Niliziona hisia za Daktari huyu

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,658
22,255
Jana usiku nikiangalia taarifa ya habari ya kituo kimoja cha runinga kulikuwa na habari zilizohusu hosipitali mbili za jijini Dar es Salaam. Jambo moja kubwa la kutisha ni pale dakitali mmoja alipoongea kwa hisia kubwa.

Dakitari huyo alisema idadi ya akinamama wanaopeleka watoto kwenye chanjo hosipitali imepungua! Akinamama wanaokwenda kiliniki wamepungua! Na watu wanaokwenda hosipitali kwa ajili ya tiba wamepungua!

Najua baadhi ya watu wanahofia kuambukizwa maradhi baada ya kuona watumishi wa hosipitali wanavaa barakoa, lakini pia wako ambao wameondoa imani kwenye tiba za hosipitali, hali hii inaleta mashaka ya afya ya mama na mtoto hapo baadae.
 
Hofu, pamoja na kuwa ni kweli Covid 19 ipo na inaua ila tunatiana hofu saanaa
Ni ugonjwa unaowakumba watu wengi kwa pamoja, na hauna tiba hata vifaa vya kukusaidia usukume siku ni vya shida. Siku moja nilikwenda hosipitali moja jijini lakini nilikataliwa kuingia bila barakoa.
Maisha yangu ni jukumu langu.
 
Nadhani msimamo wa Rais wetu mnaujua. Ni kutaka siku moja tusiwe na dawa zilizotengenezwa na wazungu. Tiba zote ziwe kwa mitishamba.

Katika jamii za usukumani, hasa maeneo ambayo kwa haraka unaweza kusema ni primitive, mpaka wakati huu, wapo wanaokataa kabisa kutumia modern medicine, na wengine wanakataa hata kutumia vyoo wakieleza hawawezi kuchanganya kinyesi cha baba na mtoto! Kwa hiyo mambo mengine mnayoyashuhudia kutoka kwa viongozi wetu wa awamu hii, ni matokeo ya malezi/mazingira ambayo mtu amekulia.

Nimesafiri kwenye maeneo ya vijiji vya ndani kabisa usukumani, kuna baadhi ya maeneo hata wakiwekewa zahanati, huwaoni wagonjwa, lakini nenda kwa waganga wa kienyeji, wale wapiga ramli, utakuta watu wamejaa unafikiri kuna mkutano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani msimamo wa Rais wetu mnaujua. Ni kutaka siku moja tusiwe na dawa zilizotengenezwa na wazungu. Tiba zote ziwe kwa mitishamba....
Ni kweli mkuu Kuna Kijiji Misungwi ,karibu kabisa na mjini...Mwaka 2015 Zahanati haikuea na Choo!

Daktari anaenda kujisaifia mashine ya mpungs...aisee!

Na hiyo Zahanati Ina miaka 20+
 
Ni kweli mkuu Kuna Kijiji Misungwi ,karibu kabisa na mjini...Mwaka 2015 Zahanati haikuea na Choo!
Daktari anaenda kujisaifia mashine ya mpungs...aisee !
Na hiyo Zahanati Ina miaka 20+
Kwani wanaotakiwa kujenga choo ya Zahanati ni wasukuma au Serikali ?
 
Tembea usukumani yote hautaona popote kuna bango la mganga wa kienyeji ila hapa Dar kika Nguzo ya Umeme ina bango la mganga.

Unataka kusema hapa Dar kuna wasukuma wengi kuliko Usukumani ?
Kule wanajulikana hakuna haja ya mabango!
 
Hili la watu kutokwenda hospitali lilikuwepo hata mwaka jana kipindi hofu ya corona imetanda ila hofu ilipoondoka na hili suala likarudi kama kawaida,watu wenye magonjwa ya prsha na moyo walikuwa hawaendi kwenye clinic zao kwa kuhofia watapata corona huko hospitali. Ila sasa tumeanza kutishana na hiyo hali inarudi tena hata leo asubuhi hii hii kuna mtu ananiambia anajisikia kuumwa anahisi malaria,nikamwambia nenda kapime akaniambia sasa hivi hospitali sio pakwenda hovyo hovyo bora akanunue dawa za malaria ameze bila kupima kujua kama kweli ana malaria.

Kwahiyo tuachane kutishana.
 
Back
Top Bottom