Nimeambiwa eneo linamilikiwa na majini na nimeshalipia pesa

Kiwanja ushanunua kaa utulie.kama unaratiba ya kuanza kujenga endelea.
Kuhusu majini si umeambiwa yatakuja subiri yaje.
Au ukijenga Nyumba ukakuta haipo ndo utajua kuwa majini yapo kweli.
Ukisha fahamu leta mada hapa wamo wataalamu wengi humu ndani utapata majibu ya nini kifanyike.
Haha jamaa umenichekesha
 
Hakuna majini ndugu wazaramo wanaishi kwa michezo hio

Mimi miaka ya nyuma nilinunua eneo siku naenda ku clear nikakuta ma tunguli ... nikachoma moto jirani mmoja akanifata akanambia hichi kiwanja cha moto wewe kwa usalama wako ondoka kabla mabaya hayaja kukuta.

Leo ni mwaka wa 15 hakuna kitu kimenipata nilikuja gundua ni njia ya kupiga hela hata zile tunguli aliye ziweka ni mwenye kiwanja RiP alifariki mimi bado na peta hadi leo
 
Asiyesikia la mkuu...wengine humu hayo mambo hawayajui...chanika uko waganga wamejaa kibao...uliza wengine wawili watatu wakikuambia hvyo liache
 
Wakuu heshima kwenu.
Katika harakati za kimaisha nilipata kaeneo maeneo ya CHANIKA sehemu inaitwa ZINGIZIWA .

Nilipelekwa mara ya kwanza na nikaoneshwa kuwa eeneo liko safi kabisa na ni eneo kubwa linaonesha vyanzo vya maji vipo karibu. Pia linafikika kirahisi na nikaenda kwenye mamlaka ya kiserikari nikaoneshwa Ramani kuwa haliko kwenye mipango ya serikari.

Na mtu aliyenitaftia hapo alinihakikishia hilo ila ilinibidi nichunguze mimi kama mimi.

Baada ya kuona eneo liko safi nikaanza mchakato wa malipo kwa kufuata sheria zote.

Sasa juzi nilipo kwenda kulitembelea nikamwona mtu mwenye asili ya pwani (mzaramo, mmakonde) akinifuata na kuniomba aongee na mimi kidogo. Basi bila hiana nikamruhusu.

Alinipa historia ndefu juu ya hilo eneo nikisema niandike ntawachosha. Ila kwa ufupi tu alisema hilo ni eneo ambalo lina wenyewe ati sio langu pamoja na kwamba nalimiliki watakuja kunitfuta siku moja.
Na alidai kuna watu wanakuja maeneo ya jirani kila mwaka kucheza maeneo hayo.
Na kila mwaka hapo tunaokota maiti moja mwisho wa mwaka huwa haijulikani kwanini inakuwa eneo lile na hata wakiitoa hiyo maiti huwa inarudi hapo mpaka baada ya siku saba inapotea yenyewe .Na aliniambia kuwa kama mi ni mzito basi nikae ama la niondoke tu.

Sasa inaonekana pana nguvu za giza pale mahali
.ipi njia bora ya kuepuka hilo tatizo...?

Nafikiria au yule jamaa ananidanganya ni uoga wake tu mbona kwa pembeni kuna watu wanaishi vizuri tu.?

Kwasababu eneo ni zuri sana hasa kwa watoto wangu miaka ijayo.
Au na mimi niliuze kwa mtu mwingine...

Yani nafikiria mengi hadi nakosa usingizi na pesa nimeshatoa kubwa tu.
Kuna mliokutana na shida hii mlifanyaje?
Mkuu wangu, fanya hivii

“Mzaramo” si anakuambia kwamba jilo emeo ni la watu na kwamba kila mwisho mwa mwaka wanaokota maiti inayoonekana kwa siku 7!!

Hii ni perfect timing kabisa tunaelekea mwisho mwa mwaka, kama ni kweli hiyo kitu inatokea basi utaiona tuu kwa macho yako na kama ni fix hutoona,

Kama hutofanikiwa kuprove basi zitakua ni stori za vijiwe vya kahawa
 
Aliwazalo mpumbavu ndilo humtokea!
Ebu achana na hizo imani za ajabu ajabu,kaendeleze kiwanja chako.
 
Imani yako ndiyo itakayokuokoa. Sie tuna Mungu wao wana mungu wa baali. Songa mbele kakutia hofu ili uanze ushirikiana.

Nyunyuza DAMU YA YESU KONA ZOTE NNE ZA SHAMBA. Tena futa ujinga wa hyo kigagula akilini mwako.
 
Watanzania wengi bado wana akili ndogo sana na imani za kipuuzi...huu ndio ujinga uliofungulia thraed naamini nyie ndio wale mnaoamini nyota na Pete za bahati badala ya kufanya kazi...Damu ya Yesu Ikukomboe..ita wachungaji na wazee wa Kanisa wapige neno na maombi apo tena huyo aliyekuambia umjulishe kua umeshapatakasa kwa Damu Ya Yesu
 
Aliwazalo mpumbavu ndilo humtokea!
Ebu achana na hizo imani za ajabu ajabu,kaendeleze kiwanja chako.
Yaani ukiwaza kitu lazima kikutokee duu...
Sawa lakini haya mambo sio yakufikirika huwa yapo.
 
Hawa Ni watu gani. Ndio wanasali kanisa gani Tanzania? Nielekezwe inaelekea ni watu hatari sana
Kumbe haupo serious? Wewe hujui walokole wanapatikana wap? Anyway nilikua nakupa tu ushauri unaeza kuuchukua au kuacha
 
Wakuu heshima kwenu.
Katika harakati za kimaisha nilipata kaeneo maeneo ya CHANIKA sehemu inaitwa ZINGIZIWA .

Nilipelekwa mara ya kwanza na nikaoneshwa kuwa eeneo liko safi kabisa na ni eneo kubwa linaonesha vyanzo vya maji vipo karibu. Pia linafikika kirahisi na nikaenda kwenye mamlaka ya kiserikari nikaoneshwa Ramani kuwa haliko kwenye mipango ya serikari.

Na mtu aliyenitaftia hapo alinihakikishia hilo ila ilinibidi nichunguze mimi kama mimi.

Baada ya kuona eneo liko safi nikaanza mchakato wa malipo kwa kufuata sheria zote.

Sasa juzi nilipo kwenda kulitembelea nikamwona mtu mwenye asili ya pwani (mzaramo, mmakonde) akinifuata na kuniomba aongee na mimi kidogo. Basi bila hiana nikamruhusu.

Alinipa historia ndefu juu ya hilo eneo nikisema niandike ntawachosha. Ila kwa ufupi tu alisema hilo ni eneo ambalo lina wenyewe ati sio langu pamoja na kwamba nalimiliki watakuja kunitfuta siku moja.
Na alidai kuna watu wanakuja maeneo ya jirani kila mwaka kucheza maeneo hayo.
Na kila mwaka hapo tunaokota maiti moja mwisho wa mwaka huwa haijulikani kwanini inakuwa eneo lile na hata wakiitoa hiyo maiti huwa inarudi hapo mpaka baada ya siku saba inapotea yenyewe .Na aliniambia kuwa kama mi ni mzito basi nikae ama la niondoke tu.

Sasa inaonekana pana nguvu za giza pale mahali
.ipi njia bora ya kuepuka hilo tatizo...?

Nafikiria au yule jamaa ananidanganya ni uoga wake tu mbona kwa pembeni kuna watu wanaishi vizuri tu.?

Kwasababu eneo ni zuri sana hasa kwa watoto wangu miaka ijayo.
Au na mimi niliuze kwa mtu mwingine...

Yani nafikiria mengi hadi nakosa usingizi na pesa nimeshatoa kubwa tu.
Kuna mliokutana na shida hii mlifanyaje?
Nina swali kwako.... Umekwenda shule?
If yes; Tumia shule yako si vingine!
 
Kiwanja ushanunua kaa utulie.kama unaratiba ya kuanza kujenga endelea.
Kuhusu majini si umeambiwa yatakuja subiri yaje.
Au ukijenga Nyumba ukakuta haipo ndo utajua kuwa majini yapo kweli.
Ukisha fahamu leta mada hapa wamo wataalamu wengi humu ndani utapata majibu ya nini kifanyike.
Hili jibu lako la ki babe balaaa linakalibia kufunga huu mjadala,,

"ajenge nyumba akiikuta haipo ndo atathibitisha kuwa wapo au hawapo
 
Back
Top Bottom