Nimealikwa kuwa mgeni rasmi kwenye harambee ya kanisa.

manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,064
10,723
Husika na kichwa cha habari hapo juu, siku ya tar 29/12/2013 kutakuwa na harambee kwenye kanisa moja la K.K.K.T, Mchungaji pamoja na wazee wa kanisa wamefika kwangu kuniomba niwe mgeni rasm kwa siku hiyo ambapo 27milion zinatarajiwa kukusanywa.
Shughul hii kwa upande wangu imegeuka kuwa mzigo mkubwa kwani sina uzoefu wa shughul hii na kipato changu nikijilinganisha na waumin wenzangu pale usharikan mimi si kitu kwan kuna watu wenye pesa nying sana na ninajiuliza kwanini hawakufuatwa wao na ikawa mimi mwenye kipato cha kudunduliza?
Tumejadili na wife kwa kirefu na tukaamua kukubali ombi hilo.
Je kuna yeyote mwenye uzoefu na jambo hili ama alishawai kuwa katika nafasi hiyo hasa kwenye harambee za kanisa ili aweze toa ushauri wowote wa jinsi gan nitaweza kufanya kukamilisha jambo hili siku hiyo.

BARIKIWA.
 
Unajua kuna vitu viwili vya kuangalia kuna kuwa na hela nyingi na kuwa na moyo wa kutoa kwa hiyo wewe unaweza ukawa na hilo la pili kwamba wameshaona unaweza ukajipapasa ukaachia hapo hata ka 5m na ushawishi wako huenda umeinekana ni mkubwa then kwa wewe kutoa ka 5M basi wale wenye kipato kukuzidi wakapata changamoto wakamalizia hiyo iliyobaki.
 
Labda una mvuto
ukisimama kuhimiza hao matajiri watachanga

au unaishi kitamthilia,pesa huna lakini kwa nje umeweka image ya pesa za kinigeria..
 
Kutoa ni moyo si utajiri wameuona moyo wako usiwaze mtumikie Mungu na mali zako
 
unawez kua hauna pesa kihivyo lakini una ushwishi mkubwa kwa watu.,.ungetaja kanisa gani sasa,ili tuje
 
Mkuu usihofu kamwe hapo Mungu
ana makusudi yake lakini naamini
kabisa utaweza. Kuna siku moja
kulikuwa na Harambee sehemu moja
mgeni rasmi alikuwa DC.

Mtazamo wa wengi ni kuwa Mgeni rasmi
atoe zaidi ya wengine lakini uzuri na cha
kuvutia sana mgeni rasmi alitoa kiasi
kulingana na alivyojiandaa.

Basi wengine walitoa pesa zaidi kulingana
na walivyohamasishwa na mgeni rasmi
 
tafuta rafiki zako hata nje ya usharika unaosali wakusindikize angalau kila mmoja asikose 500,000/= kama cash au ahadi na wewe jipige angalau utoe 1,000,000/=. Usikatae wito
 
Rahisi sana ukifika pale juu Vua koti lako la suti ambalo ndani ya mifuko weka kama laki 5 tu hivi alafu omba walinadi kuanzia laki 5 kwa masharti atakaenunua anapata na pesa zilizomo ndani ya koti.

Hii aliicheza Dingi yangu zamani sana wakati nipo shule ya msingi ingawa yeye aliweka elf 30 tu koti liliuzwa kwa 90. Akawa keshatoa mchango wake na MC alipamba kwa shangwe kwelikweli wakati mabosi wanagombania koti.
 
Husika na kichwa cha habari hapo juu, siku ya tar 29/12/2013 kutakuwa na harambee kwenye kanisa moja la K.K.K.T, Mchungaji pamoja na wazee wa kanisa wamefika kwangu kuniomba niwe mgeni rasm kwa siku hiyo ambapo 27milion zinatarajiwa kukusanywa.
Shughul hii kwa upande wangu imegeuka kuwa mzigo mkubwa kwani sina uzoefu wa shughul hii na kipato changu nikijilinganisha na waumin wenzangu pale usharikan mimi si kitu kwan kuna watu wenye pesa nying sana na ninajiuliza kwanini hawakufuatwa wao na ikawa mimi mwenye kipato cha kudunduliza?
Tumejadili na wife kwa kirefu na tukaamua kukubali ombi hilo.
Je kuna yeyote mwenye uzoefu na jambo hili ama alishawai kuwa katika nafasi hiyo hasa kwenye harambee za kanisa ili aweze toa ushauri wowote wa jinsi gan nitaweza kufanya kukamilisha jambo hili siku hiyo.

BARIKIWA.

Ukiona hivyo ujue wenzio wamekataa ndiyo maana umefuatwa wewe.
 
Sijui naota !naona kama nipo MMU !
anyway waliokualika wana mapenzi na wewe mtumikie BWANA!
 
Back
Top Bottom