Niliyoyakuta na ninayoyaona uraiani bora nirudi tu chuoni nilikotoka

kesho kutwa

JF-Expert Member
Dec 7, 2016
1,086
2,000
Ni mwezi wa 6 sasa Toka nimalize chuo mwaka wa 3 mnamo mwaka Jana mwezi wa 8.

Pigo la kwanza nilinunua ngurue ili nifugiwe nyumbani kwa lengo kwamba nikirudi nije kuwauza nije fanya biashara.

Nimerudi nimekuta ngurue wote wa3 wameuzwa na niliahidiwa Kua nitalipwa pesa.. Nimekopwa Toka mwaka Jana nimerudi kutoka chuo sijapewa.

Nikiuliza naambiwa ooh sisi ndo tumekusomesha tulia dogo. Sio hilo tu nilijibana nikiwa chuoni nikaja kuuanzisha biashara ndogo tu.. Lakini licha ya biashara Kua ngumu mtu anachukua bidhaa bila kulipa ukiuliza eti sisi ndo tumekusomesha tulia.

Kila nikitia jitihada kadhaa kujishugulisha nahisi naumia tu for nothing. Wakuu naomba kuuliza hata nyie mliosomeshwa mnakumbana na changamoto kama hizi? Je mnazikabili vipi? Aisee bora tu nirudi chuoni sio kwa maumivu haya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jan 16, 2019
31
125
Tatizo la vijana wengi wa kitanzania ni kuwa wanapokuwa chuo wanaona maisha wameyapatia sana na badala yake huwaona walioko mtaana hawana ajira ama kabiashara chochote cha kujikimu maisha kuwa ni wavivu kwakuwa hataki kijishughulisha . Ndugu yangu kwakuwa na wewe ni mhitimu wa chuo na uko jikoni(uswahili) jaribu kutafuta mbinu mbadala kwa bidii sana ili uweze angalau ujikimu kimaisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Bulaya001

JF-Expert Member
Dec 21, 2018
5,196
2,000
hii hata mimi imenikuta sana, ila naamini haya mambo yapo familiar zetu za kimaskini lakin loyal families hakuna mambo kama hizi, wazazi wengi rich wanakuwa hawana njaa pia wanaheshimu jitihada za mtoto!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom