Niliyemdhamini kakimbia kesi naomba ufafanuzi wa kisheria katika hili

sawe6

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
559
365
Nimemuwekea mtu dhamana mahakamani

Mwaka 2017. Mtuhumiwa akawa anaudhuria mahamamani. Vizuri tu .lakini mwishoni mwa mwaka Jana mtuhumiwa akakata mawasilianao na mimi na mahakamani akawa haendi.

Juzi polisi walifika nyumbani kwangu wakanikamata baada ya kufika kituoni nikaambiwa nijidhamini mpaka jumatatu nipelekwa mahakamni.

Sasa ninaomba kujua kwasheria ni mm ninaendelea na kesi kama mtuhumiwa au nitawajibika kulipa fungu la dhamana tu.

Ninaomba ufafanuzi na jinsi ya kujitetea wakuu.

Ninatanguliza shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikawaida mtu aliewekewa dhamana akakimbia basi mdhamini wake hua hawezi kubeba kesi yake hata iwe vp, ila mtu mdhamini ulazimika kulipa gharama ya dhamana kama ilivyoainishwa wakati ana muwekea dhamana au mali iliyowekwa kama bond hua ina chukuliwa.

Na baada ya hapo mdhamini hua anafanya maombi madogo ya kujitoa kuendelea kumdhamini mtuhumiwa na atakua huru baada ya hapo.

Kisheria ukikimbia ni sawa na umejikaanga kwa mafuta yako mwenyewe tu kwani kesi itaendelea kama kawaida pasipo kukusikiliza wewe au wewe kuwepo na utatiwa hatiani na hukumu ita toka kama kawaida na itakua inakusubiri uje ukamatwe ukakitumikie kifungo chako gerezani rasmi kuanzia tarehe uliyokamatwa, yaani ukikamatwa unaenda straight jela.
 
Ahsante wakili msomi hakika unatusaidia sana,Muumba akutangulie

HAPANA huwezi kujitoa kabla ya Mtuhumiwa kukamatwa
pesa/dhamana itauzwa na pesa zitatumika kumtafuta wakati ukiwa ndani labda iwe kesi ya kuku
Kesi za kujihusisha na mauaji uhujumu uchumi, nyara za Serikali, madawa Mtuhumiwa akitoroka harudi kwa hiyo mdhamini hawezi omba kujitoa
Labda mnipe hicho kifungu
 
Naaam,ahsante kujazia nyama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha msingi mtafute ulie mdhamini apatikane alaka iwezekavyo. Dhamana ni kumuamini u ae mzamini. Akivunja uzamini unabeba ulicho kubaliana na mahakama.
 
Hapo cha msingi ni kutambua.
1. Ametoroka wakati ameshatoa utetezi baada ya mashahidi kufika na kuhojiwa na mlalamikaji kutoa lalamiko?

2. Ametoroka wakati pande zote bado hazijasikilizwa?

Kwa kawaida japo mimi sio mwanasheria ila nishawahi kuwa mashtaka ambayo mshitakiwa alikimbia kabla ya kesi kusikilizwa. Ifahamishe mahakama mshitakiwa kweli ametoroka. Kisha omba muda ambao unafikiri unatosha kufanikisha kumkamata, utajaza kuna form zipo hapo mahakamani za ruhusa ya kumkamata utapeleka kituo cha polisi karibu unakoishi msako utaanza.

Ukifika mwisho wa muda ulioomba umeisha, rudi mahakamani kutoa taarifa kuwa umeshindwa. Ukiwa mtata unaweza kuomba tena muda ukitoa sababu za kwa nini unafikiri sasa hivi utafanikiwa. Ukishindwa kumpata kesi itaendelea kwa upande mmoja kusikilizwa pasipo mshitakiwa kuwepo. HAPA NI PA MUHIMU. Usilipe fungu la dhamana mpaka mahakama imtie hatiani mshitakiwa kwa maana unaweza lipa wakati mlalamikaji hana ushahidi utakao ifanya mahakama imtie hatiani.

Kwa ufupi ni hivyo kama unaona kesi ina maslahi na fungu la dhamani ni kubwa omba muda umtafute au ruhusu kesi isikilizwe pasi na mshitakiwa kuwepo ukisubiria hukumu kama itakuwa upande wako ila jukumu ni kuhudhuria mahakamani wakati wote wa kesi.

Mkuu nimekuelewa vema kwa mchanganuo wako nina imani wote na muhusika mmemuelewa huyu jamaa
 
Back
Top Bottom