Nilizani bia aghari nikarudi katika komoni kumbe ni aghari zaidi.

Midavudavu

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
287
59
Bia baada ya kupanda hadi 1800/= nikarudi katika vikao vyetu vya mzunguko wa kopo moja la komoni kwa wachezaji 12. Tukaagiza kopo la ltr 4, yaani amboni. Tukaanza kubugia, mimi nilikuwa namba 10. Ngoma ilipofika kwangu nikaipuliza kwanza kama kawa halafu nikaitikisa. la haula!nilichoona ndani ya ile pombe sikuamini. Mjusi mkubwa alikuwa amefia ndani ya ile pombe tena inaonekana alikufa siku nyingi maana alivimba na kuchubuka ngozi. wasela wakaanza kunikolomea"oya kunywa basi tumalize mzunguko twende wa pili". Nikawambia naomba niimwage hiyo pombe maana kilichomo ndani ambao weshakunywa wasikione. wakang'ang'ania niwaonyeshe kabla sijaimwaga. Baada ya kuwaonyesha wakaanza kutapika kila mmoja wao; kama ndio unafika kwa mara ya kwanza unaweza kufikiri hapo palikuwa zahanati na waliokuwa wanatapika walikuwa wagonjwa.
 
wewe umetumwa na makaburu udhalilishe chimpumu ili wa maximize faida kwenye bia
 
Back
Top Bottom