Niliyemdhamini ametoroka baada ya kutolewa mahabusu

Mzolewa

Member
Dec 15, 2016
35
8
"Wanajamvi naomba msaada kwa yeyote mwenye ufahamu wa kisheria anisaidie"
Kuna mtu nilimwekea dhamana mahakama ya mwanzo kwa kosa la jinai ya kujipatia mali/huduma kwa udanganyifu baada ya kutoka selo alitoroka na juhudi za kumpata hazijafanikiwa, ili niwe sehemu salama sheria inasemaje?
 
Sheria inasema wewe ndo utabeba adhabu yake nakushikiliwa mpaka atakapo patikanaa... Mzee kesi ya uhujumu uchumi kuna dhamana kweli???
 
Bro kesi iko katika mtindo wa madai ila kwa kuwa ilianzia police ndo ikaenda mahakamani jalada likabadilika kuwa jinai
 
Sheria inasema wewe ndo utabeba adhabu yake nakushikiliwa mpaka atakapo patikanaa... Mzee kesi ya uhujumu uchumi kuna dhamana kweli???
Hiyo sio kesi ya uhujumu uchumi ni kesi ya kawaida chini ya kanuni za adhabu...
 
Hapo mkuu kesi inakugeukia. Kama vipi onana na anayedai umlipe mfanye utaratibu wa kuondoa kesi.
Shida ya dhamana ndio hiyo
 
"Wanajamvi naomba msaada kwa yeyote mwenye ufahamu wa kisheria anisaidie"
Kuna mtu nilimwekea dhamana mahakama ya mwanzo kwa kosa la jinai ya kujipatia mali/huduma kwa udanganyifu baada ya kutoka selo alitoroka na juhudi za kumpata hazijafanikiwa, ili niwe sehemu salama sheria inasemaje?
Kimbia haraka katoe taarifa mahakamani
 
Katoe taarifa polisi kabla kesi haijatajwa mahakamani ila asipopatikana itabidi ulipe kama ulivyoandikisha kwenye dhamana lakini yeye ataendelea kuwa mtuhumiwa
 
Back
Top Bottom