Niliyoyaona Kwenye Kongamano la Vijana Chadema: Kadi 20, Mwanamke Mmoja!!

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Ziliandaliwa kadi mpya 20 kwa ajili ya vijana wapya waliojiunga na Chadema.

Katika hao 20, kulikuwa na mwanamke mmoja tu.

Hii ni changamoto kama si tatizo. Lazima tung'amue na tuchukue hatua na mapema.

mimi naumia sana nikiona mwanamke wa Tanzania anazurura mchana kutwa na kibeseni cha mihogo huku amefunga kiremba cha CCM kichwani.

(Lazima tuwaelimishe au 2015 tuwanyang'anye shahada za kupigia kura ili wasipige kura kama walivyofanya majita wa Mwanza)
 
Na imagine, hapo palikuwa eneo la vijana WASOMI, ambao wanategemewa ndio wangekuwa msitari wa mbele kubadilika, hasa baada ya kung'amua haki zao.
Nimemsikia Dr Mkumbo akiwaasa kuwa hakuna kitu kama kuwa NEUTRAL katika politiki. Ni lazma uwepo upande fulani wa mfumo kuonyesha msimamo.
Ukiona msomi anakuwa mwoga, basi ujue haku'grasp vema nadharia aliyoshehenezwa, hivyo ana shaka kuibadili kuwa MATENDO.
 
Manajamii mwenzangu... unaweza kumlazimisha punda aende mtoni lakini huwezi kumlazimisha anywe maji.. tatizo hapa ni tatizo la kutokujua haki zao za msingi wanafikiria kuwa kuna watu waliumbwa na mwenyezi Mungu kuwa masikini kizazi chao chote mpaka mwisho wa dunia na kuna watu waliumbwa kula raha siku zote..... sasa hatua ya kwanza iwe kuwasaidia kuwapa elimu ya utambuzi... :disapointed:
 
Usifadhaike mkuu, mimi binafsi sina kadi ya Chadema, kiufupi si mwanachama wa chadema, kadi yangu ya chadema nimeihifadhi moyoni mwangu, kuwin politics hakuhitaji rundo la wanachama bali wapenzi wenye mapenzi mema, ccm ilikuwa inajitamba kila siku ina wanachama millioni tano je wako wapi hao wanachama millioni tano? amini amini ninachokuambiaitikadi ya kweli itatoka moyoni mwa mtu, kuna matapeli wengi tu wana kadi karibu za vyama vitano tofauti. simba na yanga zingekuwa zinategemea wanachama wao zingeshakufa siku nyingi. huo ni mtazamo wangu tu, niko tayari kukosolewa.
 
Itakuwa vigumu sana ku-encourage wakinamama kujiunga na chadema simply nikutokana na misingi mbovu ya chama chenyewe, sio tu tatizo la ukabila na udini bali pia siasa dume.

Kuitisha uchaguzi halali ndani ya chama ni kitu muhimu kabla yakung'ang'ania ikulu
 
Uchaguzi halali ni upi? mbona chadema ilifanya chaguzi na viongozi wapo madarakani kihalali? je msajili wa vyama vya siasa anaweza kuruhusu viongozi wakae madarakani ambao sio halali? kweli ukiwa ccm hata kunguru anaweza kukuzidi kifikra.
Kifuta jasho: Nitajie safu nzima ya uongozi wa ccm Taifa walichaguliwa na nani?
 
Ziliandaliwa kadi mpya 20 kwa ajili ya vijana wapya waliojiunga na Chadema.

Katika hao 20, kulikuwa na mwanamke mmoja tu.

Hii ni changamoto kama si tatizo. Lazima tung'amue na tuchukue hatua na mapema.

mimi naumia sana nikiona mwanamke wa Tanzania anazurura mchana kutwa na kibeseni cha mihogo huku amefunga kiremba cha CCM kichwani.

(Lazima tuwaelimishe au 2015 tuwanyang'anye shahada za kupigia kura ili wasipige kura kama walivyofanya majita wa Mwanza)
Swala hapo nikwamba hao wanawake walikuwepo?afu lazima uelewe Mtu halazimishwi kuwa Mwanachama au kuchukua Kadi ya Chama hadharani cha Msingi ni ule Ujumbe na Elimu walioupata hapo huo ndo unabakia unaishi katika fikra za Mtu na Mtu wanamna hiyo anakuwa yuko Tayari kufanya Mabadiliko baada yakujitambua juu ya unyonyaji na maisha magumu anayoishi chanzo chake ni nini.Kwangu Kadi haisound saana its just an Option.
 
Sio mbaya mkijifariji kama kadi hazikuuzika. Ingekuwa hapa JF zisingetosha.
 
Ziliandaliwa kadi mpya 20 kwa ajili ya vijana wapya waliojiunga na Chadema.

Katika hao 20, kulikuwa na mwanamke mmoja tu.

Hii ni changamoto kama si tatizo. Lazima tung'amue na tuchukue hatua na mapema.

mimi naumia sana nikiona mwanamke wa Tanzania anazurura mchana kutwa na kibeseni cha mihogo huku amefunga kiremba cha CCM kichwani.

(Lazima tuwaelimishe au 2015 tuwanyang'anye shahada za kupigia kura ili wasipige kura kama walivyofanya majita wa Mwanza)

This is kind of thinking that alienate women from your party. How in this day and age suggest kwamba wanawake wanyang'anywe haki yao ya msingi. Chief, are you out of your mind? Daaamn.

Tone down the rhetoric on Anna Makinda, Mama Salma, Celina Kombani. Wanawake wanawasikia mnavyowasema vibaya and it reflects badly on Chadema.

One more thing. You should also send Ms. Mushumbusi to solicit women votes.
 
Mbona wanaume hawakususia kwasababu ya Rhetoric kwa RA,EL,Cheng,n.k. !
Mimi naamini wanawake wanauwezo sawa na wanaume tatizo lao ni kujiamini. Akina Regia, Halima Mdee mbona wapo hapa JF na wanaheshima kamili. Kama tunaweza kuwasifu akina Asha Rose Migiro, Bibi Titi Mohamed, Getrude Mongela, Akina Thabita Siwale, Kate Kamba, na wengine wengi, kwanini tusiwaseme akina Anna Makinda na Kombani kwa ubovu wao. Hawasemwi kwasababu ni wanawake bali viongozi wasio na vision. Tena kama ungalijua hawa wanawadhalilisha akina mama kwa utendaji wao pengine ungeunga mkono hoja.
Mimi nadhani hili ni changamoto kwa akina Regia/Halima n.k kwenda kuwahamasisha wanawake kujiunga katika siasa, kwasababu anayedhani siasa haigusi maisha yake anahitaji matibabu haraka.
 
Kati ya jamii ilyo katika hali dunia ni wanawake, panahitajika mpango mkakati kuwakomboa, ama sivyo, hivyo vilemba vya chichiem, haitoki kichwani mwao.
 
Sio mbaya mkijifariji kama kadi hazikuuzika. Ingekuwa hapa JF zisingetosha.

hatuko kiushabiki hapa wewe.

we are trying to address a problem here. and that should be handled by chadema people, not you arrogant ccm puppets.
 
Katika wale 20 waliochukuwa kadi waliwakilisha wenzao. kwani waliopaswa kupewa kadi walikuwa 300 pia kuna wale kadhaa walirudisha kadi za ccm na cuf na kujiunga na chadema, Kuwa mwanachama wa chama fulani kadi ya uwanachama inakuidentify hivyo lakini unaweza kuwa mfuazi wa chama fulani ambopo si lazima uwe na kadi kama nionavyo mimi CDM inawafuazi wengi ambao siyo wanachama na ndiyo siasa ya vyama vingi ilivyo.
 
hata huyo mmoja ni mafanikio makubwa. Kumbuka hakuna pesa zilizotolewa kuwahonga, wala hakukuwa na bolingo/bongo fleva na magari ya kuwasomba watu.
Kwa vile wanawake wengi si watu wa mabadiliko, si jambo la kushangaa sana. Ipo siku watajua kuwa wanadhulumiwa kwa maneno matamu yaliyopo sasa
 
Ushauri...CDM waanzishe movement ya kuwaelimisha kina mama kuhusu siasa na yanayoendelea nchini.Wengi sana hawafahamu!
 
Wanawake wengi wa Dar wanaipenda Ccm kutokana n vijizawadi vya kipuuzi wanavyopewa na kutokana na woga walionao kwa serikali. Waige mfano wa wenzao wa Arusha walivyohamasika.
 
Hawa ccm vp!!? Hawajiulizi kina BIBI TITI walikuwa wangapi kati ya ile midume? Wanawake ndivyo walivyo (Adam first then Eve/Hawa). Kasome misaafu.
 
Mkuu Ngwanangwa hilo lisikupe shida mkuu.
Kadi za CCM watu wanazo mfukoni kwa ajili ya kuombea kazi na kupandishwa vyeo makazini lakini mapenzi yao hayapo kwa ccm wala kura hua hawa wapigii ccm!!

Wanaishi kwa ujanja wakisubiria ccm wamalize muda wao 2015.
 
Hata IMANI yako ikiwa ndogo kama punje ya haradali. Wewe uambie mlima "ng'ooka", utang'oka tu! Ivi umemsahau Nyerere? Ilihitaji nyerere wangapi kumtia adabu mkoloni? Tafakari!
 
Back
Top Bottom