Niliyoyashuhudia kwenye mkutano wa injili wa Mwamposa Moshi

Nazani kakutuma humu kumtetea. Ishu iko lazima ukifika wasalimie waumini wako, wapungie mkono, yeye hicho hafanyi. Ishi sio kuingia na Gari kali bali salimia kabla ya kuanza mkutano.

Sikiona akisalimia
Umaskini kitu kibaya mno kwa hiyo ulitaka aingie na bodaboda ndio roho yako ifurahi? halafu pale ni sehemu ya ibada ulitaka aingie akipunga mikono? ule haukuwa mkutano wa siasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siwezi enda tena. Kule ni shetani ndo yupo pale hakuna kitu pale.
Usiende, sababu hata ulipoenda hukwenda kusali bali ulienda kama mshtaki ibilisi, farisayo na sadukayo ukitafuta umshtaki Mwamposya kwa lipi.Toka mwanzo hadi mwisho hukuwa kusali ulikuwa kupeleleza kama mshtaki ibilisi uone ni kipi upate kumdhalilisha Mwamposya,Hukwenda na roho ya ibada

ulienda na mapepo yako na ukatoka nayo usirudi nayo tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi najua kuna huduma ya ukombozi hasa kwa wale watu ambao wana matatizo sugu ya kishirikina, kiukoo, mapepo na mengine. Kwa huduma maalumu ndio hutumika vitu ka vile mafuta, chumvi, unga, udongo n.k kumfanyia mtu huduma ya ukombozi. Hii ninewahi kuishuhudia mwaka 2010.
Kuna mzee alipagawa na nguvu za giza (mapepo) akapelekwa kwa mwinjilisti mmoja wa kilutheri (kkkt) baada ya kuonekana hana ugonjwa kutoka hospital. Yule mgonjwa aliombewa kwa wiki mbili ila hakupata nafuu, Ndipo akafanya hiyo huduma ya ukombozi.
Walichukua unga wa mahindi, mafuta ya kupikia, chumvi, udongo, maji, n.k. ila vitu vyote vilitoka kwa nyumbani kwa mgonjwa anakoishi.
Likasomwa neno, vitu vikachanganywa vikaombewa, na akaja kuombewa mgonjwa ndipo akapona na fahamu zikarudi, maana alikua hajielewi hata watoto na mke wake akikua kawasahau.
Ila hii huduma ya kuuziana mafuta mafuta, cjui ya upako, vitambaa vya upako, Maji ya upako n.k nashindwa kuamini Kabisa kiukweli.
Nitakua mtu wa mwisho kuinywa hii Chai maana ya moto sana.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huduma ya delivarance au kufungua waliofungwa ni tofauti na huduma ya mahubiri ya kawaida uliyozoea.UNAONA watu wa delivarance wengi huwa na walinzi hicho wewe hukushangaa? Wale walinzi kazi yao kubwa ni kumlinda mtumishi asije vamiwa na wapandisha mapepo au vichaa waliokuja kufunguliwa

Kwa nini huanza delivarance moja kwa moja na sio kuhubiri kwanza?
KUNA mhubiri toka Nigeria alienda marekani kuhubiri ni mhubiri mkubwa tu .Wenyewe wamarekani waliposikia ni mhubiri mkubwa mwenye jina kubwa wakasema njoo wakamlipia kila kitu .LAKINI KWA siri wakapanga kumpima kama kweli ana nguvu za kiroho na ufahamu wa kiroho

wakampeleka kwenye semina akakuta ukumbi umefurika watu wamekaa .Akakaribishwa aanze huduma yake akafungua Biblia akaanza kuhubiri akahubiri kama dakika kumi mwenyeji akasema inatosha.TUONDOKE akaambiwa live kuwa hawamtaki hayuko kiroho.
sababu nini ilikuwa?

wote waliokuwepo ukumbini walikuwa viziwi walichukuliwa sehemu mbali mbali wakaletwa kwenye semina wakamtegeshea wakasema huenda atalijua hilo awafungue kwanza ndipo aanze kuhubiri ,yeye kafika tu na BIBLIA yake kaanza kubwabwaja kwa viziwi

Na hawakumwambia akawauliza kwa nini mlinijaribu wakajibu neno la Mungu linaturuhusu kuzijaribu roho ndio maana tukakujaribu tukakuona huna uwezo wa kiroho kama unavyosifiwa

Watu wenye mapepo kuanza kuwahubiria kwa mtu wa delivarance huwa haaanzii huko

Ni kweli mikutano ya Mwamposya wengi huwa biblia hawana pia sababu wengi HUWA ni waislamu sio wakristo

yapo mengi tu ila cha msingi ujue kuna tofauti kubwa kati ya huduma ya deliverance na hii ya kuhubiri tu kwa kutumia Biblia
Curious...

Mtumishi hata hakuwa anawaambia BWANA asifiwe au alikuwa anapata response gani??

So mwanzo mwisho alikuwa akiongea mwenyewe?

Changes
 
mkuu, mbona hujasimulia wakati wa watu kukanyagana ? from what i heard kuna mama mmoja yeye anasema alianguka chini akawa akijaribu kuamka anapigwa ngumi na vijana

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kuna mmoja alisema eti alipokanyaga mafuta alihisi Kama sumaku vile akashindwa kunyanyua mguu ndo watu wakamkanyaga ila yeye hakufa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siwezi enda tena. Kule ni shetani ndo yupo pale hakuna kitu pale.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakubaliana na imani yako ila kwa kuwa ni yako na katiba ya nchi imekupa Uhuru wa kuamini chochote

Na Mimi kea mujibu wa imani yangu wewe Ni shetani mshtaki wa watu wa Mungu na imani yangu juu ya Mwanpsya naiaona ya Mungu na ya kwako naiona ya kishetani .Hiyo ni kwa mujibu wa imani yangu
 
Ila hii huduma ya kuuziana mafuta mafuta, cjui ya upako, vitambaa vya upako, Maji ya upako n.k nashindwa kuamini Kabisa kiukweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivyo ni vifaa vinavotumika kwenye ibada ya ukombozi Kama unavyouziwa vitabu vya mwimbieni Bwana KKKT au hivyo vitabu mnavyotumia kwa ibada huwa mnapewa bure?
 
Yesu mwenyewe alikuwa na mabaunsa 12 mitume wake.POPOTE alipoenda alienda nao
kuna siku alivamiwa baunsa wake petro akatoa kisu chake akamkata sikio mtu
Yeesu anayekuwa potrayed kwenye makanisa siyo Yesu wa kwenye Biblia. Yani Yesu wa kwenye biblia alikuwa kama outcast, alikuwa ni yule mtu ambaye kampani yake ni wale watu ambao jamii inaowaona wamepotea yani sawa na mateja zama hizi. Yani alikuwa mwana wa masela ndiyo maana utaona walikuwa wanajuliza kwanini jamaa anakula na kukaa na wenye dhambi? Yani ilikuwa ni sawa nabii wa masela (gheto gospel)
 
Nilifanikiwa kuhudhuria mikutano miwili siku ya Ijumaa na Jumamosi. Kuna vitu nilivishuhudia ambavyo kwa kweli kama Wakristo tunapotoka sana.

1. Kwenye mkutano hakuna aliyekuwa amebeba Bible-Hiki ndo kitabu cha mwongozo kwa Wakristo ila pale sijaona mtu mwenye bible.

2. Mtumishi alivyo mkuwa anafika Jukwaani anaanza na watu watoe shuhuda. Nilishangaa sana kwa kweli badala watu wahubiriwe wokovu mtumishi anaanza na watu wenye shuhuda.

3. Watoa shuhuda wana utata sana. Baadhi ya miujiza ina utata kwa kweli. Mmoja wa mtoa ushuhuda alidai baada ya simu yake kuombewa na Nabii alitumiwa pesa laki 2 na baada ya kufika nyumbani akakuta na mume wake ametumiwa laki 3 kimiujiza.

Hakufafanua alitumiwa na nani hasa. Je ni alikuwa anadai mtu? Je kuna ndugu yake alimtumia? Je ni Vodacom walimtumia? Je ni pesa ilitumwa kimakosa kwake? Hapa kuna utata.

4. Watoa shuhuda wengi ni wanawake na hasa kwenye mambo ya uzazi.

5. Mtumishi anasisitiza sana watu watoe sadaka ile noti yenye thamani.

6. Mpaka naondoka siku ya pili sikusikia sehemu mtumishi anahubiri kuhusu watu waache dhambi, watu wawe wema, watu wajiandae na kurudi kwa yesu mara ya pili. Haya sikuyasikia kabisa.

7. Ni sehemu chache sana mtumishi alikuwa anatumia bible. Mahubiri yake mengi ni juu ya mikosi, kurogwa na kadhalika.

8. Mkutanoni mtumishi aliuza sana stika, mafuta ya upako, Jarida lake na Maji. Sijajua maji kama ni kampuni yake.

9. Mtumishi alikuwa anaingia na V8 tinted na hakuna cha kupungia hata waumini mkono.

Kwa kuhitimisha sasa.

Kwa kweli zile shuhuda nyingi ni za kupangwa watu wanapangwa watoe shuhuda.

Baada ya ule mkutano nimeapa.kutokwenda kwenye mikutano ya Manabiii.

Kwenye kukanyaga wese ya upako mimi niliwahi kukanyaga wa kwanza kwanza hivyo wakati majanga yanaanza tayari nilikuwa nje ya uwanja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aliwaambia ukishakanyaga nini kitatokea na je kimekutokea?
Asante!

Hawa manabii wetu,wengi ni matapeli,waumini wakilokole,wajaribu kuwaangalia pastor,John Hagee,TD jakes,Myles Munroe,
Hakuna madudu ya kukanyaga mafuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huduma ya delivarance au kufungua waliofungwa ni tofauti na huduma ya mahubiri ya kawaida uliyozoea.UNAONA watu wa delivarance wengi huwa na walinzi hicho wewe hukushangaa? Wale walinzi kazi yao kubwa ni kumlinda mtumishi asije vamiwa na wapandisha mapepo au vichaa waliokuja kufunguliwa

Kwa nini huanza delivarance moja kwa moja na sio kuhubiri kwanza?
KUNA mhubiri toka Nigeria alienda marekani kuhubiri ni mhubiri mkubwa tu .Wenyewe wamarekani waliposikia ni mhubiri mkubwa mwenye jina kubwa wakasema njoo wakamlipia kila kitu .LAKINI KWA siri wakapanga kumpima kama kweli ana nguvu za kiroho na ufahamu wa kiroho

wakampeleka kwenye semina akakuta ukumbi umefurika watu wamekaa .Akakaribishwa aanze huduma yake akafungua Biblia akaanza kuhubiri akahubiri kama dakika kumi mwenyeji akasema inatosha.TUONDOKE akaambiwa live kuwa hawamtaki hayuko kiroho.
sababu nini ilikuwa?

wote waliokuwepo ukumbini walikuwa viziwi walichukuliwa sehemu mbali mbali wakaletwa kwenye semina wakamtegeshea wakasema huenda atalijua hilo awafungue kwanza ndipo aanze kuhubiri ,yeye kafika tu na BIBLIA yake kaanza kubwabwaja kwa viziwi

Na hawakumwambia akawauliza kwa nini mlinijaribu wakajibu neno la Mungu linaturuhusu kuzijaribu roho ndio maana tukakujaribu tukakuona huna uwezo wa kiroho kama unavyosifiwa

Watu wenye mapepo kuanza kuwahubiria kwa mtu wa delivarance huwa haaanzii huko

Ni kweli mikutano ya Mwamposya wengi huwa biblia hawana pia sababu wengi HUWA ni waislamu sio wakristo

yapo mengi tu ila cha msingi ujue kuna tofauti kubwa kati ya huduma ya deliverance na hii ya kuhubiri tu kwa kutumia Biblia
Waislam tena?????
Una lako mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mikutano ya Mwamposya wengi huwa biblia hawana pia sababu wengi HUWA ni waislamu sio wakristo.... Ila wee jamaa weee... Haya bana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mathayo 17:24-27
27 Lakini ili tusiwaudhi, nenda baharini ukatupe ndoana. Mchukue samaki wa kwanza utakayemkamata; mfungue kinywa chake nawe utakuta fedha zinazo tosha kulipia kodi yangu na yako; ichukue ukawalipe.”

Fedha za manabii wa kisasa zinatumika kwenye kujenga mansions, magari ya kifahari nguo, pete, viatu vya kifahari, nk. Watoto wao wanaishi maisha ya anasa watu wa parte after parte...after parte after parte...!!!

Wakati huo huo waumini wao wanaishi kwenye umaskini!!!
 
Hayo yote ulikua unayaona na ukaenda zaidi ya siku mbili na mafuta ukakanyaga!
Mi huyo jamaa mambo yake mengi sijakubali, ila mahubiri yake hasa yale ya asubuhi kwenye tv "Inuka na Uangaze" ni ukweli na yanabariki.
 
..................Usijumlishe jamii yote kwa kusema “WAKRISTO TUNANAPOTOKA SANA” ukiwaweka na wale walio timamu vichwani mwao na wanaojua thamani ya Imani ya Kristo,sema “SISI TUNAOJIITA WAKRISTO HUKU HATUJUI TUNAABUDU NINI TUNAPOTOKA SANA”

Ni ujinga na wendawazimu kama mtu unaweza kwenda kuchomwa na jua kiwanjani kumsikiliza mjanja mjanja mmoja akinyofoa baadhi ya vifungu vya Biblia na kuwadanganya watu na kuwauzia baraka,eti anauza maji na mafuta ya baraka mikate ya baraka juzi sijui ni huyu niliona pic's za chvpí kwamba wale walio wagumba wazinunue wavae watajaaliwa uzao,hivi kweli nyie waumini mna akili sawasawa kweli vichwani mwenu???

Kwa sababu anawaona mapoyoyo juzi akaona awape home work ya kufanya ili mjue thamani ya Imani zenu akawadanganya mkagombanie kukanyaga mafuta aliyomwaga chini mmeenda kama nyumbu akaondoka hapo na ishirini,ninini mnafanya ni njaa ama nini?shida zimezidi?Imani haba mnapenda miujiza na mnataka kufanikiwa kwa kuombewa na mtu,mkiambiwa fanyeni kazi hamtaki huku maisha mazuri mkiyataka mnatamani muendeshe magari na kujenga nyumba nzuri kwa kuitikia tu Aminaaa,Aminaaa huku mikono mmeiinua kwa juu.

Hiyo paragraph ya mwisho nashangaa kwanini upo hapa,hata wewe unayeaminika kusoma kwenye ukoo wako unaamini upuuzi wa kukanyaga mafuta?Mungu anisamehe ila ningekuwa Israel na wewe nisingekuacha lazima kingeeleweka siku ile,Mungu hafanyi kazi kibwege hivyo otherwise asingeweka kitu maarifa kwenye bongo za wanadamu amkeni.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Chakusha ngaza hao hao wachungaji huwa wana wacheka nakuwaita wapumbafu ila hawa elewi hao hao wachungaji eti unasikia watu wajinga eti wanataka vitu vyabule wakati wao wenyewe Wana vitaka jamanii walokole mmezidi kuweni kiakili Mungu Ni imani yako tu jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom