"nimeachwa nimepata mwingine" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"nimeachwa nimepata mwingine"

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Dec 17, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,512
  Likes Received: 5,744
  Trophy Points: 280
  Nimeachwa, nimepata mwingine!

  Mimi na wewe milele Duniani kuna wakati wa kutoa machozi, wakati wa kucheka, wakati wa kuhuzunika, wakati wa kufurahi, wakati wa kuchukiwa, wakati wa kupendwa, wakati wa kuponya nk.


  Kama umewahi kupendwa na mwanaume au mwanamke then akakupiga chini bila sababu za msingi au kwa mgogoro mkubwa, ukweli hali hii huumiza na huweza kuzidi maumivu ya operation hospitalini kama si kuwa na mawazo hadi unanusurika kugongwa na magari barabarani.
  Kupendwa kutamu na kuacha kuchungu !  Ni kawaida kujisikia huzuni, kuvunjika moyo, kujisikia hatia na hata kuwa na siku za machozi na hata kushindwa kufanya kazi kama kwenda kazini maana love is greater than faith and hope.  Ni kweli uliwekeza muda wako wote hata rasilimali zako kuhakikisha unampa umpendaye kile ambacho kinatoka ndani ya moyo wako, hata hivyo amekukimbia na kukuacha.  Ni kweli umeumizwa, umekasirishwa, hata unajiuliza una tatizo gani hata hivyo jambo la msingi ni kumshukuru Mungu kwamba sasa una nafasi ya kusahihisha makosa na kwamba alikuacha kabla ya kuwa ndoa hivyo una nafasi nzuri zaidi kufanya maamuzi ya kweli.


  Wengine akishaachwa, kwa haraka anajiingizwa mahusiano na mtu mwingine ili kuziba pengo au nafasi iliyoachwa wazi moyoni na kuendelea kumlaumu aliyeachana naye kwamba ndiye alikuwa chanzo na sababu.

  Kabla ya kuingia kwenye mahusiano mapya ni jambo la msingi kuwa makini zaidi kwani unaweza kuingia kwenye mahusiano mapya na ukagundua kwamba umefanya terrible mistake kuliko mara ya kwanza ukaishia kujuta zaidi nakujikuta umebadilisha sura, rangi, kimo na shape hata hivyo mwanaume au mwanamke ni yuleyule na tabia zake.

  Data zinaonesha kwamba ukiwa na mahusiano na yakavunjika ukienda haraka unaweza kuishia kwa mtu wa aina ile ile na kuendelea kuumizwa zaidi.

  Maswali mawili ya msingi kujiuliza kabla ya mengine ni kwanza je, nitawezaje kumpata mwingine ambaye hataniumiza kama yule wa kwanza?


  Na pili je, nitawezaje kubadilika na kuwa mtu mwingine tofauti na nilivyokuwa mara ya kwanza kabla ya mahusiano kuvunjika?

  Tunatakiwa kujifunza kutokana na mahusiano ya kwanza na kujua tulihusika vipi kusababisha mahusiano kushindikana au je ni kitu gani kinatakiwa kubadilisha?


  Yafuatayo ni maswali ya kujiuliza kabla hujaingia kwenye mahusiano mapya
  Je, nimekuwa na muda wa kutosha kuponya (heal) majeraha yangu kabla sijajiingiza kwenye mahusiano mapya?
  Je, nimefahamu kwa nini mahusiano ya kwanza yalivunjika?
  Je, nimebadilika katika tabia, mitazamo, maneno, kufikiria na mawazo yangu kabla ya mahusiano haya?
  Je, nipo wazi na huru katika mahusiano haya ninayotaka kuanza?


  Tumeshaongelea malengo ya baadae, dini, pesa?
  Je, nataka kuanza mahusiano mapya kwa sababu ni mpweke au nataka kufanya naye mapenzi au namuhitaji sana kifedha, au ni mtu sahihi kwangu?


  Je, nimemuomba Mungu
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Duh ume copy na kupaste sio?
  Naona kama sio yako vile Mama mia
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,046
  Likes Received: 24,047
  Trophy Points: 280
  Leo huyu mama ameamua kufungua mathread ya kukopi na kupesti kwa wingi! Agriiiiii!
   
 4. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  [​IMG] No comment,
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,367
  Likes Received: 22,229
  Trophy Points: 280

  ajidhaniaye amesimama aangalie asianguke.
  unaweza ukapata halafu ukaachwa tena na ukajikuta hupati ila unahangaika na website za kuwatafutia watu wenzi.
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,512
  Likes Received: 5,744
  Trophy Points: 280
  Duh ume copy na kupaste sio?
  Naona kama sio yako vile Mama mia

  ANS

  BWANA NDIYE MCHUNGAJI WANGU SINTOPUNGUKIWA NA KITU." ZABURI 23
   
 7. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  haya Mama Mia. Hapa mimi umenipiga stop kabisaaaaaaaa
   
 8. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #8
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,046
  Likes Received: 24,047
  Trophy Points: 280
  Badili avatar yako mama!
   
 9. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hili iendane na title yake ya 'Mama' hii title ina heshima bana
   
 10. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  hater!
   
 11. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  hater...
   
 12. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,046
  Likes Received: 24,047
  Trophy Points: 280
  Nimemwomba mara nyingi huyu mama anayejiita mtumishi wa Mungu! Avatar yake haiendani na anavojiita! Otherwise lazima atakuwa nabii wa uongo huyu!
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,046
  Likes Received: 24,047
  Trophy Points: 280
  Lover!
   
 14. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  whatever, you can say that again...
   
 15. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #15
  Dec 17, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  na leo ndio deadline ya kubadilisha otherwise nitkubaliana na wewe hapo kwenye bold
   
 16. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #16
  Dec 17, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  haujui ulitendalo!
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,512
  Likes Received: 5,744
  Trophy Points: 280

  msamehe huyo

  waacheni wafu wazike wafu wao
   
 18. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #18
  Dec 18, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,367
  Likes Received: 22,229
  Trophy Points: 280
  jamani yeye analisubiri treni kwa hamu.
  ana uhuru wa kuelezea hisia zake
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,250
  Trophy Points: 280
  Isije ikawa treni ya RITES. Utasubiri forever!:confused:
   
 20. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #20
  Dec 18, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,250
  Trophy Points: 280
  Mama Mia,
  In this case ningekuwa mie ningejitafuta kwanza (Mh, fnamaanisha find yourself first). Jipe break like a year hivi, have fun, discover who yoy are, make new friends etc. Wenzio ndo tunapataga na pHD hivyo hivyo. Kila degree ilikuwa solution ya frustrations hahaha!
  Move on. He is not worth that, may be he was not meant to be in the first place! Pandisha vioo, God has greater plans for you!
   
Loading...