Nimalizieni ubishi kuhusu mpira wa kurushwa

kyatamato

JF-Expert Member
May 14, 2015
387
269
Wana sport, nisaidieni kwa hili swala
hivi, mpira wa kurushwa , ukirushwa moja kwa moja golini bila kuguswa na mchezaji yeyote na ukatinga nyavuni inakuwa Goli au sio Goli????
make kuna utata Hapa…
 
Nenda kasome sheria za soka km haipo basi watafute waamuzi wenye beji ya fifa akina Israel nkongo
 
We goli la wapi hilo unajua mpira wa miguu toka lini goli likafungwa kwa mikono au si mpira wa miguu unaozungumzwa hapa
 
Hilo ni Goal sababu, mpira ukisha rushwa unakuwa upo mchezoni ivo ukiingia goloni ni goal bila shaka!
 
hilo litakuwa goli La mkono na kwenye mpira hakuna goli La mkono ila ungemgonga mtu lingekuwa goli
 
Mpira wa kurushwa ukiingia golini bila kuguswa ni Goli maana kurusha kwa mikoni nitofauti na mpira wa kuucheza kwa mkono ambayo ni faul so ni moja ya mchezo
 
Nenda kasome sheria za soka km haipo basi watafute waamuzi wenye beji ya fifa akina Israel nkongo

Israel Nkongo .. kibinafsi simjui… nafanyaje ili nimalize ubishi?? au wewe unaamuaje kama wewe ungelikuwa Refarii??
 
Nigoli mkuu wala usiwaze,mpira wakurushwa kwa mikono huwa unarushwa wkt mchezaji yupo nje ya uwanja lkn ukishaingia ndani mpira sio wamikono tena.
 
aasilimia kubwa naona wanasema lina kuwa goli halali
so nimalize ubishi?? au kuna mwenye evidence zaidi?? nisije haibika… hapa..
 
Wana sport, nisaidieni kwa hili swala
hivi, mpira wa kurushwa , ukirushwa moja kwa moja golini bila kuguswa na mchezaji yeyote na ukatinga nyavuni inakuwa Goli au sio Goli????
make kuna utata Hapa…

Sio Goli hlo, kwa tukio kama hlo inategemea huo mpira unalushwa upande gani, kama unarushwa upande wa goli la mpinzani basi Ref. anatakiwa aweke goal kick ila kama unarushwa upande wa mrushaji basi Ref. anatakiwa aamuru corner ipigwe katika upande huo huo wa goal la mrushaji... Kumbuka hii ni katika ule mrusho wa moja kwa moja pasipo mpira kuguswa na mtu yoyote yule
 
Feyenoord score illegal goal straight from a throw-in against Standard Liege, hiyo habari ipo ktk Mail online
 
Back
Top Bottom