani tena ya kummtafuta baba mwingine?
mthamini huyo ulie nae kama amaekupa mapenzi ya kibaba.
waza maisha yako kijana kama wasoma pigabuku kwenda mbele
huyo unaetaka kumtafuta hatakupa future kwa sasa.

Hapo kwa red; ndiyo maana ameleta uzi huu hapa!
 
Kwa kweli naanza kukubaliana na mila ya baadhi ya makabila ambayo yanachukua ukoo kutoka kwa mama.Makabila mengi ya Ghana yanatumia hiyo system kuwa mama anapokuwa mjamzito kila mtu anamuona na hakuna haya ya vipimo kwa sababu mtoto atakaye mzaa ni wa damu yake, hivyo mtoto anachukua ubini kutokea kwa mama na sio upande wa Baba kwani hakuna uhakika Baba halisi ni nani

Huko ni kuendeleza uzinzi na kutojali haki ya mtoto.

Uzinzi ndio unapelekea haya majanga. Hata Taifa linakuwa halina akili, si unaiona Tanzania ilivyo?
 
Muulize mama yako kama ni wewe tu au na Kaka zako na dada zako pia wana baba zao. Kama mko wengi fanyeni maamuzi kwa pamoja.
 
Ushukuru mungu hata alivyokuambia. Mwite pembeni mwombe akuonyeshe baba yako. Baada ya hapo ongea na mzee wa heshima hapo jirani ili akupe taratibu za kufuata.
 
Kama amekulea vizuri tangu ulipokuwa na akili ya kumuita Baba hadi sasa una miaka 22 basi wala hakuna sababu ya kuvurugwa. Endelea kumuheshimu kama ulivyokuwa unamuheshimu kabla ya mama yako kukwambia aliyokwambia. Huyo aliyetia mimba hana sifa ya kuitwa Baba, yeye alikuwa ni sperm donor tu labda ndio maana akaingia mitini kukimbia majukumu au labda mama hakumtaarifu kwamba ana mimba yake.

Ndugu wadau wenzangu wa jukwaa kwa takribani miaka 22 niliyo nayo nimekuwa najua kuwa ni baba yangu lakini hivi karibuni mama yangu alinitobolea kwamba huyo siyo my biological father ni kama mlezi wangu tu. kwa kweli sielewi hata nianzie wapi nahisi kuvurugwa. Naombeni ushauri wenu wana jamvi
 
…kwa takribani miaka 22 niliyo nayo nimekuwa najua kuwa ni baba yangu lakini hivi karibuni mama yangu alinitobolea kwamba huyo siyo my biological

Kumbuka Baba ni baba.. hata kama angekuwa ng'ombe.. Jiulize kama angekuwa sio baba yako ungefika hapo ulipo na kuwa na jeuri ya kuuliza eti where is my biological father?

kwa kweli sielewi hata nianzie wapi nahisi kuvurugwa. ..

Ukiona unavurugwa ..ujue akili yako haijatulia…au imejaa makamasi..

Ushauri: Potezea mawazo ya biological father..hakuna relationship katika maisha kati yako na biological father.. baba ni baba.. Hata mama yangu kesho akija na kuniambia huyu sio baba yangu tutagombana… Huyu ninayemjua na aliyenisaidia ndio baba yangu…wengine wote ni wahuni hata kama walidonate manii zao!
 
Ndugu wadau wenzangu wa jukwaa kwa takribani miaka 22 niliyo nayo nimekuwa najua kuwa ni baba yangu lakini hivi karibuni mama yangu alinitobolea kwamba huyo siyo my biological father ni kama mlezi wangu tu. kwa kweli sielewi hata nianzie wapi nahisi kuvurugwa. Naombeni ushauri wenu wana jamvi
mwambie akuoneshe original maana umechoka huo mchina sawa baba..
 
Kwa kweli naanza kukubaliana na mila ya baadhi ya makabila ambayo yanachukua ukoo kutoka kwa mama.Makabila mengi ya Ghana yanatumia hiyo system kuwa mama anapokuwa mjamzito kila mtu anamuona na hakuna haya ya vipimo kwa sababu mtoto atakaye mzaa ni wa damu yake, hivyo mtoto anachukua ubini kutokea kwa mama na sio upande wa Baba kwani hakuna uhakika Baba halisi ni nani
kwenye ward za wazazi wahudumu hawapo makini sana hawakawii kuwa-cross watoto wachanga kwa mama tofauti.
 
Forget it period!!!!!!!!! What do you mean he is not your father! DONT HURT THE GOOD MAN WHO HAS ALWAYS LOOKED AFTER YOU AND MADE SURE YOU NEVER WENT HUNGRY FOR SOME ONE WHO DOESNT GIVE A ---- IF YOU EXIST!!!!!!!!!!!!!

HE IS YOUR FATHER KID! MARK MY WORDS! THE OTHER IS JUT SOME ONE WHO HAPPENED TO DONATE A SPERM THAT TURNED OUT TO BE YOU!

BEING A FATHER IS MORE THAN DONATING A SPERM!!!!!!!!!!!!! be very very very grateful!!!!!!!!!!!!!

Dont even dare dream your father will be happy to see you! YOU WERE A MISTAKE KID PUT THIS IN YOUR BRAIN AND MAKE IT STICK THERE FOREVER! 22 YEARS!!!!!!!!!!!!! Come on the guy has even believed the gods were kind to be blind of his MISTAKE! Let it go kid!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom