Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,646
- 35,981
Nilikuwa napita jioni kuelekea job. Si mnajua night shift zetu walinzi ndugu zangu. Nilikuwa nimempa lift mfanyakazi mwenzangu tukitokea Chanika.
Sasa nafika NMB Gongolamboto nikiwa barabarani jamaa akaniambia ona ile foleni, nikacheki kushoto nakuta foleni ya haja. Nikakumbuka kuwa ni tarehe ya mshahara. Mimi tayari nishatoa kwa simu, nina karibu mwaka siijui ATM machine.
Kwanini niseme niliyoyaona ni aibu kwa watumishi wa umma?
1. Hivi enzi hizi bado mtu na akili zake timamu anapoteza muda kwenye foleni huku makato ukitoa kupitia internet au sim banking yanalingana. Huu muda unaopotea kuokoa mia 4, buku au mia 5 mtu haoni ni hasara.
2. La pili linalotia aibu ni kwamba watumishi wengi wameambatana na wadeni wao ambao ndio walimiliki ATM card zao mpaka siku ya mshahara.
Jamaa yangu aliniambia wale waliokaa kwenye mawe ni wadau wanaowakopesha watumishi na kumiliki kadi zao na kuwapa siku ya mshahara wanapokutana kwenye ATM.
Nikafanya utafiti kuhusu hilo na kujihakikishia kuwa ni kweli. Aibu hii itaisha lini?
Serikali ipeleke wataalamu wa fedha na uchumi kwenye taasisi zake ili kuwafunda watumishi. Pamoja na maslahi ndogo ila mambo mengine yanatokana na ujinga (kukosa elimu ya kiuchumi na fedha) kwa watumishi.
Mtu anashindwa hata kui sacrifice laki 3 kujitosa kwenye ufugaji wa kuku. Aibu.