Niliyoyafanya tangu niwe Mbunge-Shukrani kwa WanaJF

Status
Not open for further replies.
Mkuu nashukuru sana.Napenda kujibu maswali yako kwa kifupi sana Kama ifuatavyo;
1. Kwamba ningependa kubaki kuwa Mbunge ama napenda majukumu makubwa zaidi jibu ni kuwa sijui kwa sasa. Hali ya kisiasa ndio huamua destiny ya Wanasiasa wengi.
2. Nimeyafanya haya kwa kuwa niwajibu wangu kuyafanya hayo.Nimelelewa katika kutimiza Wajibu wangu. Rekodi yangu tangu nimeanza Kazi CHADEMA inajionyesha wazi ni mtu wa kutimiza wajibu na Mnyika alinifundisha kurekodi na kuripoti kila ninachokifanya. Hivyo niwajibu wangu kuyatimiza haya niliyoyafanya na kuweka wazi in public kwani hakuna Siri wala ubaya katika kuripoti uliyoyafanya.

Thanks




Mimi nina kaswali, je ungependelea kubakia kuwa mbunge ama unadhani unaweza majukumu makubwa zaidi?

Je haya uliyoyafanya na kuya mention, ni kwasababu unataka ubakie kuwa mbunge, upate nafasi ya juu zaidi, ama ni moyo yu umekutuma kuonyesha jinsi unavyowatumikia wananchi bila kutegemea kuwa utachaguliwa tena?

Je kama usipochaguliwa tena ni kweli kuwa hutajali licha ya kuwafanyia wananchi hao mambo yote hayo? Would you hold grudges for it happend the second time?

Sitll naamini kama ni kweli hayo uliyomention hapo juu ni kutokana na jitihada zako, basi hii itatufanya pia tuwaulize kina Zitto na wengineo kama they can do the same.

Shida niliyonayo na wanasiasa ni kwamba they do something in order to get something of move value to them...
 
Dada regia namba 8 barabara ya kidatu ifakara naomba uendlee kuipigania nikilometa chini ya sabini lakini kwa ubovu wake unatumia masaa zaidi ya mawili hata matatu kipindi cha mvua ndio kabisa aifai ukiwa na gari dogo unaweza lala njiani.wekeni mkaka na wabunge wenzako mama kombani na dk mponda tena ni mawazi wanashdwaje kuharakishia maendeleo wananch wao.congratulation dada and happy new year,office ya cdm ipo wapi maeneo ya kibaoni feb nitakuja uko!

Mkuu barabara ya Kidatu - Ifakara - Mlimba iko kwenye ilani ya CCM kwa ajili ya kuwekwa lami.Nadhani iko kwenye MCHAKATO
 
Mkuu nashukuru sana.Napenda kujibu maswali yako kwa kifupi sana Kama ifuatavyo;
1. Kwamba ningependa kubaki kuwa Mbunge ama napenda majukumu makubwa zaidi jibu ni kuwa sijui kwa sasa,Hali ya kisiasa ndio huamua destiny ya Wanasiasa wengi.
2. Nimeyafanya haya kwa kuwa niwajibu wangu kuyafanya hayo.Nimelelewa katika kutimiza Wajibu wangu.Rekodi yangu tangu nimeanza Kazi CHADEMA inajionyesha wazi ni mtu wa kutimiza wajibu na Mnyika alinifundisha kurekodi na kuripoti kila ninachokifanya.Hivyo niwajibu wangu kuyatimiza haya niliyoyafanya na kuweka wazi in public kwani hakuna Siri wala ubaya katika kuripoti uliyoyafanya.

Thanks




QUOTE=jmushi1;3060744]Mimi nina kaswali, je ungependelea kubakia kuwa mbunge ama unadhani unaweza majukumu makubwa zaidi?

Je haya uliyoyafanya na kuya mention, ni kwasababu unataka ubakie kuwa mbunge, upate

Je kama usipochaguliwa tena ni d grudges for it happend the seco
Sitll naamini kama ni kweli hayo uliyomention hapo juu ni kutokana na jitihada zako, basi hii itatufanya pia tuwaulize kina Zitto na wengineo kama they can do the same.

hing of move value to them...
[/QUOTE]
Mkuu kwa hiyo mwanafunzi anaonekana kufanya vizuri (kuripoti) kuliko mwalimu wako? Wapi Mnyika naye aripoti alicjokifanya Ubungo ili tuone anaendeleaje. Pia ni vema wabunge wengine wa CDM nao atupe update ya utekelezaji wa majukumu na ahadi kama ulivyofanya wewe hapa JF
 
Regia,

..according to Johnson Mbwambo wa gazeti la Raia mwema, kuna uharibifu mkubwa sana wa MAZINGIRA ktk maeneo ya bonde la mto KILOMBERO. vipi hili suala la MAZINGIRA umelishughulikia namna gani?

..kuhusu elimu naomba ujielekeze ktk kuhakikisha wanafunzi wa Kilombero wanapata elimu yenye viwango. msiridhike na kuandikisha watoto shule, au kuwalipia ada na karo. elekeza nguvu zako ktk kuhakikisha kwamba wanafunzi ktk jimbo lenu wanajifunza na kufanya vizuri ktk mitihani ya kitaifa.

..you r doing a great job, but I believe there is room for improvement.
Mkuu pia kuna suala la ardhi huko Kilombero watu wanagombea ardhi (hasa wageni) kama mpira wa kona. Tuangalie wananchi wa huko wasije wakawa ombaomba wa ardhi baada ya muda si mrefu. Wanapewa wageni huku wazawa tukinyimwa. Mimi nimeomba ardhi huko sijapata lakini wageni wanapewa. Mkuu Regia fanya utafiti maeneo ya Mlimba, Mpanga hadi Tanganyika Masagati ujionee mwenyewe
 
Hongera sana Mh Regia kwa kutoa mrejesho wa kile ulichokifanya,labda napenda tu kujua taarifa hizi hata kwa wapiga kura wako zimefika?maana najua watani zangu huko hata internet sio wote wana access.sijui una strategy gani ya kusambaza taarifa za haya ulofanikiwa kuyatekeleza.
Kingine nigeshauri kwa mwaka ujao ulenge masuala yanayogusa jamii kubwa na wala sio kutatua shida za mtu mmoja mmoja,nashauri uelekeze nguvu kwenye kuijengea uwezo jamii iweze kujitegemea kama ambvyo umeshafanya kwenye vikundi vya wajane na akina mama,pia jikite zaidi kwenye kero zinazoigusa jamii moja kwa moja,na uongeze nguvu ya ku-identify priority kwa njia ya mbinu shirikishi-participatory approach,otherwise nakupongeza kwa hili ulilolifanya la kutoa mrejesho.Mungu akutangulie,binafsi nina imani kubwa na future yako kisiasa kama utaendelea kutulia
 
Regia Mtema,
Hongera sana kwa kazi nzuri uliyofanya kwa kipindi kifupi.
Uongozi ni dhamana na umetudhiirishia hivyo, mpo wabunge, viongozi wachache mnaoelezea wananchi nini mmefanya, nini mtapanga kufanya kwa ustawi wa jamii na wa Taifa.
Mungu akutangulie kwa kila jambo, na heri ya mwaka mpya 2012



Wakuu habari!

Ni matumani yangu kuwa tumejiandaa kumaliza mwaka vizuri na kuplan vizuri for next year.

Tukiwa tunafunga mwaka nimeona niandike kwa kifupi yale niliyoyafanya kwa kipindi Cha mwaka mmoja tangu kuapishwa kuwa Mbunge wa Vitimaalum Nov 12,2010.

Taarifa hii inaonyesha utekelezaji wa Kazi za Ubunge,Kazi za chama Wilayani Kilombero na Kazi za Chama Kitaifa.

A. KAZI ZA KIBUNGE
Tangu nimeapishwa nimefanikiwa kufanya Kazi mbalimbali za Kibunge Wilayani Kilombero,Jimbo ambalo niligombea na kupata Kura 38,550 sawa na asilimia 45 ya kura zote zilizopigwa. utekelezaji wa awamu hii ulikuwa ni QUICK WINS. Quick zifuatazo zimefanyika;
1. Nimepigania bei ya Sukari ishuke -Kuna maeneo Bei imeshuka lakini maeneo mengine hali bado ni mbaya. Kilombero ni Wilaya inayozalisha Sukari, Kiwanda Cha Illovo hivyo bei ya Sukari unapaswa kuwa chini kuliko maeneo yasiyodhalisha Sukari.
2. Nimepigania kituo Cha Polisi Cha Wilaya kiboreshwe-kimeboreshwa
3. Nimepigania kituo Cha afya Cha Mlimba kipatiwe Maji na Ambulance lirudishwe hivi vyote vimefanyika.Ambulance ilikuwa gereji zaidi ya miezi Sita mwaka 2010.
4. Nimepigania utekelezaji wa huduma bure kwa Wajawazito,Watoto chini ya Miaka Mitano,Wazee na Wenye Ulemavu-Kuna maeneo imefanikiwa maeneo mengi bado.
5. Nimetetea haki za Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Na KPL-Baadhi ya Kero zimetekelezwa lakini nyingine bado-Suala la Maslahi bado ni tete,suala la Usalama Kazini bado ni tete.
6. Nimetetea na kusimamia kero ya Wakulima na Wafanyabiashara ya kuongezeka kwa Ushuru bila kushirikishwa katika hatua zote muhimu.
7. Nimepigania haki ya Umeme kwa Wananchi wa Kilombero kwani tunavyanzo viwili ya umeme,Kihansi na Kidatu.REA imeenda kule ila inasua sua sana lakini Wizara imetuhakikishia kuwa inatekeleza azma yake ya kupeleka umeme maeneo yote ya karibu na vyanzo vya umeme.
8. Nimepigania barabara ya Kidatu-Ifakara kwa kiwango Cha lami-imeshindikana kwa mwaka wa fedha 2011-2012.
9. Nimesomesha Wanafunzi 86 Sekondari,13 Vyuo Vikuu hawa wa Vyuo Vikuu walihitaji kutoa advance ili waweze kusajiliwa then wapate Mkopo
10. Nimeezeka madarasa mawili(2) ya shule ya Msingi Mkula
11. Nimegharamia Visima viwili vya maji
12. Nimehudumia Baba aliyekuwa kipofu kwa miaka 8 akaweza kuona tena kupitia hospitali ya CCBRT
13. Nimesaidia wagonjwa wengine zaidi ya 42 wakapata huduma za afya na kupona
14. Nimesaidia Jezi kwa Vijana katika Kata 12 Kati ya 23 za Wilaya ya Kilombero
15. Nimefanikisha ligi Mbili katika Kata Mbili-Ligi za Mpira wa Miguu na Netboli
16. Nimeshiriki kwenye fundraising katika Misikiti 3 na Makanisa 4
17. Nimekuwa sehemu ya kufanikisha Uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishirki Cha Mt Fransisco
18. Nimeshiriki kuwasaidia Wahanga wa Mafuriko Wilayani Kilombero
19. Nimefanikisha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kushirki Umitashumta ngazi ya Wilaya,Mkoa na Taifa
20. Nimefanikisha Vikundi Viwili vya kina Mama Wajane kuweza Kujiajiri na kuendesha maisha yao wenyewe.
21. Nimefanikisha Vikundi 5 vya kina mama kuweza Kujiajiri.
22. Nimefanikisha Vikundi 3 vya wenye ulemavu Kujiajiri wenyewe.
23. Nimefanya Mikutano ya Hadhara ya Elimu ya Uraia pamoja na Shukrani zaidi ya 20.

Na mengine madogo madogo mengi.

B. KAZI ZA CHAMA WILAYANI KILOMBERO

Katika kukuza chama Wilayani Kilombero nimefanikiwa kufanya yafuatayo;
1. Nimelipia na kufungua Ofisi za CHADEMA katika Kata 5
2. Nimefungua na Kuzindua Matawi 13 yaliyojengewa na yenye Uongozi wa Kudumu
3. Nimeingiza Wanachama zaidi ya 8,000

C. KAZI ZA CHAMA ZA KITAIFA
1. Nimeshiriki Maandamano ya CHADEMA Kanda ya Ziwa katika Mikoa yote ya Kanda hiyo katika kupigania haki za watanzania.
2. Nimeshiriki Maandamano ya CHADEMA Nyanda za Juu Kusini kasoro (Mikoa ya Iringa na Ruvuma) katika kupigania haki za watanzania.
3. Nimeshiriki kwenye Kazi za Siasa Arusha - Sakata la Kuvuliwa Uanachama Madiwani kusaka muafaka.
4. Nimeshiriki kwenye Uchaguzi Mdogo wa Igunga
5. Nimeshiriki kutoa Mafunzo ya Mapungufu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2011 katika Mkoa wa Ruvuma
6. Nimeshiriki kwenye Siasa za Vyuo Vikuu, Makongamano, Mikutano ya Hadhara na Uzinduzi wa Matawi
7. Nimeshiriki kwenye Siasa za Dodoma, Singida na Morogoro.

Natambua nilipaswa kuyafanya zaidi ya haya lakini kutokana na sababu mbalimbali hayo ndio niliyofanikiwa kuyafanya. Angalau nimefanikiwa kufanya karibu asilimia 70 ya niliyopanga kuyafanya kwa mwaka huu 2011 kama Mbunge wa Vitimaalum Wilayani Kilombero.

Naomba nichukue fursa hii pia kuwashukuru wanaJF wote kwa support yenu kwangu kwa hakika ninawashukuru sana tena sana.JF imekuwa ni nyumbani, JF imekuwa ni darasa, Vile vile JF imekuwa ni Tanuru la Moto maana wakati mwingine huwa ninaingizwa kwenye moto hasa. Na mwisho nichukue fursa hii kuwaomba radhi wale wote niliowakwaza kwa namna moja ama nyingine, tuanze upya mwaka ujao..

With Love
Regia
 
Maelezo ya utekelezaji yanahitaji kuandikwa kitaalam zaidi. CDM Taifa watoe format ya namna ya kutoa Taarifa za utekelezaji kwa Wabunge wake.

Hongera dada!
 
Dr Slaa nakuomba ukubali maombi ya wananchi wengi kwamba Regia Mtema anafaa kuwa mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi.Pamoja na uzuri wote wa Chadema lakini kuna udhaifu mkubwa kwenye idara hii.Kwanini lakini viongozi hamtaki kusikiliza kilio cha watu??
 
@Regia
Pia 2012 jaribu Shirkiana na wakufunzi wa SUA research zao zilizo makabatini ziwasaidie wananchi. kwa vitendo.

Naamin Uikitumia chuo cha SUA na finding za reasech zao wakulima wadogo wadogo wengi watanufaika na mazao au hata mboga mboga wanalima huko vijijini zifike sko la mjini na zipate bei bora.

Nadhani kuna reseacrh nyingi za kilimo kikubwa na kidogo na utekelezaji wake ziko makabatini zinakosa msukumo wa wanasiasa na siasa kuwanufaisha wananchi.

happy 2012
 
Dr Slaa nakuomba ukubali maombi ya wananchi wengi kwamba Regia Mtema anafaa kuwa mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi.Pamoja na uzuri wote wa Chadema lakini kuna udhaifu mkubwa kwenye idara hii.Kwanini lakini viongozi hamtaki kusikiliza kilio cha watu??
umesema kweli 100%
 
Nadhani wabunge wengine wasio wa Viti Maalumu walihitajika kuwajibika na kuwa Wakweli hata zaidi yako..lakini ndhania wako Usingizini...Hongera sana mama nakutakia maisha marefu
 
Mambo mengi tangible aliyoripoti Regia hapa ni kwa kutumia pesa zake.
Hapo tunaona kuwa posho ndio maana inapiganiwa na wabunge.
Na kwa vipimo hivi siku zote wale wenye pesa nyingi wataonekana wanaongoza vizuri zaidi. kwa mfano, akija Abood kuorodhesha misaada aliyotoa inaweza kujaza kurasa 10.
Je, tunataka kuendelea kuwa na wabunge sponsors au tunahitaji wabunge viongozi?
 
Hata kama serikali ikisema tuko tayari kufanya MOU na waislamu. Hebu orodhesha basi waingie nao MOU kwenye nini i.e Hospitali zipi, vyuo vipi ama kwa huduma gani ya kijamii wanayotoa isiyo na ubaguzi ? au wao wanataka tu kusiwe na MOU?
Mie ni mkristo lakini nakerwa sana na malalamiko ya waislam kuwa wakristo tunabebwa na MOU, kwahiyo naomba Dada regia pamoja na mambo mazuri unayofanya lakini suala la MOU lifuatilie ili waislam wasiwe na kisingizio. Mie naona serikali iondoe hata hiyo misamaha ya kodi kwasababu hakuna kitakacho haribika maana makanisa yatapandisha bei ya huduma. Nimechoka kusikiliza malalamiko ya waislam kwa vitu ambavyo tunafaidika wote.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom