Niliyojifunza kwenye safari yangu na Auric Air kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam

Spanishboy

Senior Member
Apr 24, 2011
118
65
Novemba 15 mwaka 2013 Shirika la ndege la Auric Air lilianzisha safari mpya za ndege za kila siku kati ya Dar es Salaam na Morogoro ikiwa ni mipango yake ya kuwafikia wananchi wengi katika mikoa mbalimbali Tanzania.

Actually, toka safari hizo zianze sikuwahi kupata nafasi ya kusafiri nao, lakini hivi majuzi tu nikitokea Dodoma kwa basi niliamua kushuka Morogoro kutekeleza majukumu yangu kadhaa. Kesho yake nilikuwa na kibarua kingine huko Dar es Salaam tena asubuhi na mapema hivyo niliona njia pekee ya kuwahi miadi yangu kutoka Morogoro ni kutumia usafiri wa ndege.

Kesho yake asubuhi nikaelekea uwanja wa ndege wa Morogoro ambao kwa kweli watu wengi hawafahamu ulipo. Hilo lilidhihirishwa na dereva tax aliyenipeleka uwanja huo, maana alikuwa hajui geti la kuingilia uwanjani hapo jambo lililofanya tuzunguke huku na kule kutafuta geti la kuingilia.

Hata tulipowauliza watu wanaoishi maeneo ya modeko karibu na uwanja huo nao hawakujua geti lilipo (hapa inabidi kufanyike matangazo ya kutosha na kuweka bando kubwa kwenye barabara ya kuingia uwanjani hapo). Lakini hatimaye tulifanikiwa kufika kwa wakati na kuketi kusubiri muda wa kuondoka ndege.

Nikiwa uwanjani hapo nilikutana na bwana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Benard Myinga ambaye ni Afisa Ugavi kutoka Tanzania Tree Seeds Agents, wasambazaji wa mbegu za miti, ambaye alieleza mtazamo wake kuhusu usafiri huo mpya wa ndege katika mji kasoro bahari.

"Hakika ni jambo jema kupata usafiri wa ndege hapa Morogoro, unajua kuna watu wengi wanamahitaji ya kufanya safari za haraka za kibiashara, matibabu na mapumziko lakini kwa muda mrefu kumekuwa hakuna huduma hiyo"

"Mfano sasa nakwenda Dar kwa matibabu ya mkono wangu ambao ulivunjika kwenye ajali ya gari nikielekea Iringa, nimekuwa nikipata tabu sana kupanda mabasi mpaka dar kwa matibabu, kwanza inachukua muda mrefu, pili mkono unarushwarushwa hivyo kuniongezea maumivu lakini inaniongezea gharama maana nikienda kwa basi siwezi kurudi siku hiyohiyo na lazimika kulipia hoteli"
Kwa maelezo hayo mafupi nilipata picha ni kwa namna gani usafiri wa ndege utakuwa msaada mkubwa kwa wanamorogoro, hasa katika kukuza uchumi, maendeleo na kuwezesha mipango ya mji huo kuwa jiji.

Safari yangu ilikuwa nzuri maana nilitumia saa moja kufika Dar es Salaam na kuwahi kufanya mambo yangu

Tazama picha.. Niliyojifunza kwenye safari yangu na Auric Air kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam - Tabianchi
 
Dar moro saa 1, je hiyo ndege ikienda mwanza si itakuwa 5 hours,

Au ikienda usa si ndio safari ya mwezi mzima
 
Wewe ndiye huyu?

13.JPG
 
JF kiboko.........ukileta uzi......jipange....la sivyo.........mmmh.....

Nikiwa uwanjani hapo nilikutana na bwana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Benard Myinga ambaye ni Afisa Ugavi kutoka Tanzania Tree Seeds Agents, wasambazaji wa mbegu za miti, ambaye alieleza mtazamo wake kuhusu usafiri huo mpya wa ndege katika mji kasoro bahari.

huyo bwana alikuruhusu uje umwanike humu JF........

"Mfano sasa nakwenda Dar kwa matibabu ya mkono wangu ambao ulivunjika kwenye ajali ya gari nikielekea Iringa, nimekuwa nikipata tabu sana kupanda mabasi mpaka dar kwa matibabu, kwanza inachukua muda mrefu, pili mkono unarushwarushwa hivyo kuniongezea maumivu lakini inaniongezea gharama maana nikienda kwa basi siwezi kurudi siku hiyohiyo na lazimika kulipia hoteli"

kwa hiyo.........?
 
Anachomaanisha mleta uzi kama unaenda moro ili kuepuka foleni za ubungo,kimara,mbezi panda ndege,umeeleweka mkuu
itabidi watu wa Auric air wakulipe kwa kuwatangazia biashara.
 
Anachomaanisha mleta uzi kama unaenda moro ili kuepuka foleni za ubungo,kimara,mbezi panda ndege,umeeleweka mkuu
itabidi watu wa Auric air wakulipe kwa kuwatangazia biashara.

Na foleni ya tazara unaikwepaje?
 
Hapa kinachoonekana ni ulimbukeni jamaa alikuwa anapanda ndege kwa mara ya kwanza kwa hiyo alitaka wana jukwaa wajue hilo,hongera sana mkuu!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom