Massa
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 647
- 794
Habari za jioni wapendwa,
Kuna inshu inanitatiza kuhusu mzazi mwenzangu.
Ni kwamba nilizaa nae mtoto miaka 13 iliyopita alafu tukaachana baada ya yeye na familia yake kudai hawezi kuwa na mimi maana kwetu na mimi mwenyewe masikini choka mbaya. Na kweli tulikua choka mbaya baada ya mzee kutumbuliwa enzi za Nyerere.
Sasa tatizo lake ni kwamba kizazi kwake kimekataa kabisa yaani tokea alipo achana na mimi baada ya miaka mitano akaolewa mpaka leo hajapata mimba.
Anasema wameenda hospitali na wote wako poa yeye na mmewe. Sasa amekuja kwangu nipo na mke wangu na watoto wawili + mwanae na mwingine yupo njiani ananiambia nimsahidie ili apate mtoto nae labda kuna kitu nilifanya na anasema labda kutokana na tulivyoachana kwa masimango labda nilifanya chochote kibaya.
Ingawa ukweli sikufanya lolote baya kwake na wala sina hata wazo hilo.
Ndugu zangu naomba ushauri hivi sasa yupo kwangu siku ya tatu leo yeye na mme wake ingawa mme yuko kwa ndugu yake sio mbali na kwangu.
Yaani mke analala kwetu mme analala kwa ndugu zake