Nimeachwa na mpenzi sababu anataka tuishi pasipo ndoa (sogea tuishi)

Upendo iswa

Upendo iswa

Senior Member
146
250
Wakuu kuna jambo linanitatiza.
Nimekuwa na mahusiano kwa miaka miwili sasa huyu mwenzangu anataka tuchukuane kimya kimya (sogea tuishi) pasipo ndoa rasmi. Anaeleza kuwa baada ya mimi kwenda kwake wazazi wake waende nyumbani kwetu kutoa taarifa kuwa nimeolewa!

Kwa upande wangu nimejaribu kumueleza kuwa siyo jambo la busara mimi kufanya hivyo nahofia wazazi wangu kusononeka (nitakosa baraka za wazazi)

Nimejaribu kumweleza tutambulishane rasmi tufunge ndoa simple tu isiyokuwa na shamrashamra ila amekuwa mgumu kuelewa.

Ameamua kuniacha kisa nimekataa kuolewa kimyakimya pasipo kuwaeleza wazazi kuwa nimepata mchumba.

Bado nampenda sana nifanyeje ili tuweze kufikia suluhu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAWAZO UJENZI

MAWAZO UJENZI

JF-Expert Member
2,401
2,000
Njoo PM tuyajenge,pia niliachwa kama wewe,demu hataki ndoa,sogea tukae yuko radh
 
Dr. Wansegamila

Dr. Wansegamila

Verified Member
1,995
2,000
Acha ujinga. NEVER compromise your values kwa ajili ya ujinga wa aina hiyo hata siku moja.
Huyo most likely anataka kukutumia tuu (naongea hivi kwa experience binafsi kama mwanaume). Mwanaume anaekupenda from the bottom of his heart, hawezi kufanya hicho anachofanya jamaa yako.
Stick to your values, do not degrade yourself kisa tu kuolewa (tena bila utaratibu).

Asante mkuu mimi nimekuwa na huo msimamo sasa ameamua kuniacha kisa tu sijakubali kuolewa kimyakimya pasipo kuwapa taarifa nyumbani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dr. Wansegamila

Dr. Wansegamila

Verified Member
1,995
2,000
Asante mkuu mimi nimekuwa na huo msimamo sasa ameamua kuniacha kisa tu sijakubali kuolewa kimyakimya pasipo kuwapa taarifa nyumbani

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa ndo unataka ulegeze msimamo ili akurudie?
Usifanye hilo kosa. Utakuja kulilia chooni. I am telling you.
Kama kweli atakuacha kwa kusimamia huo msimamo, kuwa na uhakika (I can assure you by 100%, though hautaamini coz you are blinded by love), kuwa huyo mwanaume NEVER LOVED YOU. So, be happy for that!! Upendo iswa
 
Siwezi legeza huu msimamo wangu ni kitu ambacho hakiwezekani ila napenda anielewe umuhimu wa kufunga ndoa rasmi , pia atambue nahitaji baraka za wazazi wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
gwankaja

gwankaja

JF-Expert Member
5,459
2,000
Mwanaume anayekupenda kweli hawezi kukwepa process wala kuogopa gharama, hapo jamaa yupo na ww ili siku ziende tu.
Alafu inaonekana wewe ndo unampenda zaidi, ukikubali huo ujinga kwanza atakudharau!!

NB: Ongea naye vizuri na uweke msimamo wako, mkishindwana njoo kwangu tuyajenge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads
1,424,948

Messages
35,076,913

Members
538,170
Top Bottom