Nimeachwa na mpenzi sababu anataka tuishi pasipo ndoa (sogea tuishi)

Kama mwanaume hawezi kuoa basi hawezi kulea mtoto, narudia kama mwanaume hawezi kuoa, hawezi kuhudumia mke, hana uwezo au hata ujasiri wa kufanya maamuzi kuwa sasa naoa basi jua huyo mwanaume hawezi kulea mtoto. Hii Makala ni kama narudia lakini kwakua ukiingia kwenye inbox yangu nina meseji karibu elfu moja na kila unapofungua meseji kumi tatu zinakuambia mwanaume amenitelekeza basi naomba niirudie hata kama nakuchosha.

Kuna wanaume wanadhani ni rahisi kulea mtoto, ni kweli ni rahisi kama huyo mtoto hatataka kula,. Kama hataumwa, kama hatavaa na kama hatataka kwenda shule. Ukipata mtoto wa namna hiyo aisee ni rahisi na hakuna mwanaume anashindwa kulea. Lakini kama ni hawa watoto ambao wanakula, wanakunywa, wanaumwa nakuambia ndugu yangu kama mwanaume hajawa na ujasiri wa kukuoa, akakuambia nizalie tu nitalea basi jua kuwa siku akianza kuumwa anakukimbia.

Majukumu ya mtoto ni makubwa kuliko ya mke, mtu unaweza kuoa ukamuambia mke wako leo tupige deshi hakuna chakula mkavumilia, akaumwa ukamtafutia mitishamba mambo yakaenda. Lakini mtoto akija, akiumwa kwanzai hakuna cha mitishamba lakini chakula sio kwamba tu atataka lakini pia atachagua na chakula, kama maziwa atataka yale ya elfu 18, haya ya lita elfu mbili hataki na wala hajali chochote.

Hii ndiyo maana wanaume wakiona tu nugumu kidogo hukimbia, tena wengina hata mtoto hajazaliwa, ile tu mwanamke kila siku kuumwa, hospitali mimba inasumbua, sijui bedrest na mavitamin na mambo hayo anakimbia kwani anapakukimbilia. Lakini dada yangu mimba umebeba wewe, tena jamaa mjanja kabisa anasubiri mpaka mimba ikifikisha meizi sita anajua hapa hawezi kutoa akitoa anakufa ndiyo anakimbia hapokei tena simu zako.

Yaani mara nyingi wakinipigia simu nawauliza lini kaanza kukimbia, wengi kama si miezi sita ni saba na wachache miezi minne, ni ngumu kuona mwanaume anatakaa mimba ya wiki mbilili kwani hapo anajua kuwa unaweza kuitoa dakika mbili tu. Ukiona anaikataa ya wiki mbili jua hata mtoto alikua hataki, wewe mwenyewe umejibebesha umehsindwa kuhesbau tarehe basi, lakini kwa wale wanaokuambia nataka mtoto dada yangu wewe beba tu.

Ile mikiki mikiki ya miezi sita ikianza hutamuona, yaani atatafuta sababu ya kugombana na wewe mpaka basi. Nakuamb9ia hivi ujue kuwa kama hawezi kukuhudumia kama mke basi hawezi kukuhudumia kama Mama wa watoto wake. Tena hapa mnielewe, unajua sisemi labda mwanaume ana hela u la, mwanaume kuhudumia mke haina uhusiano na hela, hapana bali ni ule utayari wa kubeba majukumu.

Kwamba usijipe moyo kuwa yeye ana hela basi atahudumia, hapana huhitaji kuwa bilionea kuhudumia mtoto. Kinachoshidna wengi ni zile kero za mtoto hivyo wengi wanakua hawako tayari na kukimbia. Hembu jiulize tofauti ya kuoa na kuzalisha mwanamke. Kuoa inamaana anakuchukua wewe mtu mmoja, mnaishi naye tena mtu mzima anakuhudumia wewe na kama ni kero basi ni zako mwenyewe.

Lakini sasa kuhudumia mtoto nialzima uhudumie watu wawili, kwamba ili mtoto ashibe ni alzima mama ashibe, ili mtoto awe na furaha ni lazima mama awe na furaha hivyo ni sawa na kuoa mara mbili. Sasa kama hawezi kuoa hiyo mara moja hiyo ya pili ataiweza wapi? Nimalize kwa kusema na kurudia tena nyie ambao mnaniuliza hili swali kila siku kuwa kaniambia tuzae kwanza? Jibu ni moja zaa kama unataka kuwa single mother ila kama ni kuolewa dada yangu hapana!

Si semi wote hawaoi hapana wapo wengi tu wanaoa lakini wakati anakuambia kuwa umzalie kwanza unatakiwa kujua kuwa hajapanga kukuoa, atapanga huko baadaye, anakuambia umzalie kwakua anjua unaweza kulea basi. Naomba leo nimalizane na hii mada, sikukatazi kubeba mimba ila beba ukijua kuwa huyo unayembebea hatataka umsumbue huko mbeleni, siku akichoka kulea na kuondoka basi uwe tayari kulea pake yako na si kusumbua watu wa ustawi wa jamii!

Iddi Makengo facebook

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu kuna jambo linanitatiza.
Nimekuwa na mahusiano kwa miaka miwili sasa huyu mwenzangu anataka tuchukuane kimya kimya (sogea tuishi) pasipo ndoa rasmi. Anaeleza kuwa baada ya mimi kwenda kwake wazazi wake waende nyumbani kwetu kutoa taarifa kuwa nimeolewa!

Kwa upande wangu nimejaribu kumueleza kuwa siyo jambo la busara mimi kufanya hivyo nahofia wazazi wangu kusononeka (nitakosa baraka za wazazi)

Nimejaribu kumweleza tutambulishane rasmi tufunge ndoa simple tu isiyokuwa na shamrashamra ila amekuwa mgumu kuelewa.

Ameamua kuniacha kisa nimekataa kuolewa kimyakimya pasipo kuwaeleza wazazi kuwa nimepata mchumba.

Bado nampenda sana nifanyeje ili tuweze kufikia suluhu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabla ya kushauri ni vema nikajua miaka yenu kwanza

Ukiendelea kumfuata
Atakujaza halafu akutelekeze

Husiseme sikuambiwa baadae
 
Asipoichukua hii point na kuifanyia kazi basi yajayo yatamfurahisha
Acha ujinga. NEVER compromise your values kwa ajili ya ujinga wa aina hiyo hata siku moja.
Huyo most likely anataka kukutumia tuu (naongea hivi kwa experience binafsi kama mwanaume). Mwanaume anaekupenda from the bottom of his heart, hawezi kufanya hicho anachofanya jamaa yako.
Stick to your values, do not degrade yourself kisa tu kuolewa (tena bila utaratibu).
Upendo iswa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umechana mulemule, huyo jamaa anataka kuchakata mtambo tu

Back
Top Bottom