Niliyokutana nayo kwenye Msiba wa Mzee wetu Maalim Seif Shariff Hamad

Ngoja tuone baada ya wiki mbili watakavyo kufa kwa sababu hawajavaa barakoa.
 
Tulifika mimi na wenzangu kadhaa wa kazini. watu walikuwa wengi hasa viongozi waliopo madarakani na pia wastaafu. Kabla sijaingia umatini nilipata muda mzuri wa kusimama nje kuangalia wageni wakifika. Wengi wao katika viongozi walio madarakani walikuwa wakivua masks zao ndani ya magari na kutoka garini kuja nje kwenye kusanyiko. Nyuso zao zilionesha huzuni,simanzi na mashaka lakini walitembea kwa ukakamavu na kujiaminisha vizuri mbele ya ndugu wananchi wanyonge.

Viongozi wachache ambao hawakuwa katika uongozi hawa walinishangaza kidogo. Wengine walishuka wakiwa wameshavaa barakoa zao na wengine walionekana kuanza kuvaa baada ya kufika sehemu ya tukio na kutakiwa kushuka. Nilihisi hawa wavaa barakoa hawa ndo wenye Corona, nikawashukuru kwa kuwa wastaarabu wasije ambukiza na wengine. Ila nikawashukuru pia kwa kuonesha upendo wa hali ya juu kuwa pamoja na kuumwa COVID19 hadi COVID20 bado wameamua kuja sehemu ya wazi kujumuika kumuaga mzee wetu lakini zaidi zaidi wameona wawakinge watanzania wengie ambao bado hawajapata "Barakoa" dhidi ya maambukizi ya Covid.

Kushoto kwangu nilimwona mwananchi mmoja mnyonge akiwa amevaa barakoa, nilitamani nimwambie avue maana niliona ile Barakoa inaweza mpa changamoto ya Upumuaji jinsi ilivyokuwa chafu,imechakaa,imekauka n.k naye alikuwa ameivaa kinadhifu kabisa ikifunika Mdomo wake na kuacha pua wazi ili asishindwe kupumua. Nikamtizama vizuri akitembeza macho huku na kule akiwa amesimama kwa kujiegesha karibu na nguzo ili iweze msaidia. Niliachana na huyu na kuamua kuelekea jukwaani sehemu yetu sisi wananchi.

Nikiwa huko pembeni yangu nilikuwa nimekaa karibu na mabwana wawili hivi mmoja akiwa busy sana na simu yake akipiga picha kwa pozi mbalimbali. Huyu wa pembeni akaanza nisemesha nadhani akitaka kupata maoni pia toka kwangu."hivi huu ugonjwa upo kweli au ni mbinu za mabeberu kutudhoofisha?" nilimtizama nikamwambia "itakuwa ni hujuma za mabeberu hasa wivu kutokana na maisha yetu na kasi ya ukuaji wetu wa uchumi."nilikunja sura yangu kuonesha machungu na hasira nilizo nazo dhidi ya mabeberu.

Jamaa akageuka kunitizama akaitikia na kusema nipo sahihi. Ila sasa akataka kujua ni nini ambacho kimemua mzee wetu? nilimuuliza kwani mgonjwa alisema anaumwa nini? Jamaa akasita kidogo. Nikamuuliza unadhani kafariki sababu ya ugonjwa wa Corona au sababu ya Ugonjwa wa changamoto ya kupumua? Jamaa akanyanyua simu yake kama anaongea na mtu....akanyanyuka kuondoka, hakurudi.

Niliondoka na kwenda kukaa karibu na wananchi wengine wakiwa wanabishana mmoja akasema huku akinitizama. "hivi si tuliambiwa tuwe tunakaa kwa umbali wa MITA 200?" niligeuka kumtizama naye alikuwa amefungua mdomo wake na kuacha meno yake nje ili aweze ona vizuri tukio lile mbele yake. Nilimtizama kisha nikageuka na kuangalia mbele alipokuwa amekaaa Rais Mstaafu J.K.Kikwete akiwa na viongozi wengine, nilipata shida kidogo kumtambua maana alikuwa amevaa Barakoa.

Wengine niliwatambua kirahisi tu akiwepo mama Makamu wa Rais, Naibu Spika (huyu nadhani ni kijana kidogo) ila yule mama Makamu naona naye si haba ni Jioni. Nikarekebisha barakoa yangu ambayo nilikuwa nimevaa ili kuepuka vumbi hasa kipindi hiki cha kiangazi nikaiweka vizuri na kushusha pumzi kwa nguvu nikageuza geuza macho.

Well, Corona si ugonjwa wa kutisha kivile ni tu mafua tu tena kama tumafua twa ndege we umewahi wasikia ndege wakipiga chafya? Ndo inavyokuwa so haiwezi mpa shida mtu kama wewe na yule.

Nikageuka na kuelekea sehemu ya kutokea nikiwaza mambo mengi kichwani. Nikamshukuru Mungu kwa yote. Nikarudi sehemu niliyofikia.

Nimejifunza mengi kwenye msiba huu wa Mzee wetu. Ila nikagundua ni mwanzo wa misiba mingine mingi hapo baadaye au mauguzo kama watu hawatakuwa wakimuomba Mungu.
Mkuu nimecheka sana
 
nimemuona mzee jk hapo na barakoa ya N95 naikumbuka slogani yake ''zakuambiwa changanya na zako"
 
Nikiwa huko pembeni yangu nilikuwa nimekaa karibu na mabwana wawili hivi mmoja akiwa busy sana na simu yake akipiga picha kwa pozi mbalimbali. Huyu wa pembeni akaanza nisemesha nadhani akitaka kupata maoni pia toka kwangu."hivi huu ugonjwa upo kweli au ni mbinu za mabeberu kutudhoofisha?" nilimtizama nikamwambia "itakuwa ni hujuma za mabeberu hasa wivu kutokana na maisha yetu na kasi ya ukuaji wetu wa uchumi."nilikunja sura yangu kuonesha machungu na hasira nilizo nazo dhidi ya mabeberu.

Jamaa akageuka kunitizama akaitikia na kusema nipo sahihi. Ila sasa akataka kujua ni nini ambacho kimemua mzee wetu? nilimuuliza kwani mgonjwa alisema anaumwa nini? Jamaa akasita kidogo. Nikamuuliza unadhani kafariki sababu ya ugonjwa wa Corona au sababu ya Ugonjwa wa changamoto ya kupumua? Jamaa akanyanyua simu yake kama anaongea na mtu....akanyanyuka kuondoka, hakurudi.
Hahaha 😂🤣
 
Kwa kifupi ulikua umevurugwa
 
Back
Top Bottom