Niliyoyashuhudia nikiwa ziarani Wilayani Tarime Mkoani Mara

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,206
4,698
Niliyoyashuhudia nikiwa ziarani Wilayani Tarime Mkoani Mara

Ziara yangu ya muda mfupi kanda maalumu imenipa uzoefu wa mambo kadhaa ambayo sikuyajua hapo awali!

Hata hivyo nitataja kwa uchache yale yaliyo mema na ya kuvutia!

Kwa upande wa chakula

1.Uji wa ulezi halisi uliochanganywa na maziwa halisi pamoja na karanga mbichi gharama yake tshs 700

2. Lita moja ya maziwa flesh kabisa na yanayopatikana kwa wingi tshs 800-1,0003.

3. Ndizi za tshs 500 mnakula watu 2-3

4.Ugali wa udaga, nyama choma na kichuri tshs 1,500

5. Matumizi ya maziwa mgando na karanga ni makubwa sana

6. Wakazi wa huku ni wakarimu sana upande wa chakula!

Kwa upande wa mavazi

1. Nimetathmini sana uvaaji hasa watoto wa kike!

2. Wengi hupendelea magauni na kanga na chini hupiga raba

Sio rahisi kuona mtoto wa kike amepiga pamba za kisasa!

3. Wengi wamefunga kitambaa kichwani au kusuka au kutokusuka bila kuweka dawa

4.Sio weledi kwenye mazu gumzo na wagumu kuele
ewa somo ( hawana kabisa romantic language)

Matumizi ya lugha

1. Wakazi wengi hawana soft au romantic language kabisa!


Kwa ujumla nimefurahia ziara yangu Kanda maalumu japo sikubahatisha kupata mnyama hata mmoja!
 
Ugomvi ugomvi? Wanatembea na silaha? Usafiri mkuu hapo town? Bar? Wadada watoa huduma? Elimu madogo wanaenda shule?
 
Generally tunapenda wageni, hasa wanyenyekevu. ukileta maringo tunatafuta jinsi ya kukukomoa.

Hali ya hewa ni nzuri mno tarime ukilinganisha na mikoa mingi.

Hatuchumbiani barabarani, ukimpenda msichana ulizia kwao ni wapi ukaongee naye huko kwao, anakukataa au kukukubali hapo kwao
 
Fika Musomo Town Hapo Mkendo Ule Raha
Ugali Wa Ukweli Na Samaki
 
Hivi kuna basi la Dar to Tarime? Au unafika kwanza Musoma ndio unaenda Tarime?
 
Back
Top Bottom