Nimeagiza simu mtandaoni imefika walichonifanyia TRA leo sitokaa nisahau mpaka nakufa

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Niliagiza simu mtandaoni kwa aliexpress na ikatumwa kwa njia ya posta kama kiparcel tu

Cha ajabu mzigo nikitrack uliandikwa upo held by custom.

Nikaenda posta leo kuufata nikaukuta posta wakanambia nilipie 5900 nikalipia.

Cha ajabu nikaambiwa mzigo nichukulie ofisi za TRA hapo hapo posta.

Nilivyofata mzigo akaja huyo afisa wa TRA akaja na hiyo simu akafungua akasema natakiwa nilipie kodi 35900
Yaani elfu thelathini na tano na mia tisa!

Hapo tayar posta washanipiga 5900 ya kulipia hiyo simu

Nililalamika mno haikusaidia mwisho akanambia niondoke siku nitakayokuja kupata hiyo hela nitaenda kukomboa hiyo simu.

Roho imeniuma mnoo tra nyie ni wanyonyaji tena wanyonyaji wakubwa nyie sijawahi kuona unyonyaji mkubwa kama huu

Hebu imagine hiyo ni simu tu vp kuhusu mfanyabiashara akiagiza simu nyingi?si ndio wanapigwa kodi hadi wazimie?

Leo kuna mzee mmoja hivi nadhani wa kizungu naye alikuja kufata mzigo wake pale
Akalipa 5900 ya posta cha ajabu viparcel bei 2,230 lakini unalipishwa 5900

Baada ya kulipa akawa anasubiria simu cha ajabu tra wamemkadiria kodi kubwa mnoo hadi akawauliza kwamba inakuaje alipe kodi tena wakati tayari posta washamchaji 5900? Alichojibiwa ni kwamba hiyo ni kodi lazima alipe kwani hata mtoto anayezaliwa au hata aliyepo tumboni analipa kodi

Nimeumia sana nikikumbuka hiyo simu nilivyopoteza muda wangu kufatilia posta bado imekaa kama siku 40 njiani na nimelipishwa hiyo elfu 41800 nimeumia mnoo hii nchi imefika pabaya kama mambo ndo haya.

TRA KWA HILI SITOSAHAU SASA NAELEWA KWANINI WATU WANAENDA KUWEKEZA NCHI NYINGINE WANASUSA BONGO YETU
 
Kama simu Ni 180,000 ongeza shipping. 10,000 ongeza insurance 3000. CIF ya simu Ni 193,000 .

193,000*18%=34,740
Ofisa wa TRA Yuko sahihi kabisa Tena anastahili pongezi kwa kulitumikia taifa lake kwa uadilifu.

Kalipe hiyo pesa ndani ya siku 21 vinginevyo itapigwa mnada na itauzwa Kati ya sh 40,000 na 50,000.

Angalizo.....usitegemee kuinunua kwenye mnada kwani maofisa watainunua kwa sh 45,000
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom