Niliyojifunza kutoka ujenzi wa nyumba yangu ya kwanza

Yeah, ni kati ya 52M hadi 90M pamoja na fensi. Bila fensi ni kati ya 52 hadi 70M
Wewe sasa ndo unakuja na hesabu za kueleweka, sometimes gharama za finishing zinaweza kuchukua hela ndefu kuliko zile za kusimamishia boma.
 
Bati moja la futi 10 migongo mipana linaanzia 33k hadi 41k kulingana na kampuni. Na migongo midogo kuanzia 27k hadi 39k.
Kupaua nyumba ya kawaida yenye vyumba 3, sebule,dinning, stoo na jiko utahitaji si chini ya 4m kwa bati na misumari pekee. Hapo bado fundi
Mimi ya vyumba vinne vya kulala, sebule, dinning, stoo, jiko, corridor 2 na varrandar 2, choo cha master na cha public nimetumia 6 milioni sasahivi ndio nachongesha madirisha na milango miwili wa mbele mmoja na wa nyuma mmoja grill acha kabisa
 
Ukisevu 250K kwa mwezi, kwa miaka 3 ni only 9 Million. Haitoshi hata msingi wa nyumba ya vyumba 3 na makolombwezo mengine. Labda uwe na chanzo kingine cha pesa. Ila kwa laki tano na nusu kwa mwezi, ukitoa matumizi ya mwezi. Hata miaka 9 bado utakuwa unajenga. Mimi naona kujenga kutegemea mshahara pekee ni ngumu sana, labda mshahara uwe mamilioni kwa mwezi
Inawezekana ila it's a hard way,unanunua vifaa kwa kuwekeza,then unakusanya hela ya ufundi,then unapiga hatua flani,hivyo hivyo mpaka unamaliza,ndio tunavyofanya sisi wa kipato cha chini.Ila tuache tabia ya kutishana na ma bei ya ajabu ajabu,ujenzi ni gharama ila wengine wana exaggerate...
 
Kunakauli inakatisha tamaa, gharama za kupaua/za bati, zinanitoa damu...ila hapa naona kuwa ukipaua ndio unaanza ujenzi...wtf!!!si bora niache
Kuamua kujenga na kuamua kutokujenga kabisa yote ni maamuzi sahihi, inategemea na kile kinacho kuweka mjini ni nini? I mean nature ya kazi yako, kama unasubiri mshahara, please jenga, kama unafanya biashara and may be hadi watoto na mkeo umewa tune kwenye biashara hadi maisha yao yote hapa duniani then kujenga sio deal kabisa; nitafafanua sababu zote 2.
1. Kwa mtu anaetegemea mshahara ni vizuri uwe na nyumba yako mwenyewe, mambo ya kuajiriwa yana uncertainties nying sana, kuna kufukuzwa kazi, kuna kuacha tu kazi ili utafute kazi nyingine, kuna KUFA na hujaacha urithi kwa wanao na mkeo, kuna kustaafu pia; hapa sasa huna kazi (tuseme Mungu nae hajakuchukua ) unakua busy kutafuta pesa ya chakula na makazi/malazi, may be na watoto wanasoma. Mwanaume unaweza kupata KICHAA, bora utafute pesa ya kula na wanao wapo nyumbani, itakusaidia kuondoka na fedheheha ndogo ndogo hasa za majirani/wapangaji wenzio, au hata ukifa, wanao wanapo mahali pa kivuli. Wanaweza kutukanwa huko mitaani but watarudi nyumbani kwao.
2. Kwa mfanyabiashara wa level ya kati na kubwa, hawa watu kujenga sio deal kiviile, hawa ni watu ambao pesa yao yote inayopitia mikononi mwao ina hesabu, is not ideal kufukia zaidi ya Tsh 50M kwenye ujenzi ilihali hiyo pesa ikizungushwa itazaa pesa zingine zaidi, hawa watu wenyewe ni bora wapange. Kumbuka hawa ni watu ambao hata life style yao iko tofauti na mleta UZI, watoto wanasoma shule za maana, so kiwanja tu kinatakiwa kua sehemu yenye watu wenye status zao, again kwa kua pesa yao yote ina mahesabu then hata nauli za kwenda na kurudi kazini kwao wao wanazihesabu tofauti na mfanyakazi, huyu kukaa mbali sana na sehemu ilipo biashara yake sio poa, angependa kukaa karibu na biashara yake. Ndio Wahindi wanavyo ishi, huwezi kuwasikia wakifiria habari za ujenzi wa nyumba, wameachana na hayo mawazo kabisa. Zamani tulikua tunadhani eti ooh hawa jamaa, huku sio kwao ndio maana hawajengi, but mbona wanafia hapa hapa???
 
Wewe sasa ndo unakuja na hesabu za kueleweka, sometimes gharama za finishing zinaweza kuchukua hela ndefu kuliko zile za kusimamishia boma.
Ni kweli kabisa mkuu, hii mara nyingi hutegemea na quality ya finishing mtu unayotaka
 
Mkuu nyumba hizo za bei nafuu zinawezekana kwa mikoa ambayo wanatumia tofali za kuchoma na kujengea udongo baadala ya saruji. Ukienda Mafinga, ujenzi wa aina hiyo ni kawaida kabisa, gharama zinakuwa kubwa kwenye kupaua tu. Vilevile kwa uzoefu wangu ujenzi kwa baadhi ya mikoa, labour charge zipo chini sana, mtu nyumba nzima kuanzia msingi hadi kukamilisha boma ambalo halijaezekwa anakuambia laki 8. Wakati kwa Dodoma nyumba hiyo hiyo utajenga kwa labor chaji ya 3.5M hadi 4.5M. Mikoani huko, labour chaji ya kupaua unaweza kuta laki tatu tu lkni njoo Dodoma utakuta haipungui 1M
Na ndio hoja yangu ilipo, maana kuna mtindo wa watu wa Dar kuteka kila mjadala kujifanya ndio standard case.
 
Mimi ya vyumba vinne vya kulala, sebule, dinning, stoo, jiko, corridor 2 na varrandar 2, choo cha master na cha public nimetumia 6 milioni sasahivi ndio nachongesha madirisha na milango miwili wa mbele mmoja na wa nyuma mmoja grill acha kabisa
Uko mkoa gani, umetumia bati aina gani(migongo midogo au mipana) na umetumia mirunda au mbao kupaulia?
 
Pole Sana naweza kumpa ramani ya vyumba 3 na kama yuko mkoani ambako atatumia tofari za kuchoma na udongo wa mfinyanzi kujenga atatoboa vizuri tuu..

Mbao bei itategemea mkoa uliko na aina ya mbao unazotaka kutumia,mikoani kuna options nyingi sio lazima za Njombe/Mafinga.

Kuhusu nondo usikariri hujengi ghorofa unatumia 8mm unafunga 3 Kwa ringi hapo haizidi 50,000 badala ya kununua 12 mm mbili kwa 52,000..Mwisho unaweka beam ukuta wa nje hakuna haja ya Kuta za ndani hazibebi mzigo ..

Kama uko mkoani nipe 7.5m nikujengee hadi kupaua.
Duh
 
Ukipaua ndo mwanzo wa ujenzi ni kweli finishing inakung'oa kucha kuanzia plasta roughing, wiring milango tiles plumbing grils gypsum skimming me boma hadi kupaua vyumba vinne ilicost almost 38 but finishing imekula 60m plus with no fence na landscaping
 
Kupaua ni gharama kwa sababu itakuhitaji uwe na mbao na bati kwa wakati mmoja
Nikweli kabisa ila ukianza na kuweka kidogo kidogo haiwi kazi ngumu sana.
Kwa mfano halisi mimi kipindi nahitaji kupaua gharama ya kupaua jumla ilikuwa 7M (hapa inajumuisha mbao, misumari, pesa ya ufundi, pesa ya ubebaji mbao na bati kwenda site pamoja na batibati nilikuwa nahitaji Alafu kwa hiyo ni ghali kidogo na nyumba yangu ni kubwa)
Kwakua nilikuwa nikiweka pesa haijai najikuta naipunguza.
Nilifanya haya.
1. nilianza kununua bati kidogo kidogo mpaka nikafikisha idadi aliyonitajia fundi ( Na kwasabubu bati za alaf ni bora baada ya kupau hazikutofautiana rangi, zote zilikuwa rangi moja)
2. nikanunua misumari kwa idadi aliyo nitajia fundi.
3.nikalipia mbao ila sikuchukua kwa wakati huo.
4. Nikatafuta hela ya ufundi tuliokubaliana.
5. Baada ya vyote hivyo nikatafunda pesa ya akiba si unajua ujenzi unaweza kupigiana mahesabu na fundi halafu mwisho wa siku vitu visitosha. Kisha nikaanza kupau.
NOTE
Kupau kweli ni kipengele kigumu sababu kinahitaji pesa ndefu na kwa wakati mmoja na kama tunavyojua pesa haiekeki so anza na ulichonacho
 
6. Siku unayomaliza kupaua ndio ujenzi unaanza, kati ya vitu ambayo ni kuhimu katika nyumba na vina gharama kubwa ni kama mfumo wa maji, umeme, milango ya mbao na grill, hivi vitu usivichukulie kirahisi kwenye budget, gharama zake hua ni M M tu.
Hii kauli husemwa na watu wengi lakini sio kweli. Sema tu baada ya kupaua mfuko huwa unayumba sana. Hivyo matarajio ya wengi ni kuwa kazi imebaki ndogo. Sasa wanapoona wanatakiwa kutoa tena number of Milions wanachanganyikiwa na kudhani kuwa Finishing ndio gharama kulikoz hatua zingine. Sio kweli.

Fikiria gharama ulizotumia kuanza msingi, boma, renta, Mbao , bati na kupaua ni bei gani?? Ukipata pesa kama hiyo tena unamaliza kila kitu cha finishing. Sasa iweje finishing uonekane ndio ghali sana kuliko ulikotoka?
 
Ukipaua ndo mwanzo wa ujenzi ni kweli finishing inakung'oa kucha kuanzia plasta roughing, wiring milango tiles plumbing grils gypsum skimming me boma hadi kupaua vyumba vinne ilicost almost 38 but finishing imekula 60m plus with no fence na landscaping
🤣🤣🤣🤣finishing gharama mnazitaka wenyewe. Lakini haina gharama sana
 
Nikweli kabisa ila ukianza na kuweka kidogo kidogo haiwi kazi ngumu sana.
Kwa mfano halisi mimi kipindi nahitaji kupaua gharama ya kupaua jumla ilikuwa 7M (hapa inajumuisha mbao, misumari, pesa ya ufundi, pesa ya ubebaji mbao na bati kwenda site pamoja na batibati nilikuwa nahitaji Alafu kwa hiyo ni ghali kidogo na nyumba yangu ni kubwa)
Kwakua nilikuwa nikiweka pesa haijai najikuta naipunguza.
Nilifanya haya.
1. nilianza kununua bati kidogo kidogo mpaka nikafikisha idadi aliyonitajia fundi ( Na kwasabubu bati za alaf ni bora baada ya kupau hazikutofautiana rangi, zote zilikuwa rangi moja)
2. nikanunua misumari kwa idadi aliyo nitajia fundi.
3.nikalipia mbao ila sikuchukua kwa wakati huo.
4. Nikatafuta hela ya ufundi tuliokubaliana.
5. Baada ya vyote hivyo nikatafunda pesa ya akiba si unajua ujenzi unaweza kupigiana mahesabu na fundi halafu mwisho wa siku vitu visitosha. Kisha nikaanza kupau.
NOTE
Kupau kweli ni kipengele kigumu sababu kinahitaji pesa ndefu na kwa wakati mmoja na kama tunavyojua pesa haiekeki so anza na ulichonacho
Duuh hongera. Ila mimi ujenzi wa hivi unakuwa na headache miaka yoote. Kwa nini usikusanya pesa ukafanya kwa pamoja?
 
Nimefanya finishing mwaka huu January, tile hazishikiki sokoni yaani zimepanda ghafla sana.
Box moja la 50*50 ni 48K na vinakaa 7 tu.
Mara nyingi 50*50 vinakaa chache ila square mita 1.2-1.35 lakini dah kweli maisha magumu sana mimi nilinunuaga for 35,000 na kushushiwa mpka 33,000 mwaka 2017
 
Back
Top Bottom