Nimeambiwa eneo linamilikiwa na majini na nimeshalipia pesa

Veyron

JF-Expert Member
Feb 6, 2012
572
378
Wakuu heshima kwenu.
Katika harakati za kimaisha nilipata kaeneo maeneo ya CHANIKA sehemu inaitwa ZINGIZIWA .

Nilipelekwa mara ya kwanza na nikaoneshwa kuwa eeneo liko safi kabisa na ni eneo kubwa linaonesha vyanzo vya maji vipo karibu. Pia linafikika kirahisi na nikaenda kwenye mamlaka ya kiserikari nikaoneshwa Ramani kuwa haliko kwenye mipango ya serikari.

Na mtu aliyenitaftia hapo alinihakikishia hilo ila ilinibidi nichunguze mimi kama mimi.

Baada ya kuona eneo liko safi nikaanza mchakato wa malipo kwa kufuata sheria zote.

Sasa juzi nilipo kwenda kulitembelea nikamwona mtu mwenye asili ya pwani (mzaramo, mmakonde) akinifuata na kuniomba aongee na mimi kidogo. Basi bila hiana nikamruhusu.

Alinipa historia ndefu juu ya hilo eneo nikisema niandike ntawachosha. Ila kwa ufupi tu alisema hilo ni eneo ambalo lina wenyewe ati sio langu pamoja na kwamba nalimiliki watakuja kunitfuta siku moja.
Na alidai kuna watu wanakuja maeneo ya jirani kila mwaka kucheza maeneo hayo.
Na kila mwaka hapo tunaokota maiti moja mwisho wa mwaka huwa haijulikani kwanini inakuwa eneo lile na hata wakiitoa hiyo maiti huwa inarudi hapo mpaka baada ya siku saba inapotea yenyewe .Na aliniambia kuwa kama mi ni mzito basi nikae ama la niondoke tu.

Sasa inaonekana pana nguvu za giza pale mahali
.ipi njia bora ya kuepuka hilo tatizo...?


Nafikiria au yule jamaa ananidanganya ni uoga wake tu mbona kwa pembeni kuna watu wanaishi vizuri tu.?

Kwasababu eneo ni zuri sana hasa kwa watoto wangu miaka ijayo.
Au na mimi niliuze kwa mtu mwingine...

Yani nafikiria mengi hadi nakosa usingizi na pesa nimeshatoa kubwa tu.
Kuna mliokutana na shida hii mlifanyaje?
 
Hao majini mwambie baba yao sheh Sharif majini awafuate ila andaa kafara maana sheh siyo MTU wa kisport sport
Dr Luis shika atakupa msaada zaidi mm nimeishia hapo.
 
Hahahaha nimecheka sana.
Hivi we jamaa unaweza weka picha yako hapa tukuone.
Maana pengine unafanana sura na Dr Shika.
Yani hela utoe wewe alafu wakudanganye wapumbavu hao.
Weka mjengo hapo acha utoto.
Kama vipi jenga alafu ukimaliza tu nicheki unipangishe mwaka mzima uone nitakavyonenepa humo ndani.
Acha kuwa na mawazo ya huyo mpumbavu aliyekupa hadithi ya kitoto.
 
Kiwanja ushanunua kaa utulie.kama unaratiba ya kuanza kujenga endelea.
Kuhusu majini si umeambiwa yatakuja subiri yaje.
Au ukijenga Nyumba ukakuta haipo ndo utajua kuwa majini yapo kweli.
Ukisha fahamu leta mada hapa wamo wataalamu wengi humu ndani utapata majibu ya nini kifanyike.
 
Back
Top Bottom